wiseboy.
JF-Expert Member
- Aug 11, 2014
- 2,932
- 4,534
Nataka mtuambie nyie watu,hao wapinzani wanaohamia huko CCM hadi sasa hivi wamejenga viwanda vingapi?
Kauli mbiu ya awamu ya tano ni kuwa na Tanzania ya viwanda, sasa badala ya ujenzi wa viwanda kuna mlipuko wa wapinzani kuhamia CCM kwa kile kinachoitwa kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Rais wetu Magufuli.
Kila wanapohama(kununuliwa) ni lazima uchaguzi mpya ufanyike,naambiwa kuwa gharama ya uchaguzi wa Diwani pekee ni sh mil 300,kwa taifa letu Tanzania lilivyo bado lina mahitaji ya msingi kwa watu wake kama Ajira,afya,Elimu na miundo mbinu (infrastructures) inakuwaje huu mlipuko wa Kubumba wa wapinzani unaachwa utokee?
Uchaguzi wa madiwani 10 tu unagharimu sh Bil 3, hizo pesa zinatosha kujenga kiwanda cha kusindika juice na chenji inabaki,kiwanda ambacho kina uwezo wa kuajiri watu 200 na kuwapunguzia ukali wa maisha.
Kama wapinzani kuhamia CCM ndo viwanda vyenyewe basi kazaneni yetu macho,lakini mkumbuke kuwa muda huwa hausubiri.
Sent using Jamii Forums mobile app