Wapigania uhuru wa Zanzibar waungwe mkono!

Mods nakunasihini musiunganishe huu uzi wala kuiondosha tafadhalini.

Vuguvugu la mabadiliko ikichangiwa na fujo zinazoendelea zanzibar linaonesha ni jinsi gani watu wamechoka na utawala uliokuwepo huko na katika muungano uliokuepo pia. Me kwa uweliowangu wapewe nchi yao wajiytawalie wenyewe na sisi huku bara tuidai tanganyika yetu cuz sisi midomo mengi na bla bla zisizoisha bt kuitetea tanganyika yetu hatuwezi ni sawa na nyoka wa kibisa ni mkubwa lakini hang'ati tumebaki humu ndani ya jf kulumbana na kutukanana dini zetu tuu in battle ground sisi ni zero simaanisho jeshi letu hapana sisi wananchi hatuwezi kitu tumebaki bla bla tuu
Niko teari kukosolewa kama nimekosea
 
Jambo la ajabu sana ikiitishwa kura ya maoni Zanzibar 70% au zaidi ya wakazi watasema hawataki muungano ,ikiitishwa Bara 60% au zaidi watasema hawataki muungano. Sasa inakuwaje hapa :hatari: ???

Hivi hii kitu mbona wanasisasa wana dilly-dally?
 
zanzibar na tanganyika ni majina tu. hata kama wanayoyataka wakipewa hayatawasaidia lolote kwa kuwa na majina hayo, kama uchu wao wa madaraka hautapatiwa suluhisho. Hata km muungano unakufa sasa zanzibar haitakuwa na amani km ubinafsi na ubaguzi unaodekezwa hivi sasa unabaki ulivyo. na watakaoumia si wengine ni wazanzibari na wapemba wenyewe..
 
Jambo la ajabu sana ikiitishwa kura ya maoni Zanzibar 70% au zaidi ya wakazi watasema hawataki muungano ,ikiitishwa Bara 60% au zaidi watasema hawataki muungano. Sasa inakuwaje hapa :hatari: ???

Hivi hii kitu mbona wanasisasa wana dilly-dally?

True dat bro
 
Jambo la ajabu sana ikiitishwa kura ya maoni Zanzibar 70% au zaidi ya wakazi watasema hawataki muungano ,ikiitishwa Bara 60% au zaidi watasema hawataki muungano. Sasa inakuwaje hapa :hatari: ???

Hivi hii kitu mbona wanasisasa wana dilly-dally?

we have perfected the art of living a lie.
 
zanzibar na tanganyika ni majina tu. hata kama wanayoyataka wakipewa hayatawasaidia lolote kwa kuwa na majina hayo, kama uchu wao wa madaraka hautapatiwa suluhisho. Hata km muungano unakufa sasa zanzibar haitakuwa na amani km ubinafsi na ubaguzi unaodekezwa hivi sasa unabaki ulivyo. na watakaoumia si wengine ni wazanzibari na wapemba wenyewe..

Naona umeangalia upande mmoja wa shilingi.

Kwa kukusaidia zaidi upande wa Tanganyika ndio itakuwa mbaya zaidi kwani chuki za Kidini mlizoachiwa na wakoloni na kupaliliwa kwa kasi sana wananchi wenyewe ndizo zitawaumbua. Mtaacha sasa kuuwa vikongwe na wenye vipara ikiwemo kukata viungo vya albino na mtaingia kuumizana wakristo na waislam.

Kwani kwa sasa pengo hilo linzibwa na waZnz ambao kwa % ni waislam.

Poleni sana

 
Mimi nafikiri waZanzibari wapo wazi saaaana na kila wakti wanasema msimamo wao hivi ni wakti muafaka kuungalia kwa kina sana muungano wenyewe kabla ya kuangalia kero za muungano kwa vile Muungano umechangi kwa kiwango kikubwa kuathiri sekta ya uchumi visiwani.

Na wapo tayari kwa lolote litakalo amuliwa na mjadala huo.

