Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
UMEFIKA wakati watu wa bara (Tanganyika) waanze kuwaunga mkono wapigania uhuru wa Zanzibar wakiongozwa na Seif Sharrif Hamad na Ismail Jussa. Viongozi hawa wawili kutoka chama cha CUF wamejitambulisha kuwa wanataka Zanzibar iwe Dola Kamili kwanza na baadaye kuwepo Muungano wa Mkataba.
Kwa muda mrefu viongozi hawa na wengine walio nyuma yao wanaamini kuwa Zanzibar imebanwa na Tanganyika na wapo ambao kati yao wanaona Tanganyika imegeuza Zanzibar kuwa koloni lake.
Makala yangu hii basi ni ya kuwaunga mkono wapigania uhuru hawa ili hatimaye kabla ya mwisho wa mwaka huu Zanzibar iwe taifa huru lenye mamlaka kamili ya mambo yake ya ndani na nje na ikipeperusha bendera yake kwenye Umoja wa Mataifa na ikiwa ni nchi kamili.
Kwa vile sasa hivi Zanzibar imemezwa na Tanganyika na kwamba wananchi wanaamini nchi yao inatawaliwa kimabavu na utawala wa Rais Jakaya Kikwete wakati wao wanahitaji kuwa huru kutoka katika ukoloni huu ili hatimaye na wao waweze kupumua kama vile mtu anayevua koti lililokuwa likimbana.
Sababu zao zina nguvu
Kundi hili la Wazanzibari ambalo wanataka uhuru wao linaamini kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Tanzania siyo halali na kuwa una kasoro nyingi ambazo haziwezekani tena kutatuliwa isipokuwa kwa kuvunja Muungano huu. Wanaamini kuwa mfumo wa sasa unaneemesha zaidi Tanganyika na kuwa Zanzibar inakuwa na kutendewa kama sehemu ya Mkoa wa Tanganyika.
Lakini sababu kubwa ambayo ina nguvu sana ni kuwa Zanzibar tayari ilishawahi kuwa dola kamili na hivyo kudai dola kamili ni kudai kurudishwa kwa kilichopotezwa. Haijalishi kwa kweli kinachotakiwa kurudishwa ni Zanzibar ipi; kama ni ile kabla ya uhuru wa 1963 au ile ya kati ya uhuru na mapinduzi ya Zanzibar (chini ya Waziri Mkuu Shamte) au ni ile ya mara tu baada ya mapinduzi na kabla ya Muungano (chini ya mzee Karume). Vyovyote vile ilivyo wapigania uhuru wanachotaka ni kile kinachoimbwa sana siku hizi kuwa Zanzibar Kwanza halafu mengine baadaye.
Njia ya haraka ya Zanzibar kupata uhuru wake
Nimeshaandika huko nyuma lakini leo nimeona nirudie kwa sababu kwa namna fulani wapigania uhuru hawa wa Zanzibar wanatumia njia ndefu sana ya kulalamika majukwaani badala ya kutumia njia rahisi zaidi. Kuna msemo kuwa umbali mfupi zaidi kati ya sehemu A na B ni kwa kuchora mstari ulionyoka. Hii ni kweli kwa sehemu ambayo ni tambarare kwani mahali ambapo kuna mabonde, milima na makorongo sehemu mbili zinaweza kuwa karibu sana lakini haziwezi kufikiwa kwa mstari ulionyoka isipokuwa kwa kuzunguka.
Binafsi naamini suala la Zanzibar kuwa huru siyo suala la kuzunguka kivile kwani linaweza kumalizwa kwa mstari ulionyoka endapo tu wapigania uhuru hawa watakuwa tayari kufuata ushauri wangu ambao tayari nimeutoa mara kwa mara mwaka huu hasa baada ya kutambua kuwa hatuna viongozi wa Muungano (ukiondoa wachache sana) ambao wameweza kuutetea Muungano. Hakuna cha viongozi vijana wala wazee ambao wameweza kuwa watetezi wa Muungano huu. Na kwa vile Muungano huu sasa hauteteeki ni muhimu kufanya kila jitihada ili uvunjwe mapema na kila mtu achukue zake.
