Wapinzani kuhamia CCM hadi sasa hivi viwanda vingapi wamejenga?

wiseboy.

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
2,932
4,534
Nataka mtuambie nyie watu,hao wapinzani wanaohamia huko CCM hadi sasa hivi wamejenga viwanda vingapi?
Kauli mbiu ya awamu ya tano ni kuwa na Tanzania ya viwanda, sasa badala ya ujenzi wa viwanda kuna mlipuko wa wapinzani kuhamia CCM kwa kile kinachoitwa kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Rais wetu Magufuli.
Kila wanapohama(kununuliwa) ni lazima uchaguzi mpya ufanyike,naambiwa kuwa gharama ya uchaguzi wa Diwani pekee ni sh mil 300,kwa taifa letu Tanzania lilivyo bado lina mahitaji ya msingi kwa watu wake kama Ajira,afya,Elimu na miundo mbinu (infrastructures) inakuwaje huu mlipuko wa Kubumba wa wapinzani unaachwa utokee?
Uchaguzi wa madiwani 10 tu unagharimu sh Bil 3, hizo pesa zinatosha kujenga kiwanda cha kusindika juice na chenji inabaki,kiwanda ambacho kina uwezo wa kuajiri watu 200 na kuwapunguzia ukali wa maisha.
Kama wapinzani kuhamia CCM ndo viwanda vyenyewe basi kazaneni yetu macho,lakini mkumbuke kuwa muda huwa hausubiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani mpinzani akihamia ccm ndo wanamhamisha, si ana hama mwenyewe. Na uchaguzi unafanyika kwa mujibu wa sheria halali, so kwa akili yako ndogo ulifikiri jimbo likibaki wazi uchaguzi pia usifanyike.. Leo sina mode ya kutukana ngoja nikuache tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nataka mtuambie nyie watu,hao wapinzani wanaohamia huko CCM hadi sasa hivi wamejenga viwanda vingapi?
Kauli mbiu ya awamu ya tano ni kuwa na Tanzania ya viwanda, sasa badala ya ujenzi wa viwanda kuna mlipuko wa wapinzani kuhamia CCM kwa kile kinachoitwa kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Rais wetu Magufuli.
Kila wanapohama(kununuliwa) ni lazima uchaguzi mpya ufanyike,naambiwa kuwa gharama ya uchaguzi wa Diwani pekee ni sh mil 300,kwa taifa letu Tanzania lilivyo bado lina mahitaji ya msingi kwa watu wake kama Ajira,afya,Elimu na miundo mbinu (infrastructures) inakuwaje huu mlipuko wa Kubumba wa wapinzani unaachwa utokee?
Uchaguzi wa madiwani 10 tu unagharimu sh Bil 3, hizo pesa zinatosha kujenga kiwanda cha kusindika juice na chenji inabaki,kiwanda ambacho kina uwezo wa kuajiri watu 200 na kuwapunguzia ukali wa maisha.
Kama wapinzani kuhamia CCM ndo viwanda vyenyewe basi kazaneni yetu macho,lakini mkumbuke kuwa muda huwa hausubiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hats kununua wapinzani wanne nao ni sawa na uchumi wa viwanda! Tanzania inaongoza duniani kuwa na chaguzi nyingi kila mwezi.
 
Wamefanikiwa kujenga kiwanda cha kisasa kabisa ambachohakijawahi kutokea duniani cha kununua wapinzani.
 
Back
Top Bottom