Serikali: Ni wakati sasa ya kuviweka hadharani Viwanda 4,000 tulivyojenga Wapinzani waone haya

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,272
23,046
Najua wapinzani walipiga sana kelele kuwa serikali haijafanya kitu. Na Waziri akajikuta anatoa siri ya kujenga viwanda 4000 na ajira zaidi ya milion 3.

Sasa nadhani tunapoenda kwenye uchaguzi Serikali iviweke wazi viwanda hivyo watu wajionee.hawa wapinzani wana ujinga wa kupinga kila kitu wanakataa hatujajenga viwanda 4000.

Serikali ilijua hilo ndo maana ikavificha kwanza mpaka ufike wakati muafaka ili kumwaibisha shetani. Siku hiyo tutaamka asubuhi na Voilaaa.... Tunakuta kiwanda hapa ,tunaenda kule tunakuta kiwanda na tukigeuka huku kiwanda.

Hapo mipinzani itapata kigugumizi. Na ajira ambazo tumeziweka kiporo nazo siku moja tu tunaamka watu wanakuta text za kuitwa kuanza kazi mara moja siku hiyo hiyo asubuhi.wapinzan watatafuta pa kujificha.na hawatapata kabisa.

Wengine wanapiga kelele kuhusu zile 50,000,000 kila kijiji. Hawajui serikali ilishagawa kimya kimya na sasa wakati huu tunategemea wanakijiji mbalimbali waje watoe ushuhuda jinsi ambavyo wamefaidika nazo.tunaona maendeleo mbalmbali na shukrani za wanavijiji ambao wameweza mpaka kufuga majogoo makubwa.

Majogoo hayo unaweza kutumia hata kuolea.badala ya ng'ombe. Tunaona jinsi wakulima wa mahindi wanavuna mpaka hindi moja unaweza liuza kwa tsh 5,000. Ni kutokana na zile pesa na juhudi za serikali ya 5.

Wapinzani mwaka huu hamna chenu zaidi ya kupita kutusimulia tu kuwa lissu alipigwa risasi 30+ na amesurvive.so what? Watu walipigwa hadi mabomu na waka survive. Jamaa tu walikosa shabaha.

Je hizo ajira watoto wenu hawatapata? Je siku serikali ikiamua sasa kuviweka viwanda hadharani ninyi hamtanunua bidhaa zake?

Mwaka 2020 twendeleeni tena na CCM imalizie pale ilipoishia... Na wapinzani mwaka huu mta pagawa zaidi hapo.mtapagawa kwa nani mimi sijui.ila hata kusoma namba hamtaweza mtaona vumbi tu.
 
117195765_3213508722074131_2911542144163865371_n.jpg
 
nafikiri walikuwa wanahesabu vitambulisho vya wamachinga.

serikali ya ccm imejaa hadaa ya kiwango cha mvua ya masika.
 
Vikifika viwanda hata asilimia sita (6) tu ya idadi hiyo mm nakunywa sumu. Labda kama mtajulisha na blender za watu za kusagia juisi
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom