Wapiga debe wasiokuwa na sare kufukuzwa leo Ubungo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wapiga debe wasiokuwa na sare kufukuzwa leo Ubungo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 23, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,982
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Wapiga debe wasiokuwa na sare kufukuzwa kesho Ubungo Saturday, 22 January 2011 20:07

  Mariam Sagafu, MUM

  HATIMAYE lile agizo lililotolewa hivi karibuni na Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu la kuwataka wapiga debe wote wasiokuwa na sare za kuwatambulisha mabasi yao wanayofanyia kazi waondoke katika kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo (UBT) jijini Dar es Salaam litaanza rasmi kesho kituoni hapo.

  Wakizungumza jana na Mwananchi kwa nyakati tofauti kituoni hapo, baadhi ya wapiga debe hao walisema matangazo yalitolewa juzi na jana eneo hilo kupitia vipaza sauti kituo hapo, yaliyosema kuwa siku ya Jumatatu watafukuzwa kama hawataondoka kwa hiyari yao.

  “Tutafurahi sana kama zoezi hili likifanyiwa kazi kwani wapiga debe wasiokuwa na sare wengi wao ni wezi na kesi nyingi zimeshajitokeza na kusababisha ugumu wa kazi yao,” alisema Hassan Issa ambaye ni mpiga debe katika kituo hicho.
  Kwa upande wake, Christopher ambaye alijulikana kwa jina moja alikuwa amevaa sare ya basi la Mohamedi Trans alisema wanaumia sana na mambo yanayofanywa na wapiga debe holela kwani yeye ana mke na watoto watatu na anaishi kwa kutegemea kazi hiyo.
  Mapema wiki iliyopita, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu aliwataka wapiga debe hao wafuate agizo la Waziri kabla serikali haijaanza kuchukua hatua.
  “Napenda kuwapa taarifa wapiga debe hao wafuate agizo la waziri kabla ya serikali haijachukua hatua,” alisema Kenyela.
  Hatua hiyo itakayochukuliwa na uongozi wa kituo inaweza ikaleta usalama zaidi kituoni hapo kwani abiria wengi wamekuwa hawana imani na wapiga debe hata wale waliosajiliwa na mabasi na kuleta ugumu wa kazi yao.

   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,982
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Hili zoezi linapaswa kuwa ni la kudumu....na mkakati uwekwe vibaka wasije wakazishona hizo nguo na kuondoa umaana wa zoezi lote...............kama polisi bandia wanavyosumbua mitaani..................
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Badala ya kuhangaika na matatizo makubwa yanayoeleweka wanang'ang'ana na sare ambazo mtu yeyote anaweza kuzipata!
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Small minor things ambazo watendaji wengine wanaweza kufanya ndio mawaziri wanakimbilia na kuacha mambo makubwa ya nchi ambayo maswali yake hayajajibiwa
   
Loading...