Wapinzani watinga Tume ya Maadili

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
Wapinzani watinga Tume ya Maadili
Maulid Ahmed
Daily News; Monday,April 21, 2008 @19:01

VIONGOZI wa kitaifa wa vyama vinne vya siasa vya upinzani wamepeleka ombi rasmi kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakitaka kukagua fomu za viongozi 11 wa juu ambao wanasema wana wasiwasi juu ya umiliki wa mali zao.

Ingawa haijafahamika lini na kama ombi lao litakubaliwa, kwa mujibu wa kanuni ya Sheria hiyo ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ikitokea wakiruhusiwa kukagua fomu hizo hawataruhusiwa kuchapisha au kutangaza kwenye vyombo vya habari au kuitoa taarifa hiyo kwa umma.

Iwapo watakiuka sharti hilo adhabu yake ni kulipa faini ya Sh 10,000 au kwenda jela miaka isiyozidi miwili au adhabu zote kwa pamoja. Ombi la kukagua mali hizo za viongozi liliwasilishwa katika Ofisi ya Sekretarieti iliyoko Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba aliyekuwa na viongozi na wanachama wa TLP, Chadema na NCCR-Mageuzi.

Barua ya ombi hilo yenye kumbukumbu CCTN/TC/DSM/UF/2008/002 iliwasilishwa kwa Ofisa Habari Mkuu wa Sekretarieti, Augustus Kariya, huku Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, Anthony Komu ambaye ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Chadema, Wilfred Lwakatare kutoka CUF, wakishuhudia.

Katika barua yao hiyo iliyosainiwa na wenyeviti wa vyama, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), Freeman Mbowe (Chadema), Mrema (TLP) na Lipumba (CUF), viongozi hao wametaja majina ya viongozi 11 ambao wanasema wana wasiwasi kwamba hawajaorodhesha mali zao kwa Sekretarieti kama sheria ya maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995.

Miongoni mwa waliotajwa ni viongozi wastaafu kadhaa na wabunge, akiwamo aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, ambaye alijiuzulu juzi kupisha uchunguzi dhidi yake wa tuhuma za rushwa na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Daudi Ballali.

Baada ya kufika katika ofisi za sekretarieti saa 4 asubuhi viongozi hao walielezwa wasingeweza kuona majalada yenye orodha za mali za viongozi waliowataja hadi waandike barua kwa Kamishna wa Sekretarieti na wakikubaliwa walipie Sh 1,000.

Kamishna wa Maadili ni Jaji Stephen Ihema. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi barua hiyo, Profesa Lipumba alisema mbali na kutaka kujua ukweli wa mali za viongozi hao, wanataka kufahamu pia kama Chenge aliorodhesha akaunti yake ya nje yenye dola milioni moja (sawa na Sh bilioni 1.2).

“Kama tutaona akaunti yenye dola milioni moja kwenye orodha tutauliza kwa nini Rais alimteua kuwa Waziri wakati amejilimbikizia mali hiyo ya rushwa…nakumbuka mwaka 1995 Mkapa alieleza mali zake lakini huyu Chenge amewahi kusema kuwa hana sababu ya kueleza mali zake..,” alisema.

Profesa Lipumba alisema watawasiliana na wabunge wa upinzani wa nchi mbalimbali za Ulaya waweze kutafuta katika nchi zao juu ya viongozi wa nchini wenye akaunti huko kwa imani kuwa viongozi wengi wa nchini wamefungua akaunti nje ya nchi na kuficha fedha nyingi ambazo zinaaminika zimepatikana isivyo halali.
 
kumbe hii tume ni kichaka cha mafisadi,hivi wanapotaja hizo mali ni kwa ajili ya manufaa ya nani ?kwani taarifa zao bado ni siri na ni siri kwa nani ?
Wito kwa wabunge tunaomba marekebisho ya hii sheria ili mali zote na uchafu wote uwe wazi kama zilivyo cv zao.
 
Hawa wakizipata hizo fomu ni vema wakazituma kwenye mtandao kama JF. Nani atajua kuwa ni wao waliozituma??
 
sasa kama hizo form hakunam tu akayeziona, whats the point ya kuwa na form hizo?
watanzania tunataka tuzijue form zimeandikaje, na kama haiwezikani kwa moja kwa moja basi mtu na azichomoe kwenye file na aturushie hapa kwenye mtandao tuone ...
 
This is a good move for opposition leaders.
Kama ipo sheria ya kuziona na kuzitangaza kwa wananchi basi ziwekwe peupe wazione.

Hizi fomu tumekuwa tukizisikia mara tu baada ya uchaguzi na kuanza kwa bunge jipya,lakini baada ya hapo ni kimya kikuu.

Hawa viongozi wamekuwepo madarakani kwa ridhaa ya wananchi kwa nini wafiche walivyochuma kwa halali???

Hizo fomu kweli ni muhimu wizara husika watutangazie kama wanavyotangaza na kunadi kwa juhudi wagombea wajapo kutuomba kura majimboni.
 
Bajeti ya hiyo Tume ni shilingi ngapi kwa mwaka?

Wanaweza kuorodhesha output yao toka ianze?

Another wastage of fedha za wananchi!
 
Back
Top Bottom