Wapinzani na serikali tatu, kuna nini?

Wapinzani na serikali tatu, kuna nini?

Hakuna kitu kama hicho, nadhani katika hili tuache unafiki tumuunge mkono Mtikila anaedai Tanganyika ya 1961-1964, haya mambo mengine kusema kuumarisha muungano hayawezi kumaliza kero. Dawa ya hizi kero ni kuvunja muungano kila nchi ikachukua chake, zaidi ya hapo tunadanganyana.
 
Kiukweli mwenyewe siipendi serikali tatu wala mbili, kwa mawazo yangu ninafikiri serikali moja ndio dawa. kero nyingi zinasababishwa na wazanzibari wenyewe. wanafikiri wanauzalendo sana na mkoa wa zanzibar kuliko watu wa nchi ya Tanganyika. kwa kweli hoja yao ni dhaifu. wametumia fursa ya ustaarabu wa watu Tanganyika kutunyanyasa. Hebu fikiria, watu hawa wana Bunge lao la wawakilishi, wana rais wao, wana katika yao inayovunja katiba ya Jamhuri ya Muungano na Kuwafanya wao kuw a juu ya sheria kuliko watanzania wengine, wana Bunge lao la Jamhuri linaloingia katika bunge linaloitwa la jamhuri na kuiba rasili za watanganyika bila hata aibu, na leo wanadai eti wananyanyaswa, hivi inaingia kweli akilini watu milioni moja na laki nne kunyanyaswa na watu milioni arobaini na nne? watanganyika ndio tunanyanyasika hakika, na kwa kuwahurumia hawa majamaa, tunaitaji tutengeneze nchi moja inyoheshimu sheria ya nchi. pia uhuru wa wabara kuishi zanzibari kama wao wanavyo ishi bara bila vitisho na unyanyasaji.Na wakikataa wakaleta ubishi bunge maalum la katiba nawaomba mtengeneze serikali tatu kama hawa ndugu zetu wa damu hawajatukumbuka. wanawategemea waarabu ili wawarudishie wazanzibari utumwa kwa maslahi ya wachache na wengi hasa wakinamama zetu kuishi maisha ya tabu kabisha itakayowanyima nchi hii ya asali na maziwa. kama ni uzalendo hata mimi ninao juu ya nchi yangu ila ni huruma tu.
 
Upinzani wanatetea maoni ya wananchi kama ilivyo bungeni wanavyo tetea maslahi ya wananchi,HUKU CCM WANA MINYA NA KUKWAPUA MAONI YA WANANCHI KAMA ILIVYO WANAVYO FISADI MADINI NA MALI ZA WANANCHI,JIULIZE NI LINI CCM WAKAWATETEA WANANCHI?HATA RIPOTI YA BUNGE KUHUSU OPERESHENI TOKOMEZA UJANGILI WAMEKUA WAKIIKATAA NA KUWATUHUMU AKINA LEMBELI
 
Hivi kikwete alichaguliwa na asilimia ngapi ya watanzania ndugu yangu na bado kaapishwa kama rais? .ndugu hiyo inaitwa sample katika research na ni representative. Huwezi akahoji watz wore.
 
Wewe utakuwa na AKILI ZA MAITI Maoni ya Serikali 3 sio ya vyama vya Upinzani ni maoni ya Watanzania na vyama vya upinzani vinasimamia nini Watanzania wanataka kwani mapendekezo haya yapo Katika Rasimu hii ya 2 iliyowasilishwa na Warioba.
sijawahi kukubaliana na hoja za misukule ya kibavicha hata siku moja. ila hii kwa mara ya kwanza naungana na msukule kwa 100%. keep it up japokuwa inaniuma sana.
 
Tatizo ni CCM ama ni Muundo wa Muungano?? Tusianze kulaumu kwamba chama kinahujumu wakati cc wenyewe ndio tunaotaka kushinikiza mfumo mbovu wa serikali uwepo.
Tusijazwe mawazo mepesi tu tukaamua kukubaliana nayo moja kwa moja lwamba ni lweli na sahihi.
 