Njia rahisi ya Zanzibar kupata uhuru inaotamani ni kwa viongozi wa Zanzibar kwanza kabisa kukataa kutambua Muungano uliopo sasa. Hili ni jambo la muhimu sana kwani mara moja litatangaza mgogoro kati ya pande hizi mbili. Haiwezekani upande mmoja waone kuwa Zanzibar inakaliwa kimabavu na Tanganyika na kudai uhuru lakini wakati huo huo wanaishi kama wanautambua Muungano wa sasa.
Fikiria jinsi ambavyo viongozi hawa hawajajaribu kutaka wabunge wa CUF wanaotoka Zanzibar wajiondoe kwenye bunge la Muungano ili kupinga ukoloni. Maana mkoloni anayekubali kuwa na wabunge na kuwapa heshima zote kama wabunge wengine ni mkoloni gani? Lakini tukikubali kuwa Tanganyika ni mkoloni wao basi jambo la kwanza ni kukataa kutambua taasisi za Kimuungano. Hivyo, tunawatia shime kuwa kikao kijacho cha Bunge la Muungano CUF na kina Maalim Seif na wenzao wawakataze wabunge wao kuja kwenye Bunge la Muungano.
Kama watakuja wabunge kutoka Zanzibar kwenye kikao kijacho na kama miongoni mwao wamo wa CUF tutatambua kuwa wapigania uhuru hawa hawataki Zanzibar iwe huru bali wanasema maneno ya kufurahisha hadhara.
Pamoja na hilo wapigania uhuru wa Zanzibar wanahitaji kuwahamasisha Wazanzibar wao kuachilia nafasi wanazoshikilia kwenye taasisi za Muungano. Kama Muungano wa sasa siyo sahihi na kuwa ulilazimishwa na kuwa siyo wa mkataba ni wazi kuwa hakuna njia nyingine isipokuwa kuwahamasisha Wazanzibar wanaotumika kwenye Muungano huo kuachia nafasi zao.
Binafsi nitapenda kuwasikia kina Jussa na Seif na wenzao wenye kuwaunga mkono wakitoa tamko la kuwatia shime watumishi wa Zanzibar kwenye Serikali ya Muungano wajiondoe. Hii itakuwa ni kuanzia na Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal na watumishi wengine wote kuanzia jeshini, hadi kwenye taasisi nyingine nyingi ambazo si za Muungano.
Ili tujue kweli wanataka wawe na nchi yao cha kwanza ni kukataa kula cha mkoloni! Warudi kwao Zanzibar kama ambavyo wapigania uhuru wengine walivyowahi kufanya. Huwezi kumpinga mkoloni huku anakulisha, kukulinda na kukupa maisha yako!
Hatutaki muungano mwingine
Sasa mojawapo ya vitu ambavyo vimenishangaza sana wakati umefika kuviita ni vya kipuuzi ni kuwa wanaotaka kutoka kwenye Muungano huu wa sasa hawachelewi kusema ati wanataka Muungano wa Mkataba. Hivi nani kawaambia kuwa wakijitoa kwenye Muungano huu sisi Watanganyika tunataka Muungano wowote tena? Yaani wao waamue kutoka halafu wao hao hao waamue wanataka Muungano wa aina gani? Kwa kitu gani walichonacho?
Naomba niwekwe kwenye rekodi kuwa Muungano huu ukitushinda hatutaki Muungano mwingine wowote; uwe wa mahaba au wa mkataba! Kama huu wa sasa tumeshindwa kuutetea nani anafikiri ujao wa mkataba utalindwa? Kama huu wa sasa umeshafikia kuitana wakoloni hivi huo ujao utakuwaje? Na kama wa sasa umejaa kero nyingi hivi ni kwa nini tuamini kuwa huo ujao utakuwa salama?
Wanatuambia ati utakuwa ni wa mkataba kwa maana ya Muungano kama ule wa Jumuiya ya Ulaya! Hivi wameona yanayoendelea huko? Leo hii katika Muungano wa Ulaya nchi ndogo ndogo ambazo zimekuwa tegemezi kwa nchi kubwa zimejikuta kwenye matatizo mengi sana kiasi kwamba imebidi zichukue hatua kali za kujifunga mikanda. Ugiriki, Ureno na Uhispania nikitaja nchi chache zimejikuta kwenye hali ngumu sana ya kiuchumi. Cha kushangazani kuwa nchi ambayo imejikuta ikitumia utajiri wake na nafasi yake kubwa ya kiuchumi yaani Ujerumani ndio imebebeshwa mzigo wa kusaidia nchi hizi nyingine.
