Wapinzani waipinga hotuba ya kikwete

Wapinzani waipinga hotuba ya kikwete

Habari zenu wandugu?
Naandika habari hii nikiwa na majonzi sana. Sitanii wala sina hila bali namaanisha.
Kwa muda mrefu sana Watanzania walisubiri kuona wanapata katiba mpya. Duniani kote inafahamika kuwa katiba ndio muongozo uliochaguliwa na watu wa nchi husika kuwaongoza katika mambo mbalimbali. Lakini kwa hapa kwetu sivyo.
Kwa waliokuwa wakifuatilia mchakato wa bunge maalumu la katiba na hotuba ya raisi ya jana atakubaliana nami kuwa rasimu ya katiba imetekwa. Tumeona jinsi matakwa ya kisiasa yalivyowekwa mbele hasa na chama tawala. Mimi ni mwanachama mpenzi wa chama tawala lakini lazima niseme ukweli katika hili. mimi binafsi nilitoa maoni yangu. Sasa inasikitisha kwamba tume ya kukusanya maoni ya katiba imekuja na maoni ya mwisho yaliyopatikana kwa wananchi alafu baadhi ya wajumbe na wabunge wa chama tawala pamoja na raisi walazimishe kutaka maoni ya wananchi yakataliwe yao ndio yaingizwe!!!.. hili jambo linasikitisha sana. Na nadiriki kusema huu ni utekaji wa rasimu ya katiba (Maoni ya waliowengi). Najua wengi wetu tunafahamu kitu kinachokuwa kimetekwa kinakuaje. Mtu ukiwa umetekwa hauwi huru maana yake anayekuwa na maamuzi juu yako ni yule aliyekuteka. Sasa ni juu yetu Watanzania kuamua kunyoa ama kusuka katika hili. Nasema hakika kama chama tawala kitaamua kuenda kichamachama katika hili hakika katiba itakayopita haitadumu. Tena nidiriki kusema hata miaka kumi inaweza isifike maana haitakuwa na baraka.
Tuombe sana katika hili ili ikiwezekana tufikie mwisho mwema.
 
Kwa aliyesikiliza vizuri atakuwa ameelewa ila wasio wasikivu ndo hawa wapiga kelele humu ndani. kama mkuu wa nchi rais asingetoa msimamo wa chama chake kupitia hotuba ile. alichofanya ni kuweka mwelekeo wa majadiliano kwa kuifanya rasimu ya katiba kama ipo kwa ajili ya CCM na kuacha utaifa nyuma kabisa. kwangu mimi napingana kabisa na hotuba ile
 
hotuba ya mkiti Wa ccm.hajui kuwa yeye ni Rais.
 
Hapa raisi katoa mchango wake kwanza kama mwananchi pili kama raisi ndo maana na pia kama mwana ccm ndo maana mwisho wa siku akasema hatima ya haya yote mnayo ninyi sasa kosa liki wapi hapa.wapinzani kama wanalengo la kuvuruga usalama wa nchii hii basi wajipange kivingine vinginevyo dola haitamucha mtu mwenye makusudu ya kuwapa watu hofu na nchi yao.
 
Raisi hakutakiwa kutoa maoni yake wala kuelezea changamoto za muundo wa serikali, kwa nafasi yake kama raisi kauli yake ina impact kubwa kuliko unavyofikiri. Bunge hilo la katiba ndilo ambalo lina jukumu la kuainisha na kujadili hizo changamoto. Amemkosea heshima jaji warioba kwa kujibu kile alichowasilisha. Kumbuka kuwa rasimu inatokana na maoni ya wananchi na sio utashi wa jaji warioba.
Rais kama kiongozi anayo haki kabisa kuyapima mambo, kuyachuja, kuchambua mapendekezo kutoka pande zote na kutoa msimamo wake. Kama hatafanya hivyo kesho mambo yakiharibika ni nyinyi mtakuwa wa kwanza kumlaumu na kusema aliyaruhusu mambo yaende tu na kuyabariki bila kuchambua. Ktk uongozi huo ndio uadilifu wa kiutendaji. Yeye msimamo wake ni huo. Hata kama mambo hayatakwenda kama alivyoshauri bado msimamo wake na chama chake ndio huo. Hata kama Taifa likija kuingia ktk crisis msiseme chama kilichokuwa madarakani kwa wakati huo na mwenyekiti wao walikaa kimya. Thats how politic is.
 