Labda na wewe utudadavulie maana yake hakuna sehemu yoote WATANGANYIKA walipoweka Msimamo wao kuhusu Muungano. Tupe msimamo wenu?


Naunga mkono hoja mia kwa mia kero za muungano merely symptoms of an underlying disease- mfumo mbaya wa muungano. Tibu ugonjwa siyo dalili.
 
Mimi napendekeza kusiwepo mlolongo wa sijui kupiga kura za maoni kwa Wazanzibar? Cha muhimu waugomee na wasiende Dodoma hawa wabunge wao na waombe wajitoe kwenye muungano na wabaki na Zanzibar yao na sisi Tanganyika yetu. Hakuna cha kukatisha mguu eti unakuja bara bila passport na tuna uwezo wa kukuzuia. Wale walioko bara wafungashe virago warudi kwao au waombe uraia ambao tuna uhuru wa kuwapa au kuwanyima, tunaomba Watanganyika wetu warudi kwao nchi ni kubwa na tuko tayari kuwacompansate kwa hasara watakayokuwa wamepata kutokana na mali tutakayochukua kwa wapemba waliowekeza tanganyika. Cha Muhimu kelele zimekuwa nyingi na tumetukanwa vya kutoshwa eti mara wakoloni, mara makafiri wa bara, mara matusi ya nguoni. Tuna heshima yetu na watuache na heshima yetu waende zao. Hatuna haja ya kuwa wakoloni na si nia yetu kutawala nchi nyingine. Sisi Watanganyika ni nchi uru tangu 9/12/1961 muungano hautuongezee kitu zaidi ya gharama nyingi

Mkuu wangu mawazo ya serikali moja DULITY ni kupuuza Muungano wa nchi mbili.. Zanzibar ni nchi ina soveign yake na muhimu sana ktk majadiliano kama haya tuheshimu kuwepo kwa Zanzibar na kuenzi Muungano uliopo..Hivyo kuifananisha Zanzibar na Mikoa ya Mwanza, Arusha na kadhalika ni wazo linalopotosha zaidi..

Kuna njia mbili tu zinazoweza kukubalika 1. Kuunda serikali tatu,(Ya UMoja wa Taifa, na zile za Tanganyika na Visiwani) ama 2. Kuuvunja Muungano kutokana na kura za maoni za Wazanzibar ambao wataambiwa ukweli na wawakilishi wa makundi mawili majukwaani. Ikiwa ni pamoja na kundi la wale wanaoutaka Muungano wakiwaeleza wananchi kwa nini muungano ni muhimu kwao, halafu wale wanaopinga Muungano na kwa nini hautakiwi.. Kisha wananchi wakisha elimishwa hilo Wazanzibar wote watapiga kura za maoni yao na yataheshimika. Kura za Hapana zikiwa nyingi tutaendelea na mfumo uliopo wa serikali mbili na pengine kurekebisha tu kero zilizopo..
 
Ndio maana kila wakti nasema hamna msimamo nyie ni bendera kufuata upepo.

Sasa kwa kuwa hamna msimamo kaeni kimya muwaache wenye msimamo wanaposema kweli? na kama mnaona inawakera basi chukueni hatua.

Poleni sana

Bar baru kuweka msiamamo na ZNZ ni kuwa hutataki Jusa na Waarab watup[angie nini tunataka.
Sisi hatujabanwa na tunapumua, hatujawa koloni! Yule anayedhani anaonewa ndiye anapaswa aamue nini cha kufanya.
Watu milioni 40 hatuwezi kuendeshwa na kundi la Sultani. Upuuzi huo utatokea Zanzibar.

Kwa taarifa yako ZNZ hakuna msimamo, umesikia juzi ! Kinachotokea ni kuwa kundi la Sultan la akina Jusa, Ahmed na Maalim ndilo limebeba vipazi sauti.

