Wapinzani wa kweli wa nchi hii ni Mbowe na Lissu

Wapinzani wa kweli hawajazaliwa nchini!

Hujui kama Mbowe alikuwa anahongwa pesa na Mzee Mkono ili asiweke mgombea ubunge wa chadema katika jimbo alilokuwa anagombea Mzee Mkono.

Unajipa matumaini ambayo hayapo!
Una ushahidi au umerithishwa tu kelele walizopiga wenzako?
 
Mbaya zaidi, Mbowe alipewa na Rostam hela kukisaidia chama yeye akadai amekikopesha chama. Tuhuma hii ilitolewa na naibu katibu mkuu wa chadema wakati huo, na mtuhumiwa hakuwahi kuikanusha.
Kama hakuwahi kukanusha sasa si ndio ingekuwa vizuri muende mahakamani, mbona bado mnashangaa tu?!

Pathetic.
 
Mimi simshangai maalim seif kuikubal serekali hii, kwa sababu hali zote mbili keshaziishi.
Na sisi wananchi ndio tunaoumia kwa hili maalim kalipatia kiukweli...
Nikikuajiri utaharibu kazi ili serikali yangu ionekane haifanyi kazi. Piga chini, utaajiriwa na uliemchagua na ndiye unayemwamini. Utaoaje mwanamke usiyekupenda?
 
Lissu ni mpinzani kindakindaki.

Mbowe mtoto wa damu wa taifa, amekunywa maji ya bendera. Yuko kati.
 
Lisu huyuhuyu aliekimbilia kwa Amsterdam?

Mbowe kashindwa kuwaongoza watu wasiozidi 50 tena wanawake kina Mdee ndio mpinzani wa kweli?

Mwaka 2015 Mbowe na Lisu wadhalibadiri gia angani na kumkodishia Lowasa chama, hawa ndio wapinzani?

Hakuna kama Slaa! Yule mzee ni mtu na nusu. Siyo hawa wazee wa faraga.
Nakazia
 
Jiulizeni na nyie mmefanya nini ili kuwa wapinzani wa kweli?au ndio kushabikia na kupiga kelele za mitandaoni tu?
 
Habari ndo hiyo, hiyo miamba hapo juu ndo tafsiri haswa ya mpinzani wa nchi hii ni nani.

Ambaye hataki na anabisha kwa nnachokisema, aende akameze boga, akifanikiwa kulimeza basi mimi ni muongo na nipigwe mawe.

Upinzani wa kweli ni kutokuyumbishwa msimamo wako juu ya unachokiamini. Mbowe na Lissu wamepitia mengi sana ambayo yangetosha kuukana upinzani wao, lakini wameendelea kutoyumbishwa kiitikadi.

Angalia kituko cha leo cha ACT Wazalendo, sijawahi kuona jambo la hovyo kama walichokifanya leo. Yaani vile vitimbi vyote mpaka wasamaria wema wazanzibar wameuawa kikatili, halafu leo hii eti wanakubali kushirikiana tena na hao hao watesi wao? Hivi hii ni akili ya namna gani? Bado sijaona hekima iliyotumika hapa. Ni sawa tu nakusema na wao wamewatumia wazanzibari kama chambo ya wao kupiga 'Michongo'.

Bado naendelea kuwa na wasiwasi na upinzani wa Zitto Kabwe kwenye siasa, namkubali kama mtu anayejielewa kwenye issue nyingine za ki intellectual na kujenga hoja, ila kwenye upande wa itikadi halisi ya upinzani, napata shida sana kwamba akae kundi gani.
Mgoja Mbowe ateuliwe mbunge Rais atoke mbio kuenda kuapishwa
 
Back
Top Bottom