Wapiga kura kataeni rushwa-Tanzania

Wapiga kura kataeni rushwa-Tanzania

mabutu1835

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2018
Posts
1,136
Reaction score
1,916
Ni takribani miaka 64 tangu Tanganyika ipate uhuru na miaka 61 tangu Muungano uliopelekea kuzaliwa taifa la Tanzania.

Kwa miaka yote hiyo vitendo vya rushwa vinasikika na kuonekana katika kila ngazi ya uchaguzi. WAPIGA kura wanapokea rushwa za kifala kabisa eti chakula au vijihela.

Hata wapiga kura ndani ya vyama wanapokea rushwa. Eti mwenye Nia ya kugombea anatoa elfu 30 wagawane elfu 3, Hii ni aibu na laana.

NI BORA KUFANYA MAKOSA KATIKA KUMCHAGUA MTU UKIWA HUJALA RUSHWA YAKE.
UMEFIKA WAKATI WA KUWAPA KURA WASIOTOA RUSHWA NA KAMA HAKUNA MGOMBEA ASIYETOA RUSHWA INATOSHA KUSEMA HAKUNA HAJA YA KUPIGA KURA.
 
Hivi pesa ya rushwa inamlazimisha vipi mpokeaji kumpigia kura mtoaji kwenye kura ya siri?
 
Back
Top Bottom