Barubaru
JF-Expert Member
- Apr 6, 2009
- 7,161
- 2,323
Maswali yako hayatajibiwa kwasababu WZN hawana majibu. Jibu moja rahisi tunataka muungano wa mkataba.
Kwani Muungano mlionao sasa wa Tanganyika na Zanzibar ni wa aina gani?
Maswali yako hayatajibiwa kwasababu WZN hawana majibu. Jibu moja rahisi tunataka muungano wa mkataba.
Mwanakijiji.
kama kupe huyo pamoja na kubebwa kote huko lakin anakuwa mlalamishi KWANINI USIMTOSE?
Lakin kuna suala dogo nitaka kukuuliza.
Je kama kunatokea maasi upande wa Tanganyika kwa kuwafukuza waZnz, je Znz itakuwa na ubavu wa kutoa majeshi kwenda kuzuia maasi hayo.
Jusa amekiri hili katika kongamano la Jumamosi.Ametamaka kwa kinywa mbele ya kadamnasi kuwa kijiografia, kindugu, kiuchumi na kiusalama ZNZ inaiihitaji Tanganyika.! Big confession of the yearof course isingeweza; lakini Zanzibar ilipokuwa huru na majeshi yake na kila kitu chake iliomba Tanganyika msaada wa kutuliza mapinduzi! Zanzibar hata ikiwa na kila kitu chake na vifaru vyake si tishio kwa namna yoyote kwa Tanganyika. Ila Tanganyika itaendelea kuweka kivuli Zanzibar (iwe ndani ya Muungano au nje).
Kwani mwalimu alikuwa Mungu?
kama yeye alikufa na muungano unaweza kufa vile vile.
Muungano wa kikatiba.Kwani Muungano mlionao sasa wa Tanganyika na Zanzibar ni wa aina gani?
Mimi ni muumini wa Pan Africanism kwa sababu najua pasip hivyo WAAFRIKA tutaendelea kuwa watumwa wa mfumo wa kibeberu..Wakuu wangu, Mzee Mwanakijiji, Mkandara, Nguruvi3, Fundi Mchundo, wapo wapi wapigania uhuru wa Tanganyika yetu pamoja na maslahi ya Tanganyika.
Kwanini ZNZ itake mkataba na jinamizi?
Muungano wa kikatiba.
Another confession from Baru baru kuwa huu ni mkataba. For so long amekuwa katika denial state but now we're on the same page. ZNZ haihitaji mkataba mwingine kabla ya kuvunja uliopo.
of course isingeweza; lakini Zanzibar ilipokuwa huru na majeshi yake na kila kitu chake iliomba Tanganyika msaada wa kutuliza mapinduzi! Zanzibar hata ikiwa na kila kitu chake na vifaru vyake si tishio kwa namna yoyote kwa Tanganyika. Ila Tanganyika itaendelea kuweka kivuli Zanzibar (iwe ndani ya Muungano au nje).
ZNZ wanataka mkataba upi kabla ya kuvunja huu uliopo? Ahali wangu, hakuna shaka WZNZ hawajui wanataka nini.Nguruvi3.
Ndio maana nakwambia huujui hata kidogo muungano wenu ni wa aina gani na ndio maana kila wakti unakuwa mtu wa kupinga.
Ngoja nikudarsishe kidogo hapa kuhusu muungano wenu.
Kwa kukusaidia Ahali yangu Muungano wenu SIO WA KIKATIBA BALI NI MUUNGANO WA MKATABA. Kwani kila nchi ina Katiba yake na sharia zake za ndani isipokuwa kwa mambo yale tu mliokubaliana katika MKATABA
Na vile vile unatakiwa kujua hata Znz ikiwa huru na kila kitu chake, Tanganyika itakuwa si tishio kwa namna yoyote kwa Znz.
Lakin kuna suala dogo nilikuuliza.
Je kama kunatokea maasi upande wa Tanganyika kwa kuwafukuza waZnz, je Znz itakuwa na ubavu wa kutoa majeshi kwenda kuzuia maasi hayo.