Ndugu wana jamvi salaam.
Nimesema hivyo nikiwa na uhakika kabisa na mifano natoa.
Kumekuwepo Mawaziri wa serikali ya Zanzibar (serikali ya kwanza)
Pia kumekuwepo Mawaziri wa serikali ya Muungano (mambo ya muungano). (serikali ya pili ambayo ni ya JMT).
vilevile kuna Mawaziri wa mambo yasiyo ya muungano (je hawa ni mawaziri wa serikali ipi kama si serikala ya 3 yaan ya Tanganyika?)
Jaji Warioba hajaongea kitu kipya bali amewataka CCM wajitambue na kuacha kufichficha mambo.
 
mbona matusi mkuu, ni wazo lake hivyo hakuna sababu ya kumtukana cha msingi kanusha hoja yake
 
Ndugu wana jamvi salaam.
Nimesema hivyo nikiwa na uhakika kabisa na mifano natoa.
Kumekuwepo Mawaziri wa serikali ya Zanzibar (serikali ya kwanza)
Pia kumekuwepo Mawaziri wa serikali ya Muungano (mambo ya muungano). (serikali ya pili ambayo ni ya JMT).
vilevile kuna Mawaziri wa mambo yasiyo ya muungano (je hawa ni mawaziri wa serikali ipi kama si serikala ya 3 yaan ya Tanganyika?)
Jaji Warioba hajaongea kitu kipya bali amewataka CCM wajitambue na kuacha kufichficha mambo.

Big Like mdau!
 
Ndugu wana jamvi salaam.
Nimesema hivyo nikiwa na uhakika kabisa na mifano natoa.
Kumekuwepo Mawaziri wa serikali ya Zanzibar (serikali ya kwanza)
Pia kumekuwepo Mawaziri wa serikali ya Muungano (mambo ya muungano). (serikali ya pili ambayo ni ya JMT).
vilevile kuna Mawaziri wa mambo yasiyo ya muungano (je hawa ni mawaziri wa serikali ipi kama si serikala ya 3 yaan ya Tanganyika?)
Jaji Warioba hajaongea kitu kipya bali amewataka CCM wajitambue na kuacha kufichficha mambo.
Tz huwa ni wepesi wa kupokea Tekinologia zingine tena kwa kasi lakini hapa kwenye muungano mbona hatutaki kuachana na muungano Analogia?tuje na muungano Digtal kama wa USA na kule Uk
 
wandug wa jf hivi wanavyo sema serikali tatu ni maana vyama tatu au nin,naombeni msaada wenu
 
Wanamaanisha Vyama vitatu ndo vitakuwa vinatawala, kwani mkuu ulikuwa hujui hiyo ya serikali tatu imekaaje?
 
Eti mnataka serikali tatu...? Kwa vyanzo gani hasa vya mapato mpaka zanzibar iwezeze kuchangia serikali ya muungano? Hapa kinachoonekana ni kuridhisha wanasiasa wenye uchu wa madaraka tu kwani gharama ya maisha zitapanda kama wanavyolia wenzetu wa kenya maana serikali ya muungano haina vyanzo vya mapato sasa ili kufidia hayo kitakachofuata kodi nyingi zitakazo umiza wananchi. Enyi viongozi wenye uchu wa madaraka acheni kupotosha umma. Sisi wananchi tunataka maisha bora tu si uwingi wa serikali
 
KAMATI za Bunge Maalumu la Katiba zimeanza kuwasilisha bungeni maoni yake, kuhusu mijadala ya sura ya kwanza na ya sita ya rasimu ya Katiba mpya, huku wengi wakikataa muundo wa serikali tatu, kwa kusema utaibua hisia za ubaguzi kwa wananchi wa taifa moja.

Miongoni mwa kamati zilizowasilisha maoni jana bungeni ni Kamati Namba Tano, ambayo Makamu Mwenyekiti wake, Assumpter Mshama, alisema muundo wa serikali tatu ukipita, utaibua hisia hizo, ambazo hazipati nafasi katika mfumo uliopo wa serikali mbili.

Assumpter alimnukuu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyesema; "Nje ya Muungano, hakuna Wazanzibari, kuna wao Wapemba na sisi Waunguja…dhambi hii haitaacha kuitafuna Tanganyika ambayo ina makabila mengi."