Nimesikiliza hotuba ya JK kwa usikivu wa hali ya juu, hakufungua bunge maalum kwa kuwa hakutamka kuwa Bunge maalum sasa limefunguliwa rasmi. Alimalizia hotuba yake kwa kusema asanteni kwa kunisikiliza. Kwa mtazamo huu JK hakwenda kuzindua bunge maalum bali alikwenda kujibu hotuba ya mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba-Warioba. Hivi ndivyo iliyokuwa, alimjibu Wariaoba kwa mtazamo wa chama chake cha CCM, msimamo wa nchi moja serikali mbili.


Katika kujenga hoja yake ya namna ya kuimarisha muungano wa serikali mbili alisisitiza kuwa wanafanya taratibu za kiutawala ili Zanzibar iwe na uhuru mkubwa wa kujiamulia mambo yake yenyewe huku Tanzania bara ikibaki ndani ya koti la Muungano. Mtazamo huu si wa serikali mbili, nchi moja bali serikali mbili nchi mbili. Kikwete alieleza kuwa kati ya mambo ya kuipa Zanzibar uhuru zaidi ni mahusiano ya kimataifa. Hii maana yake ni kwamba Zanzibar inakuwa nchi wakati huohuo Tanzania bara ndiyo inabaki na jina la Muungano. Inakuwa kama muungano haupo kwa sababu Zanzibar inajitoa kwenye muungano kwa kuwa nchi na wakati huohuo Tanzania bara siyo nchi bali inabeba jina la Muungano.
Huu unakuwa ni muungano fake wa Tanzania bara pekee kwa sababu mambo mengi ya Muungano yanakuwa yameondolewa na kwenda Zanzibar. Hili alilisema Warioba kuwa ukiwa na nchi mbili huwezi kukwepa serikali tatu. Tanzania inakuwa nchi moja ikiwa mambo ya muungano yanaongezeka siyo kupunguzwa kama anavyopendekeza JK na wakati huohuo Zanzibar inakuwa siyo nchi. CCM wakitaka muugano wa nchi moja serikali mbili inatakiwa katiba ya Zanzibar itamke wazi kuwa Zanzibar siyo nchi. Muungano wa upande mmoja anaotaka JK na CCM ni fake na utavunja muungano kwa sababu malalamiko ya Tanzania bara kuamuliwa mambo na Zanzibar ambayo itakuwa na nchi yake na dola yake yataendelea.


Hotuba ya Kikwete ililenga kuifanya Zanzibar iwe huru zaidi lakini wakati huo huo inaiamulia Tanzania bara mambo yake kupitia koti la Muungano ambalo limebebwa na Tanzania bara pekee (kumbuka Zanzibar ni nchi na inajiamlia mambo yake yenyewe). Haya ndiyo malalamiko makubwa ya Tanzania bara na yatakuwa hayajapatiwa ufumbuzi. Mapendekezo ya JK na CCM ni njia ya kukwamisha mchakato wa katiba na hivyo kuonyesha njia ya kuvunja rasmi Muungano.
 
Wajumbe wa bunge la katiba ametuchagulia mwenyewe, umeenda bungeni kuwasemea nini cha kufanya, umeshindwa kuheshimu tume ya Warioba ambayo imekusanya maoni ya wananchi. Bunge la katiba linafanya kazi kwa maslahi ya CCM au kwa maslahi ya watanzania?
 