Nyuma kuna sauti za Mapinduzi ambazo zimekaa kimya zikiangalia hali ya Mambo.
Ndiyo maana akisema Nasor Moyo anaambiwa hajasoma, Seif Khatibu ni Kibaraka, Mapuri mwenndawazimu, Nahodha amehongwa n.k. the bottom line ni kuwa Wanamapinduzi wapo na wanaliangalia kundi la Sultan kwa ukaribu sana.
 
Mods nakunasihini musiunganishe huu uzi wala kuiondosha tafadhalini.

Vuguvugu la mabadiliko ikichangiwa na fujo zinazoendelea zanzibar linaonesha ni jinsi gani watu wamechoka na utawala uliokuwepo huko na katika muungano uliokuepo pia. Me kwa uweliowangu wapewe nchi yao wajiytawalie wenyewe na sisi huku bara tuidai tanganyika yetu cuz sisi midomo mengi na bla bla zisizoisha bt kuitetea tanganyika yetu hatuwezi ni sawa na nyoka wa kibisa ni mkubwa lakini hang'ati tumebaki humu ndani ya jf kulumbana na kutukanana dini zetu tuu in battle ground sisi ni zero simaanisho jeshi letu hapana sisi wananchi hatuwezi kitu tumebaki bla bla tuu
Niko teari kukosolewa kama nimekosea

Ndugu yangu amini mungu hakuna kilicho chomwa na mimi baba yangu mzazi na kaka zangu wa nne tunalaza magari yetu kanisani na sio sisi tuu watu wengi sana wa mji mkongwe wanaeka magari yao hapa hakuna kilichochomeqa hata kimoja

Hivi wewe ni MTANGANYIKA unayeishi Unguja na baba yako na zako wanne ambao mnalaza magari yenu kanisani? Halafu wakati huo huo uko bara ukidai Tanganyika yako.

Kweli wewe mkali! Au unatuona wote majuha. Au ni Troll!

Amandla........
 
Nguruvi3,


Nguruvi3.

Kama utakaa kusikiliza na kusimamimia nani kasemaje. Je unajuwa yaliyotokea jana na leo?

Kumbuka kuwa kila siku yanatokea mengi sana na yatatokea mengi sana LAKIN SHARIA ZINABAKI VILE VILE. Mimi nimekupa Msimamo wa Znz na waZnz. Hebo soma hapo.

Mjadala wa Muungano sasa wageuka kama kaa la moto
Salim Said na Salma Said, Zanzibar

WAKATI Watanzania leo wanaungana nchini kote kuadhimisha miaka 45 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, kero mbalimbali zinazoukabili sasa ni wazi zinatishia kuusambaratisha.
Hali hii inatokana na watu wengi katika pande mbili za Muungano kushindwa kukubaliana na muundo wake pamoja na kuwapo kero nyingi ambazo hazijapatiwa ufumbuzi.

Baadhi ya watu nchini wamedai kuwa kero za Muungano zimekuwa zikiusukasuka kwa muda mrefu sasa kutokana na serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupata kigugumizi cha kufanya mjadala wa kitaifa kutafuta suluhu ya kero hizo.

Wakizungumza katika kipindi cha Kipimajoto kinachorushwa na ITV juzi usiku, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Zanzibar, Juma Duni Haji, alisema bila ya kuwa na serikali tatu kero za Muungano zitaendelea kudumu.

"Serikali ya Zanzibar ni ya watu na kila penye watu pana ardhi na pia ukisikia kuwa kuna harusi unategemea kumkuta mwanamke na mwanamume ukiwakuta wanaume watupu utashtuka," alisema Duni.

"Shughuli za serikali ni tatu (jurisdiction) kuna Muungano, Zanzibar na Tanzania Bara, hivyo kila shughuli hapa inahitaji serikali na hapo tutamaliza kero za Muungano kama walivyo wenzetu wa Uingereza."

Alisema, Mkataba wa Muungano ni wa kimataifa na kama hivyo ndivyo, hauwezi kuingiliwa na upande mmoja tu na kufanyiwa mabadiliko bila ya makubaliano ya walioungana.