Mbali na ubaguzi, walio wengi katika kamati hiyo walielezea hatari nyingine ya muundo unaopendekezwa, utajenga mazingira ya kulisambaratisha Taifa.

"Sura ya 17 ya rasimu inathibitisha kitakachotokea endapo muundo unaopendekezwa utakubaliwa. Mojawapo ya mambo yanayozungumziwa na sura hii ni masuala ya kugawana rasilimali, kugawana watumishi wa umma, madeni na mambo mengine.

"Mambo haya badala ya kuwaleta karibu, inawatenganisha wananchi wa pande mbili za Muungano…kwa mnasaba huu, muundo wa serikali mbili ndio ulioafikiwa na wajumbe wengi kuwa unalifaa taifa letu kwa kuzingatia maslahi ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiusalama ya wananchi wa pande mbili," alisema.

Kuhusu kero za Muungano zinazodaiwa kudumu kwa miaka 50 na kuwa kichocheo cha kupendekezwa kwa serikali tatu, walio wengi katika Kamati hiyo walisema changamoto hizo wanazitambua na jitihada zinafanyika kuzikabili.

"Walio wengi wanaamini kuwa muundo wa serikali tatu hautakuwa suluhisho badala yake utaibua changamoto nyingine nyingi. Mchakato huu ni fursa kubwa na ya pekee kuzishughulikia changamoto hizi kwa mapana yake. "Mapendekezo yaliyotolewa na walio wengi, yanalenga kuzipa jitihada hizi kinga za kikatiba na kisheria ili ufumbuzi wake uwe endelevu," alisema Assumpter.

Kutokana na hoja hizo, Assumpter alisema walio wengi wanapendekeza katika Sura ya Sita, Ibara ya 60 (1), irekebishwe na kusomeka "Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa na muundo wa serikali mbili ambazo ni: "Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania; na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Wajumbe wengi pia katika Kamati hiyo, wamependekeza kuwepo kwa viongozi wakuu wenye mamlaka ya utendaji katika Jamuhuri ya Muungano waliotajwa katika Ibara ndogo ya (3), ambao watawajibika kila mmoja wao katika kutekeleza madaraka waliyopewa kuhakikisha wanalinda, wanaimarisha na kudumisha Muungano.

Viongozi wakuu hao ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano, Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano, Rais wa Zanzibar na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tanganyika kufufuliwa?

Kamati hiyo Namba Tano, walio wengi wamependekeza kabla ya Rasimu ya Katiba kupitisha muundo wa serikali tatu, ni lazima nchi inayoitwa Tanganyika iwepo kwanza na kupewa mamlaka yake, kisha iamue inataka Muungano wa aina gani.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mshama alisema rasimu ya Katiba inapendekeza muundo wa serikali tatu zitakazotokana na Muungano wa nchi mbili, lakini hivi sasa Tanganyika inayopendekezwa kama nchi mshirika haipo.

Alifafanua Tanganyika haipo kwa kuwa mamlaka, uendeshaji na masuala yake yote yalikwishakabidhiwa kikatiba na kisheria katika nchi inayoitwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania tangu mwaka 1964.

"Hivyo kama kuna shirikisho linapendekezwa basi ni lazima kwanza nchi hiyo inayoitwa Tanganyika iwepo, iwe na Katiba yake na vyombo vyote vya utawala ili iweze kuwa na mamlaka ya kuamua kama inataka Muungano. "Muungano wenyewe wa aina gani na kama ni shirikisho, basi Tanganyika iamue kwa msingi wa kuyakubali masharti ya shirikisho linalopendekezwa. Hilo likifanyika Hati ya Makubaliano iliyopo na ambayo ndiyo inayotajwa na Rasimu ya Katiba, itabaki kuwa waraka wa kihistoria," alisema Assumpter.

Kamati Namba 2

Mwenyekiti wa Kamati Namba Mbili, Dk Shamsi Vuai Nahodha, alisema katika ibara ya kwanza inayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wajumbe walikuwa na mjadala mkali kuhusu maana ya maneno Muungano na Shirikisho, ambayo ufafanuzi wake ulitolewa.

Alisema Muungano ni makubaliano ya zaidi ya nchi moja, kuunda dola moja yenye nguvu, ambapo majukumu ya msingi ya nchi hizo yanakabidhiwa kwenye Serikali ya Muungano.