Mheshimiwa ametumia muda mwingi kuwatisha WaZanzibari wanaoishi Tanganyika akigusia walima vitunguu ,nasikitika kwa nini hakugusia wale wanaoishi Vumawimbi na Makangale kule Pemba wanaolima viasi vitamu.

Kama tungeogopa kufa na kupigana na nduli Amin tusingemtoa na ndio hivyohivyo kwa WaZanzibari ,kwenye maslahi ya Nchi yao ,kwenye maslahi ya ardhi yao hawataogopa kuuliwa na WaTanganyika , hilo liwekeni wazi.

Jengine lilikwishasemwa kuwa WaZanzibari hawatosita kudai maslahi yao hata kama yatawaathiri WaZanzibari wachache waishio nje ya Nchi ,Myahudi (WaISrael) walikwenda Uganda kuwachukuwa watu wao na kufanikiwa na walijua kuwa watauwawa lakini walikwenda na kufanikisha.

WaZanzibari hawatatishwa na hayo aliyoyahofia Mheshimiwa(Inaonyesha mheshimiwa anaogopa kufa) wataendelea kudai maslahi yale wanayoyadai mpaka wajiridhishe vile watakavyo na sikutawaliwa na fikra za Tanganyika ,wao waTanganyika ni hiari yao ,na kama mliangalia mheshimiwa alisema gesi na mafuta ni ya Zanzibar ,na yapo mengine mengi tu ambayo yatajadiliwa kwa interest ya Zanzibar.

Ila Mheshimiwa amezungumza kwa hekima za hali ya juu akijaribu kubalance gumzo lake ,moja ya alichokosea ni pale alipolihusisha Jeshi au vyombo vya ulinzi na kupindua serikali ,lile ni kosa ,ni kama kuwaamsha kwamba mnaweza kufanya jambo hili ,yaani amerudisha maendeleo ya Tz nyuma na kuhemesha fikra za kupindua .
 
Points zote za vitisho zitaainishwa hapa na pia kwa wenye uwelewa ambao wataweza kufafanua zaidi kusudio wanakaribishwa ,Je unajua kama Mheshimiwa Kikwete alitukana ,alisita alishindwa kuomba samahani ,katika ile hotuba ,naitafuta na tusi nitaliweka hapa ???
 
Hapana tusikate tamaa safari bado haijesha fainali ni kura ya maoni tuna muda bado wa kujipanga na kuwazindua wengine waliolala usingizi wa pono
Utashi wetu sisi nguvu zetu na umoja wetu ndio silaha ya kuwawezesha watanzania kuipata katiba waitakayo
 
Kikwete: Siyasemi haya kwa kuwa siyo muumini wa Serikali tatu, lakini hata wanaopenda serikali tatu hawataki serikali maskini, watambue wajumbe wanaotaka serikali tatu wajue wanajenge hoja ya kuisimamia serikali hiyo ya tatu.

Kikwete: Serikali ya tatu haitakuwepo japokuwa sasa mmejiridhisha kuwa ipo lakini kwa uhalisia haitakuwepo kwani haitakuwa na uwezo kujiendesha.

Kikwete: Serikali ya Muungano itakuwa na hatari ya kupinduliwa na nchi kuwa nchini ya Jeshi badala ya rais wa kuchaguliwa.

Kikwete: Haya ni maoni yangu na inawezekana kuwa hayana maana, kitakachoamuliwa na Watanzania ndiyo chetu hicho pamoja.

Kikwete: Mara kwa mara alikuwa anawasiliana na Tume ya Katiba na kumueleza kila kinachoendelea
Kikwete: Ikirudishwa Tanganyika itakuwa ngumu kuwaondoa Wapemba ambao wameishi kwa muda mrefu Tanzania Bara na watakuwa wageni.

Kikwete: Chuki ya Utaifa ikianzishwa lazima watu wabaya wataingia kuharibu usalama wetu, tukianzisha serikali tatu tuwe na majibu ya moja kwa moja ya changamoto.

