Wapinzani ombeni msamaha kwa Watanzania, mtasamehewa

shamimuodd

JF-Expert Member
Jan 28, 2019
890
1,398
Nianze kwa kuwapongeza Watanzania kwa uzalendo wao wa kuchagua maendeleo bila kujali itikadi za vyama vyao, hakika ushindi wa CCM ni uthibitisho wa mageuzi ya ki-fikra ya Mwafrika yenye kuachana na mawazo tegemezi ya kila aletacho mzungu ni bora kuliko tulicho nacho.

Binafsi nilikuwa nina uhakika kama ilivyo kwa wazalendo wengi kuwa CCM ilikuwa lazima ishinde kwa sababu ambazo hata wapinzani walizifahamu.

Badala ya kuitisha maandamano, fanyeni press conference muwaombe msamaha watanzania kwa upotoshaji wenu, pia na ushiriki wenu wa kuisaliti nchi kwa misingi ya kutaka kuuza rasilimali za nchi yetu.

Hakika hamjachelewa, mkiomba msamaha, watanzania watawasamehe
 
...
Badala ya kuitisha maandamano, fanyeni press conference muwaombe msahama watanzania kwa upotoshaji wenu, pia na ushiriki wenu wa kuisaliti nchi kwa misingi ya kutaka kuuza rasilimali za nchi yetu.
Hivi huwa mnafikiria kabla ya kuandika kweli? Wapinzani wakataka kuuza rasilimali za nchi? How? When? Ndio waliopandisha Twiga kwenye Ndege au? Ndio waliogawa gesi kule Mtwara au? Ndio walioiingiza nchi kwenye mikataba ya ovyo au?

Anyway, furahini na kushangilia kwa sasa kwa sababu mna mbeleko ya vyombo vya dola; kwa sababu mmeshikilia mifumo yote ya nchi; kwa sababu mna madaraka ya kusema hili liwe au lisiwe na ikawa hivyo sio kwa hoja au kwa misingi ya kisheria ila kwa kutumia nguvu! Ila iko siku!
 
Ushindi wa KISHINDO
 

Attachments

  • Screenshot_20201101-101529.jpg
    Screenshot_20201101-101529.jpg
    38.2 KB · Views: 1
"Jerusalema ikhaya lami,
Ngiiiiiiiiiilondoloze,
Uuuuuuuhambe nami,
Zuuuuungangishiyi lana" x 3
 
Write your reply...wananchi wanatambua kuwa hawanahaja ya kuombwa msamaha na wapinzani kwa kuwa wanajua kuwa waliwapa kura wapinzani, kura zao zikatwaliwa na CCM kwa kutumia kura za bandia.
 
Hadi sasa nashangaa Lissu alipatapataje kura milioni moja, alistahili kupata Kura elfu 60 tu!
Mimi nilikuwa nafanya takwimu huku mitaani niliishia jamaa atapata 1.5M ila sijui hizi zingine laki nne na ushee kazitoa wapi!



MAGUFULI4LIFE.
 
Back
Top Bottom