Wapinzani 2000 Kibaha warejea CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wapinzani 2000 Kibaha warejea CCM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwanajamii, Feb 7, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Makamu wa Rais DR Mohamed Ghalib Bilal amepokea wanachama 2000 kutoka vyama mbali mbali vya upinzani mkoani pwani.

  wanachama hao 2000 walikabidhiwa kadi za CCM katika maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa chama hicho ambapo katika hotuba yake Dr Bilal aliwapongeza kwa kujitambua kwao na kuamua kurudi nyumbani.


  Bilal alitabiri CCM kuongoza Nchi hadi mwaka 3000.


  My take;Hili ni pigo kubwa sana kwa upinzani.
   
 2. Mromboo

  Mromboo JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 728
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  Tokapa we!!!! Toka lini kukawa na wapinzani Kibaha? Labda wamatoka CUF.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  kWA KIBAHA HATA WANGEKUWA 100,000, hawana ishu!
  Watu wa Pwani hawaaminiki hata sekunde moja!
  Hamuoni mikoa inayoleta mageuzi ni ipi jamani?
   
 4. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,659
  Trophy Points: 280
  Angalia usije ukapoteza hata ile hadhi ndogo uliyobaki nayo!
   
 5. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kitengo cha propaganda ni muhimu katika kuimarisha chama - Baba Riz 1
   
 6. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  he he he propaganda za kudanganya watu kuwa hali ya chama ni nzuri.....mbona wanachama wakiondoka hawatangazi?
   
 7. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #7
  Feb 7, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Ukirudi nyuma ina maana hujajitambua; kujitambua ni kusonga mbele.
   
 8. l

  luckman JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  mkutano wa bilali hata watu 300 sijui ka wamefika, sasa sijui hao 2000 wanatokea wapi!nape at work or tambwe hiza!
   
 9. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #9
  Feb 7, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Kuna uweli mkuu - Kibaha / pwani ni ngoma za mdundiko kwa kwenda mbele - hawajajua wenye kuwaza tunataka kufanya nini, na ndo maana hata JK huwa akitaka kuongea na wazee hawezi kwenda Arusha au Kanda ya Ziwa, anabaki hapo mwambao kwa wazee wanaomind Kahawa Vs Kashata na longolongo kibao.
   
 10. B

  Baba Collins JF-Expert Member

  #10
  Feb 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni huko huko Kibaha,na hao hawakua hata na kadi za uanachama kama unavyokuza wewe.
   
 11. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  hiyo ndo agenda waliyo baki nayo ccm kuonyesha umma kwamba bado wanapendwa. hawana sela. unategemea sasa hivi kuna mpinzani wa kwenda ccm? wenye akili timamu tushajua mchezo ulochezwa hapo. ova
   
 12. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #12
  Feb 7, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  iringa imechukuliwa na upinzani ikiwa na wanachama wenye kadi robo ya walioichagua,mwanza hivyohivyo,mbeya na shinyanga.
  hao unaowaita wanachama walikuwa wa ccm wote,maana yake nini?ccm inaanza kutafuta wanachama baada ya kukimbiwa.
  siasa za tanzania si zile za chama kimoja ambapo kadi ya ccm ilikuwa kitambulisho cha kuzuia usikamatwe mzururaji.

  sasa hivi watu wanajali kitambulisho cha kura,na vilevile watu wanabadilika ndani ya siku mbili kwa hiyo kama bado mpo kwenye falsafa ya kadi inakula kwenu.
  kwa taarifa yako huu mgomo wa madaktari ndani ya wiki moja ccm imeshapoteza watu kama milioni ambao hawataki hata kuisikia.


  endeleeni kuchapisha kadi za upinzani na kuzigawa kwa wanazi wenu na kujirudishia ili kujidanganya kuwa mmevaa nguo kumbe mko uchi.
   
 13. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #13
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mkuu,umenisababishia BAN lakini nimeappeal na nimerejea tena!
   
Loading...