Nadhani wote wanalipa ila takwimu za TRA kuhusu walipa kodi zinasemaje?
Na kama wanalipa kodi,mbona hawatajwi popote linapokuja suala la kuwaletea maendeleo wananchi bali linatajwa jina moja tu pindi mradi wowote wa maendeleo unapotekelezwa?
Watanzania wote tunalipa kodi nyingi sana na kuchangia pato la taifa. Kuna waliosaliwa ambao wanalipa both indirect and Direct tax na wale ambao hawajasiliwa rasmi ambao wanalipa Indirect tax kutokana na matumizi ya pato lao ambao ndio wengi. Katika walipa kodi walisajiliwa rasmi kuna walipa kodi wakubwa na wadogo pia.
Mambo ni mengi kwenye kodi ila hakuna mtanzania asiyelipa kodi hata uwe umelala kitandani kwa ugonjwa