Samahani ndg zangu nilikuwa nje ya mji kidogo. Kuhusu tonses kama zimevimba na zinakusumbua sana basi dawa yake ni kuzitoa kwa kufanyiwa operation.
Binafsi nilikuwa nazo na nikafanyiwa operation kwenye hospital moja iko pale magomeni mwembe chai inaitwa EKENYWA. wao wamespecialize kwenye ENT. Siwapigii debe ila kiukweli huduma zao ni excellent!
Nilivhojifunza baada ya kufanyiwa hii operation nikwamba kwa watoto haisumbui sana kama kwa watu wazima. Mtoto anaweza tumia wiki moja tuu anakula ugali lakn kwa watu wazima kuna complications kidogo itakuchukua almost 2-3 weeks kupona. Japo chakula lazima kiwe rojorojo kwa wiki ya kwanza na ya pili
Wiki ya kwanza chakula chako ni Uji, maziwa fresh, mtori, ice cream, Big G original na juice zote ambazo hazitakiwasha kwenye jeraha
Wiki ya pili na yatatu chakula ni
Bokoboko ya ubwabwa, juis, ugali mlaini sana na mrenda(wa mhogo unafaa zaidi)
N:B baada ya operation hadi kupona epuka vyakula vyenye citrus acid, vyenye ncha kali kama chips, nafaka kama karanga, nyama n.k
Ukiwa na bima pale EKENYWA hutotakiwa kulipia fedha yoyote tofauti na vipimo na chanjo ya homa ya ini utakayopewa baada ya operation (45,000/). Mambo mengine kama operation, dawa kabla na baada ya huduma, kitanda vyote viko kwenye bima
Ukishaonana na Dr na akakushauri kuwa utafanyiwa operation basi utapangiwa siku ya operstion na utapewa dawa za vidonge za kumeza siku tatu za mwisho kuelekea siku ya operation. Na operation inachukua kama 45 mins to 1:30 hrs, utapigwa nusu kaputi hivyo hutosikia maumivu yoyote yale wakati wa operation.
Nikushauri kitu,
Ukishafanyiwa operation omba kukaa hospital kwa siku tatu ya nne ndo utoke. Kwasababu baada ya hiyo tonsillectomy kuna dawa utakuwa unapewa kwa kupitia mishipa yaaani ziko effective sana kuliko vidonge ukipewa ukamezee home.
Karibu kwa maswali. Maana mimi nilitolewa pia hizo tonses mwaka huu mwanzoni na kwasasa niko vzuri sana hakuna kukoroma tena wala harufu mbaya mdomoni wala kutema makohozi mara kwa mara