Wapinzani waipinga hotuba ya kikwete

Wapinzani waipinga hotuba ya kikwete

Huyu upeo wake ni mdogo sana kujadili mambo nyeti yahusuyo nchi, kama haya ya katiba.


Kha ha ha ha ha ha haaaaaa! Sasa wewe jana umeona jk amesema nini cha maana kwa Watanzania wapatao 44.9M waliopo Nchini?
Unamkataa Mh. G . Lema ila utamkubali tu!
 
kazi kwelikweli,..


Aisee sijaelewa chochote mkuu!!
 
Hotuba ilikuwa ya Kuikosoa Tume kwa Baadhi ya Vipengele ila kwakuwa Zenji wanataka wawe Huru kwanini Tusiwape Uhuru Wao ambao waliupata toka kwa Waarabu ili kupunguza Msuguano.
 
Wajumbe ndio watakao andika katiba na mwisho ni kwa wananchi wakiikataa mtalaaniwa kwa kula kodi za walalahoi
 
Wapinzani wasipende kunyambulisha maneno. Rais alitoa changamoto za serikali zote tena kwa mifano. Hakusema yeye wala chama chake wanataka serikali ipi. Ndo maana alihitimisha kwa kusema kazi wanayo wajumbe. Basi. Sasa wapinzani wanapoongea hayo ndo tuseme hawakuelewa au walikuwa makini kusikiliza ili wabishane? Busara zinahitajika sana kwenye hili, ila kwa hili wapinzani wananiangusha hata mimi mpinzani. Kwani Rais atakuwepo bungeni? Mpo nyie bhana, mkichemka ni nyie, acheni tabia za ajabu za kupinga kila kitu bila hoja. Huo ni upungufu wa uwezo wa kufikiri kabla ya kunena.

Raisi hakutakiwa kutoa maoni yake wala kuelezea changamoto za muundo wa serikali, kwa nafasi yake kama raisi kauli yake ina impact kubwa kuliko unavyofikiri. Bunge hilo la katiba ndilo ambalo lina jukumu la kuainisha na kujadili hizo changamoto. Amemkosea heshima jaji warioba kwa kujibu kile alichowasilisha. Kumbuka kuwa rasimu inatokana na maoni ya wananchi na sio utashi wa jaji warioba.
 
Wazanzibar 2waachie Nchi yao, Iv k2 gan kinatufanya 2uulilie muungano wakati inaoneka wazi kuwa kuna vi2 haviko Clear.
Au 2takoxa nin km 2kitengana, haina haja ya serikali 2 wala 3.
 
Kazi ya raisi ilikuwa ni kufungua bunge na sio kutoa maoni, muda wa kukusanya maoni uliishapita, kama hakutoa maoni yake basi asitumie nafasi yake vibaya. Kwa maoni yangu angeweka mkazo kwenye uzalendo kwa wajumbe na kuweka maslahi ya taifa mbele dhidi ya maslahi ya makundi na vyama. Kauli yake kuwa uamuzi uko mikononi mwa wajumbe haimaanishi kuwa hakutoa shinikizo. Unaelewaje pale ambapo mzazi anapotoa specification za mkwe anayemtaka halafu nahitimisha kuwa uamuzi upo kwa mwanaye kuchagua mtu anayemtaka?
 
Mimi binafsi nilijiandaa kupokea hotuba kama ile,hata hivyo ni heri kumpongeza JK kuliko kumlaumu maana JK sio baba wa Taifa na sio mlezi wa vyama.JK ni RAIS wa JMT na M/KITI wa CCM.haiwezekani akaongea bila kuonyesha msimamo wa chama chake maana wenzie watamuona ni msaliti na watamchana live na kumsuta kwenye vikao vya chama chao kwa kutosimamamia msimamo waliojipangia.mimi bado naamini hotuba ya Warioba inamfunika JK,na Tanganyika yetu irudi maana hatujazaliwa ili kuifurahisha/kuilazimisha znz.
 
Hv mbona watz ni watu waajabu?? Zaidi ya asilimia 50 hamkuwahi kuishi kuona Tanganyika. Leo hii mnaitaka Tanganyika . Nyinyi watu vip?

Na kati kujadili katiba,suala la zanzibar na tanganyika sio sehemu kuu tu ya kupata katiba mpya. Kuna mambo mengi ya msingi zaidi ya hayo ya wachumia matumbo kama wakina jusa sijui.
 
Ni sawa na mwanao anaumwa terminal illness unanzisha safari ya kutoka mkoani kumleta Dar muhimbili atibiwe alafu unamtembeza Posta na kariakoo wiki nzima kisha unamwambia turudi home nimeongea na daktari kwa simu ushauri wake na vipimo mie naona haufai turudi mkoani tukatafute madokta huko tutayamaliza huko huko. Sawa wewe ni baba ila mtoto atakua na Imani na wewe tena?
 
Tujiulize ni tume ngapi zimeundwa toka Uhuru kuhusu Muungano, zimekuja na majibu gani na kwanini? Kufungua BUNGE c kuhutubia wabunge wa ccm na kuwaelekeza cha kufanya!!! Mbele ya safari watakumbuka maoni ya hizi tume!!!!
 
Kwa stahil hii atutengenez katiba bal tunaboresha katiba ya mwaka 1977
 
attachment.php
 
Hv mbona watz ni watu waajabu?? Zaidi ya asilimia 50 hamkuwahi kuishi kuona Tanganyika. Leo hii mnaitaka Tanganyika . Nyinyi watu vip?

Na kati kujadili katiba,suala la zanzibar na tanganyika sio sehemu kuu tu ya kupata katiba mpya. Kuna mambo mengi ya msingi zaidi ya hayo ya wachumia matumbo kama wakina jusa sijui.


Kwangu mimi, hutoba ya Rais Kikwete jana, ni kati ya hotuba bora kabisa alizowahi kutoa akiwa Rais juu ya Tanzania ikifuatiwa na ile ya Afrika Kusini . Rais alikuwa mtulivu na kafanya uchambuzi mwanana juu ya faida na hasara za mfumo wa serikali tatu. Kama kiongozi wetu mkuu, alikuwa na dhamana ya kutuasa, ili tutakapoamua kujikaanga kwa mafuta yetu wenyewe, yeye awe amejitoa lawamani. Tofauti na Jaji Warioba, ambaye amefanya kazi kubwa sana, Kikwete ana dhamana ya kuhakikisha Taifa halitumbikii shimoni, maana yeye ni dereva wetu sote.

Rais hakuwaamualia wajumbe mfumo wa serikali, aliowanesha hatari itakayotokana na uchaguzi mbovu, kisha akawaachia jukumu, aidha wafanye uamuzi utakaoiua Tanzania na kujitia, au wakafanya uamuzi wa busara utakaowaweka kwenye vitabu vya historia kama mashujaa. Tukiacha ushabiki na maneno ya kufundishwa kama alivyodokeza Rais, hotuba ilijaa dira na uzalendo kwa nchi hii. Tanzania kwanza, katiba mpya inawezekana!
 
Ni mawazo yako uko sahihi kabisa lakini ni vema tukaangalia zaidi uhalisia kuliko kubaki kwenye hekaya za nadharia tutakuwa hatuendelei...!!
 
Back
Top Bottom