Haya ndiyo malipo ya muungano wao. Ujerumani imejikuta kuwa kama kaka mlezi wa kuwasaidia hawa. Kama ambavyo unaweza kuwa umesikia au kusoma Chansela Angela Merkel amejikuta analindwa na askari zaidi ya 6000 katika ziara yake ya kutembelea Ugiriki nchi ambayo iko kwenye hali ngumu zaidi ya kiuchumi. Badala ya Wagiriki kumshukuru Merkel kwa kutumia utajiri wan chi yake kuokoa nchi yao Wagiriki hawa (ambao baadhi walishambulia ofisi za Jumuiya ya Watanzania huko) wamekuwa wa kwanza kumuona Merkel kama mtu anayewakandamiza. Sasa Tanganyika ikiingia mkataba kama huu na Zanzibar si ndio tutajikuta tunabebeshwa mzigo mkubwa kuliko tunavyotaka?
Wazanzibari wakitoka kwenye Muungano huu wa sasa Watanganyika hatutaki Muungano mwingine maalumu nao. Tutakutana nao kwenye taasisi nyingine za kimataifa kama ni SADC, EAC, UN au kwingine. Lakini sijui mkataba mwingine maalumu ni kujitakia matatizo na hivyo Watanganyika wanapoenda kutoa maoni yao kwenye Tume ya Katiba wawe wazi kabisa kuwa wanachotaka ni Muungano kamili wa nchi moja na serikali moja nje ya hapo ni Utengano. Utengano ambao kwa kweli siyo uadui bali ni kutambua kuwa hatuwezi kuwa na Muungano wowote kwani huu wa sasa umetosha kuumiza watu vichwa.
Tanganyika haihitaji Zanzibar na haiitegemei Zanzibar kwa chochote. Ni kwa sababu hiyo naamini ili kuharakisha Zanzibar kujitoa na viongozi hawa wapigania uhuru kuweza kupata nafasi ya kuongoza taifa la Zanzibar natoa pendekezo kuwa kwa ukarimu wetu kutoka Tanganyika tutenge shilingi bilioni 400 hizi ili kuwasaidia Zanzibar kuanza maisha mapya wao wenyewe. Tuchukue madeni yao ya nje na kuwa tayari kuwalipia mshahara wa vyombo vile vilivyokuwa vya Muungano ili Zanzibar wasije wakasema kuwa wameonewa. Nina uhakika bilioni 400 ni fedha nyingi sana ambazo Wazanzibari watashukuru.
Hivyo, nawasihi wale wote ambao wanataka kina Jussa na Seif waharakishe kuondoa Zanzibar kwenye Muungano tuwaandikie na kuwaambia Let Zanzibar Go yaani Tuiache Zanzibar Iende! Iende na kuwa taifa huru na lenye mamlaka kamili. Na itakuwa vizuri kama kina Jussa na Seif wanaamini kuwa wana mashabiki wengi basi wajue uamuzi wao wa kujitoa kwenye Muungnao utaungwa mkono Zanzibar kwani hadi hivi sasa inaonekana kuungwa mkono huku kupo.
Ni serikali ya Dk. Mohammed Shein ambayo inaonekana kubariki jambo hili na wakati umefika kuwaunga mkono na wao. Tuwaunge mkono kwani wakiamua kujitoa tu tayari mfumo wao wa serikali uko kamili na ambao hauitaji mambo mengi mapya.
Binafsi nitawapuuzia wapigania uhuru hawa kama wataendelea kungangania watu watoe maoni na kuwa wanataka Zanzibar huru lakini hawachukui hatua zozote za kutaka uhuru huo utimie. Ikumbukwe kuwa serikali ya Muungano haitatumia nguvu kuwalazimisha Zanzibar.
Kila la heri Wazanzibari, tukutane UN.