ZNZ wanataka mkataba upi kabla ya kuvunja huu uliopo? Ahali wangu, hakuna shaka WZNZ hawajui wanataka nini.
Hili swali ni la kinafik. WaTanganyika hawawezi kuwafukuza waZanzibari lakini waZanzibari wanaweza. Swali lingekuwa je Tanganyika itaweza kusimama kimya wakati raia zake wanatendewa unyama Zanziba? Je, ingekuwepo Tanganyika, viongozi wake wangenyamaza tu wakati raia wake wanachomewa sehemu zao za biashara? Mimi nadhani wasingekaa kimya lakini wasingevamia nchi ya Zanziba kuwanusuru raia wake. Lakini Zanziba ingeendeleza wimbi hilo bila shaka Tanganyika wangetuma askari wake kuwanusuru raia zake.
WaTanganyika hawawezi kuwafukuza waZanzibari maana hawajawahi kutaka kuweka tofauti kati ya mZanzibari na mTanganyika. MZanzibari anaweza maana siku zote amekuwa akitofautisha mZanzibari ni nani na mTanganyika. Na mara nyingi amefanya hivi ili kumpunguzia usawa mTanganyika. Palikuwa na wakati mTanganyika alihitaji kibali maalum kuoa binti wa kiZanzibari. Kuna wakati mTanganyika alihitaji pasi kutembelea Zanziba. MTanganyika amezuiwa kumilki ardhi Zanziba. Jaribio la kutaka MTanganyika aombe kibali cha kufanya kazi Zanziba lilishindwa kwenye BLW kwa kura chache. Leo hii kuna zoezi la kutoa vitambulisho vitakavyoonyesha nani mZanzibari na nani mgeni. MTanganyika akiwa katika kundi la mgeni. Baada ya kumtofautisha hivyo na kumfanya kiumbe cha chini kuliko mZanzibari ni hatua ndogo kuchukua hatua za kumfukuza. Kama vile mlivyofanya baada ya kufanya mapinduzi na kuainisha waarabu kuwa si waZanzibari. Mliwachinja, kuwafukia kwenye visima, kuwafungia kwenye viwanja vya michezo vilivyogeuzwa kuwa concentration camps n.k. Ni waTanganyika waliowapokea hao mliowakataa kuanzia Sultani wenu. Mlipotaka kufanya orgy ya kuchinja baada ya kuuawa kwa Karume, ni Tanganyika iliyowapa hifadhi wakina Babu. Mlipoanza ubaguzi wa wazi dhidi ya wapemba, ni waTanganyika waliowapa hifadhi Sharif Shamba, Namanga na maeneo mengine Tanganyika bila kuwabagua kwa aina yeyote. Wakati nyinyi mliwaona waPemba waTanganyika waliwakubali kama waTanzania wenzao! Leo hii ni baadhi ya viongozi wenu ambao wanapaza sauti wakiongea lugha ya kebehi na matusi dhidi ya waTanganyika. Utashangaa nini kama hao hao mara baada ya kupata uhuru hawatatangaza Zanziba kwa ajili ya waZanzibari na kuwafukuza wanyamwezi wote! Yote haya unayaona lakini bila aibu unadiriki kudai kuwa ni waTanganyika ndio watakaowafukuza waZanzibari? Kitakachotokea ni kuwa baada ya Muungano kuvunjika, waTanganyika hawataona taabu kuwakubali waZanzibari wote watakaochaguwa kuwa raia wa Tanganyika. Swali ni kuwa, waZanzibari watakubali kuwapa uraia wanyamwezi wote amabao watataka kuwa raia wa huko? Sisi tutaendelea kuwapokea kama tulivyowapokea viongozi wenu waliostaafu na wajane wao. Lakini kama Tanganyika hatutakubali kuangalia wakati mnawatendea dhulma waTanganyika wenzetu. Mkifanya hivyo mtaukumbuka Muungano. Kama wanavyosema waChina, uwe mwangalifu unachomuomba Mwenyezi maana anaweza akakupa!
Amandla.............................
ZNZ wanataka mkataba upi kabla ya kuvunja huu uliopo? Ahali wangu, hakuna shaka WZNZ hawajui wanataka nini.