Naye Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi Samuel Ruhuza alisema, serikali zinajaribu kupotosha historia kwa kuwa wanaitangaza tarehe tisa ya Uhuru wa Tanganyika kuwa ni ya Uhuru wa Tanzania na wanafunzi wanafundishwa hivyo shuleni, jambo ambalo si kweli.

Aidha, alifafanua kuwa wanaiacha Desemba 12 ya Uhuru wa Zanzibar na kusherehekea siku ya Mapinduzi ya Zanzibar na watu hawajui siku ya Uhuru wa Zanzibar.

"Tunapotosha na kufuta historia yetu, hali hii ni mbaya sana," alisema Ruhuza na kuongeza:

"Zanzibar ina rais ambaye hana dola na hawezi kupinduliwa kwa sababu huwezi kumkamata mtu na kumshtaki kuwa ni haini anataka kupindua Zanzibar, ni kichekesho".

Ruhuza alikiri kuwepo kwa kero za Muungano na kuthibitisha kuwa serikali tatu ndio suluhu ya kudumu ya kero hizo.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Victor Kimesera alisisitiza kuwa makubaliano ya msingi ya Muungano yamekorogwa na kuingiliwa bila ya makubaliano ya pande mbili husika.

Alisema hiyo ndio sababu moja ya kutofikiwa kwa malengo ya Muungano kwa kuwa upande mmoja uliingia na kuongeza mambo ya Muungano bila ya makubaliano.

"Mambo ya msingi ya Muungano yalikuwa 11 tu, lakini sasa yameongezwa na kufikia 24 haya ndiyo yanayoleta mijadala na migogoro isiyokwisha," alisema Kimesera.

Kwa upande wake, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Azaveli Lwaitama alisema, Muungano ulisababishwa na sababu za kiusalama na amani.

"Mzee Abeid Karume alikubali kuungana kwa sababu alikuwa anahitaji amani na usalama kutokana na hofu aliyokuwa nayo ya kuvamiwa na mataifa ya Magharibi; na huku Mwalimu Nyerere alikuwa na hofu ya kuathirika iwapo Zanzibar ingevamiwa. Si unajua machafuko yakiwa Zanzibar na Bara pia yana gharama zake," alisema Lwaitama na kuongeza:

"Tatizo la Muungano sio jina, jina si chochote. Tatizo linakuzwa kwa utashi wa wanasiasa tu, na ardhi ya Zanzibar kwa sababu ni ndogo ndio maana kukawa na vikwazo kwa watu wa Bara kumiliki, lakini kwetu sisi ardhi ni kubwa hata wakija Wazanzibari wote hawawezi kuimaliza."

"Mwalimu alikubali hayo ili Wazanzibari wasijione kama vile wamemezwa na ndio maana hata serikali, bendera na wimbo wa taifa wanavyo. Ukimwona mtu wa bara anapigia kelele hilo huyo ni mangi wa Tanganyika."

Lwaitama alipingana na kauli ya wanasiasa kuwa serikali tatu ndio suluhu ya kudumu ya matatizo ya Muungano, na kupendekeza kuwa serikali moja ndio suluhu na kwamba nchi haiwezi kutoka katika serikali mbili ikaenda kwenye serikali tatu ni kichekesho.

"Hata Mwalimu alisema, tukitoka serikali mbili ni kwenda serikali moja na sio tatu. Tukitoka mbili na kwenda tatu badala ya moja ni kioja na kichekesho kikubwa," alisema Lwaitama.

Naye Kiongozi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Kiongozi Zanzibar, Enzi Talib Aboud alisema wakati umefika serikali ya Tanganyika ikarejeshwa.

Aboud alisema hayo jana wakati akijadili mada yake iliyowasilishwa katika kongamano la kitaifa kwa niaba yake na Mwanasheria, Ali Omar ambalo liliwashirikisha wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Zanzibar, viongozi mashuhuri, wasomi na viongozi wa vyama vya siasa.

Aboud alisema serikali ya Tanganyika irejeshwe ili iweze kusimamia mambo ambayo hayamo katika orodha ya Muungano kwa upande wa Tanzania Bara ili mfumo unaotumika Zanzibar utumike na Bara.

