Wapinzani waipinga hotuba ya kikwete

Wapinzani waipinga hotuba ya kikwete

Jamani kwani shida nini apo Rais kaongea lakini maamuzi kawaachia wajumbe mie cjaona kosa hapo.kilichobaki ni wajumbe wakachambue pumba wapike mchele watanzania tupate ubwabwa.
 
Kwangu mimi, hutoba ya Rais Kikwete jana, ni kati ya hotuba bora kabisa alizowahi kutoa akiwa Rais juu ya Tanzania ikifuatiwa na ile ya Afrika Kusini . Rais alikuwa mtulivu na kafanya uchambuzi mwanana juu ya faida na hasara za mfumo wa serikali tatu. Kama kiongozi wetu mkuu, alikuwa na dhamana ya kutuasa, ili tutakapoamua kujikaanga kwa mafuta yetu wenyewe, yeye awe amejitoa lawamani. Tofauti na Jaji Warioba, ambaye amefanya kazi kubwa sana, Kikwete ana dhamana ya kuhakikisha Taifa halitumbikii shimoni, maana yeye ni dereva wetu sote.

Rais hakuwaamualia wajumbe mfumo wa serikali, aliowanesha hatari itakayotokana na uchaguzi mbovu, kisha akawaachia jukumu, aidha wafanye uamuzi utakaoiua Tanzania na kujitia, au wakafanya uamuzi wa busara utakaowaweka kwenye vitabu vya historia kama mashujaa. Tukiacha ushabiki na maneno ya kufundishwa kama alivyodokeza Rais, hotuba ilijaa dira na uzalendo kwa nchi hii. Tanzania kwanza, katiba mpya inawezekana!

Safi kaka. Lets goo. Tanzania kwanza
 
Suala lililopo ni la Maridhiano tu,Kufumua Rasimu inawezekana kwani Vitu vyote viletwavyo Bungeni si ni Mali ya Bunge !! Kwa hiyo Wabunge Wafanye Watakavyoonainafaa !!
 
huwezi kuwa na muungano wa nchi mbili Halafu u
kawa na serikali mbili.
 
Back
Top Bottom