Kama kawaida yako, unatumia mifano isiyofaa.Fundi Mchundo,
Labda ulikuwa mdogo sana ima ujazaliwa wakti ilipovunjika Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC). Itakumbukwa kuwa Watanzania waliwafukuza wakenya na Waganda wote kama nchi hizo navyo zilipowafukuza raia wasio wake.
Sasa kama waliweza kuwafukuza wakenya na waganda ilipovunjika EAC watashindwaje sasa kuwafukuza WaZanzibari?
Au ndio kisebusebu na kiroho papo?
Kwanini tuweke msimamo! Kwa shida gani hebu fafanua! Do we need ZNZ in any way!Mimi nafikiri waZanzibari wapo wazi saaaana na kila wakti wanasema msimamo wao hivi ni wakti muafaka kuungalia kwa kina sana muungano wenyewe kabla ya kuangalia kero za muungano kwa vile Muungano umechangi kwa kiwango kikubwa kuathiri sekta ya uchumi visiwani.
Na wapo tayari kwa lolote litakalo amuliwa na mjadala huo.
Labda na wewe utudadavulie maana yake hakuna sehemu yoote WATANGANYIKA walipoweka Msimamo wao kuhusu Muungano. Tupe msimamo wenu?
Mimi nafikiri waZanzibari wapo wazi saaaana na kila wakti wanasema msimamo wao hivi ni wakti muafaka kuungalia kwa kina sana muungano wenyewe kabla ya kuangalia kero za muungano kwa vile Muungano umechangi kwa kiwango kikubwa kuathiri sekta ya uchumi visiwani.
Na wapo tayari kwa lolote litakalo amuliwa na mjadala huo.
Labda na wewe utudadavulie maana yake hakuna sehemu yoote WATANGANYIKA walipoweka Msimamo wao kuhusu Muungano. Tupe msimamo wenu?
Barubaru, madai ya Zanzibar ni kwamba Muungano umegeuza Zanzibar kuwa koloni la Tanganyika. Na kwenye post yako (kwenye red) unasema kuwa Muungano umechangia kwa kiasi kikubwa kuathiri uchumi wa Visima. Assuming hayo madai ni ya kweli.
Now, in your right mind kwanini Zanzibar watake Mkataba na huyu mkoloni aliyeathiri uchumi wake (Visiwani) kwa kiasi kikubwa kama unavyodai? Ni kwanini Zanzibar msijenge uzio wa nguvu Chumbe ili kujikinga na huyu mkoloni?
Pili, hapo ulipo-underline, sio kweli. Zanzibar hawako tayari kwa lolote, na ndio maana mnataka Mkataba. The only way unaweza kusema Zanzibar iko tayari kwa lolote ni kuachana na hizi chorus za kitoto za Mkataba na kuvunja muungano kimoja.
Maalim Seif na wenzake wanawaaminisha watu kuwa 'Zanzibar iko tayari kwa lolote' na kwa bahati mbaya wapo-tena wengi tu wanaoamini hizo hoja bila kuuliza kama kweli wako tayari kwanini wanamng'ang'ania mkoloni? Kwanini asimalize hii issue BLW? Kwanini asiwapige marafuku wabunge wake kuja Dodoma? Mkataba wa kitu gani, wa ATM?
Mwisho, Kama umefuatilia vizuri utagundua kwamba Muungano sio issue kubwa sana kwa Tanganyika, na sababu kubwa ni kuwa Zanzibar can vanish from the map of this planet and it will not affect Tanganyika one bit! Sanasana ajira zitarudi kwa Tangayika.
Kwa Tanganyika, watu wanajua huduma duni za afya hazitokani na Muungano, barabara mbovu hazitokani na Muungano, ukosefu wa madawati shuleni hautokani na Muungano. Na nguvu kubwa ya watanganyika inaelekezwa kwenye hayo matatizo.
Niliwahi kuuliza, lakini naomba niulize tena, ahadi za Seif za kuifanya Zanzibar kuwa Singapore zimefikia wapi?
Kwanini tuweke msimamo! Kwa shida gani hebu fafanua! Do we need ZNZ in any way!