Alisisitiza Muungano wa Tanzania ni makubaliano kati ya Tanganyika na Zanzibar, ambapo Tanganyika ilikabidhi madaraka yake yote kwa serikali ya Muungano na Zanzibar ilikasimu baadhi ya madaraka yake kwa serikali ya Muungano.

Kwa upande wa Shirikisho, Dk Nahodha alisema Shirikisho ni makubaliano ya nchi mbili au zaidi, zinazounda Serikali moja chini ya kiongozi mmoja, lakini kwa muktadha wa rasimu ya Katiba iliyopo, Shirikisho linalozungumziwa litakuwa na serikali tatu na Marais watatu.

Alisema baada ya ufafanuzi wa kina, wajumbe walifanya uamuzi katika Ibara ya Kwanza wajumbe wengi ambao hawakufikia theluthi mbili walipendekeza neno Shirikisho lifutwe kwa sababu tatu; Kwanza, hati ya makubaliano ya Muungano inazungumzia kuwepo kwa serikali mbili yaani serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

"Hata Rasimu ya Katiba katika Ibara 1 (3) inatambua hati ya Muungano kama msingi na mwendelezo wa makubaliano hayo," alisema Nahodha.

Alisema sababu ya pili ni Hati hiyo ya Muungano mpaka sasa haijafutwa na wala haijabadilishwa na tatu, Shirikisho la Serikali tatu linalopendekezwa katika rasimu, litakuwa dhaifu kiasi cha kushindwa kudhibiti ulinzi wa eneo la Bahari ya Hindi lenye rasilimali nyingi ambazo mataifa makubwa wanaziwania.

"Udhaifu huu utayapa mwanya mataifa hayo kuzirubuni nchi washirika zisichangie gharama za kuendesha serikali ya shirikisho hasa tukizingatia kuwa serikali ya Shirikisho haina vyanzo vya uhakika vya mapato na endapo jambo hili litatokea Shirikisho litadhoofika na hatimaye kuvunjika."

Msingi wa Muungano

Akizungumzia Sura ya Sita, inayozungumzia muundo wa Jamhuri ya Muungano alisema wajumbe walijadili na kuchambua na kukubaliana kwamba Muundo wa Serikali Mbili, kama ulivyoanishwa katika hati ya Muungano, ndio msingi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema hata hivyo baada ya kupiga kura kwa ajili ya kupata uamuzi, theluthi mbili ya upande wa Tanzania Bara haikupatikana. Alisema ingawa theluthi mbili haikupatikana, wajumbe wengi kutoka pande zote, walipendekeza kwamba Ibara hiyo ifanyiwe marekebisho.

Alisema kutokana na marekebisho hayo; Ibara ya 60 (1), itasomeka; "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa na muundo wa serikali mbili ambazo ni (a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano na (b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Ibara ya 60 (2) sasa itasomeka kwamba "Shughuli za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitatekelezwa na kusimamiwa na (a) vyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji, (b) vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutunga sheria na (c) vyombo viwili vyenye mamlaka ya utoaji haki. Hoja kinzani Akisoma maoni kinzani, Dk Nahodha alisema katika mjadala huo baadhi ya wajumbe walikuwa na mtazamo hasi hususani neno Shirikisho lilipotumika.

Kwa mujibu wa Nahodha, baadhi walisema wajumbe walio wengi walidhamiria kwa kiwango kikubwa kuleta marekebisho ama nakala ya rasimu yao ya siri ili kubadili kiini cha rasimu rasmi, ambayo kimsingi ni maoni na mapendekezo ya wananchi kama yalivyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, iliyoundwa na Rais.

Source: HabariLeo
 
hivi mfafanuliwe hadi lini ndio muelewe gharama za muungano?!
 
Yatakuja makontena ya msaada ya tende toka uarabuni na sisi tutapata fursa ya kwenda huko kufanya kazi za ndani na pato la serikali yetu litaongezeka. Halafu tutajiunga na OIC tutapata misaada. So no problem tutakuwa vizuri zaidi kiuchumi kuliko mnavyotubana sasa.
 
Back
Top Bottom