Kikwete: Kitakachotokea baada ya kuanzishwa kwa Serikali tatu, tutakuja kujutia uamuzi huo

Kikwete: Kuna kiongozi mmoja wa dini aliniuliza, "Serikali 2 zikiwa na matatizo, dawa ni kuongeza ya 3?

Kikwete: Kazi iliyokuwa mbele yenu ni ngumu sana, kazi ya kutunga katiba mpya ni ngumu sana, ipeni nchi yetu hatma njema.

Kikwete: Wajumbe kujadili kila kipengere ni jambo zuri kwani wote watabeba mzigo wa kutunga katiba kwani ikiwa nzuri watakuwa wote ikiwa mbaya watakuwa wote.

Kikwete: Kificho anastahiri pongeni kwa kuendesha bunge la katiba kabla ya kupatikana mwenyekiti wa kudumu, alikuwa na changamoto kubwa kwani hakukuwa na kanuni.

Kikwete: Nawapongeza wajumbe wote kwa hatua mliyofikia japokuwa mmetumia muda mwingi katika hatua ya kwanza, mnatakiwa kuongeza kasi.

Kikwete: Watanzania wamewekeza matarajio yao kwenu, muonyeshe taswira nzuri katika mijadala yenu kwa lugha na vitendo.

Kikwete: Watanzania wamefadhaika na vitendo vyao walivyoonyesha katika hatua ya awali.
Kikwete: Wajumbe muweke mbele maslahi mapana ya nchi yetu, badala ya kujali maslahi yenu binafsi, kauli mbinu yenu iwe Tanzania kwanza.

Kikwete: Siyo jambo mbaya wajumbe kuwa na msimamo ya vyama vyao, kama misimamo hiyo ikiwa ya kujenga Tanzania.

Kikwete: Fuateni kilicho chema hata kama kimetolewa na mtu usiyekubaliana naye.

Kikwete: Mnatakiwa kufanya kazi kwa pamoja na kutoa kitu cha pamoja

Kikwete: Uhodari unaotakiwa ni wa kushawishi na siyo wa kulazimisha

My take:
Contradiction tupu
 
Mkulu jana ni kama alikuwa anahutubia kikao cha NEC ya chama chake. Tofauti ni pale mwishoni, wajumbe walipoimba wimbo wa Tanzania, Tanzania,nakupenda kwa moyo wote( ingawa siyo kweli)!
 
Kwani CCM wameambiwa kuwa serikali3 zitaua muungano? Shida washagundua muungano hauna manufaa ndo mana wanaogopa serikali 3 na zaidi wananiboa wanavyowabeba wazanzibar mpk wanaikana tanganyika, CCM tuelezeni nn kimejificha kwny kung'ang'ania kwenu muungano hewa na kwann hamtaki kuitambua tanganyika wakat mnaitambua zanzibar

siri inajulikana ila wao hawajui kama twaijua
 
Points zote za vitisho zitaainishwa hapa na pia kwa wenye uwelewa ambao wataweza kufafanua zaidi kusudio wanakaribishwa ,Je unajua kama Mheshimiwa Kikwete alitukana ,alisita alishindwa kuomba samahani ,katika ile hotuba ,naitafuta na tusi nitaliweka hapa ???

Nakumbuka alisema Eboooo!
 
Nakumbuka alisema Eboooo!

hILO JINGINE KUNA TUSI KUBWA SANA .nakwambia alisita lakini ndio alikwisha lisema ,kama unakumbukumbu vizuri alisema akilinganisha Zanzibar na Tanganyika ,kwamba kuna mafuta dhahabu ,sehemu ya kulima vitunguu ,na kujilabu sana sana ,akimaanisha Zanzibar ni masikini ,na asie nakitu ni sawa na kijibwa mwitu(Mbwa mwitu):A S-frusty2:
 
Back
Top Bottom