Alisema tangu kuundwa kwa Muungano SMZ, imekuwa na katiba na serikali yake ambayo inasimamia mambo ya ndani ya Zanzibar ambayo hayamo katika orodha ya mambo ya Muungano.

Alisema kwamba, uchumi wa Zanzibar umekuwa ukififia kutokana na vikwazo mbalimbali vilivyomo katika mfumo wa Muungano na kushauri Zanzibar ipate haki zake zote za misaada, utambulisho wake wa kidola na uwakilishi wake katika jumuiya za kimataifa ili iweze kukuza uchumi na kuinua kipato cha wananchi wake.

Aboud ambaye ni mwadhishi wa habari mkongwe aliyewahi kufanya kazi katika vyombo vya habari kadhaa ya Tanzania Bara na kukamata nafasi za juu za serikali ya Zanzibar, alisema kwamba wakati umefika mkataba wa awali wa Muungano ukapelekwa katika Baraza la Wawakilishi ili wajumbe wapate nafasi ya kuridhia mkataba huo.

Alisema mkataba huo wa Muungano baada ya kufikiwa mwaka 1964 uliridhiwa na upande mmoja wa Muungano, lakini baraza la kutunga sheria wakati huo Zanzibar (Baraza la Mapinduzi) halikupewa nafasi ya kuridhia mkataba uliosainiwa na Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Sheikh Abeid Amani Karume.

Kongamano hilo limefuatia kuzuiwa kwa maandamano ya kuunga mkono suala la mafuta na gesi asilia kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano kama ilivyopendekezwa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Juzi Mkuu wa Polisi wilaya ya Mjini, Mkadam Khamis Mkadam, alisema suala la mafuta na gesi asilia ni suala la kikatiba na linapaswa kujadiliwa na mabaraza ya kutunga sheria na sio jumuiya au taasisi nyingine, hivyo jeshi la polisi haliwezi kuruhusu kufanyika kwa maandamano hayo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha UPDP, Haji Othman Haji, alisema kwamba Muungano ulifikiwa kwa maamuzi ya Nyerere na Karume, lakini wananchi hawakupewa muda wa kutosha wa kufikiria na kuamua katika suala hilo.

Naye Profesa Abdul Sharif ambaye ni mtafiti wa mambo ya historia alisema wananchi katika taifa wamegawanyika kutokana na mitazamo tofauti kuhusu Muungano wakiwapo wanaofikiria uvunjwe na uundwe upya ili kwa kuzingatia masilahi ya kiuchumi badala ya kisiasa pekee.

Kwa upande wake Ali Mohammed Said alisema wananchi wajadili uhalali wa Muungano wenyewe badala ya kujadili kero zake kwa kuwa ufumbuzi wa matatizo hayo ni kurudi kuangalia mfumo wake.

Awali, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Ustadh Farid Hadi aliwataka wananchi wa Zanzibar kuondoa woga na kujadili kwa uwazi matatizo yanayoukabili Muungano kwa masilahi ya wananchi wake na vizazi vijavyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz
 
Hawa hawaondoki hawa; waondoke nani atazuia hilo wimbi la visasi!

Je umeshawahi kusoma vitabu hivi.
1.. Development and Religion in Tanzania,(1981) kilichoandikwa na Jan P van Bergen.
2. Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985. kilichoandikwa na Padre Dr John C. Sivalon,

Sasa ule utabiri laazima utatimia.

Je waTanganyika mtanusaka hapo kwenye UDINI.

Historia siku zote inajirudia. Zimeni moto wa waislam kudai haki zao sasa.
 
Barubaru,

..hayo matatizo ya UDINI ni yetu wa-Tanganyika, wewe Mzanzibari/Muomani yanakuhusu nini?

..vunjeni tu muungano. hatuna haja na mkataba wowote ule na Wazanzibari kwasababu hatuwahitaji.

..kama kushirikiana tutafanya hivyo kupitia EAC, SADC,AU, na UN.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom