Wapi nitapata matibabu ya tonsils sugu?

stevhinoz

JF-Expert Member
Jun 15, 2021
216
480
Katika ukuaji wangu sikuwa naugua ugonjwa wa tonsils mara kwa mara ilikuwa inatokea kwa nadra sana.
Miaka mitano nyuma nilikuwa kikazi ukanda wa nyanda za juu kusini kikazi ndio ugonjwa wa tonsils ukawa ni kama ugonjwa wangu wa kudumu.
Nikinywa kitu chochote cha baridi baada ya dakika tano ugonjwa unaanza.

Hapa nilipo sinywi kitu chochote cha baridi kwa miaka zaidi ya mitatu na nikijaribu iwe soda, maji, juice, ice cream au chochote kesho yake nalala ndani kwa homa kali.

Nimekuwa natumia antibiotics kutibu tonsil lakini naona nitakunywa hizi dawa mpaka lini? Nitaacha kunywa/kula vitu vya baridi mpaka lini?

Naomba mwenye kufahamu tiba ya kudumu inapopatikana iwe hospital au kienyeji anisaidie nimalize ili tatizo, naamini kuna watu walishapitia hali kama yangu na sasa washasahau hii dhahma. Au kuna wenye utaalam wa tiba wanaweza nisaidia ushauri.

Natanguliza shukrani
 
Mkuu pole sana kwa hayo maradhi yako ya tonsils sugu nitafute mimi kwa wakati wako ili niweze kukutibia maradhi yako uguwa pole.
 
Pole mkuu chukua mkaa wa moto ambao bado unawaka dumbukiza kwenye glasi ya maji wakat ule mkaa unalalamika kuzima we unakunywa yale maji usisubiri mpaka uzime no ni pale unalalamika kuzima unakunywa yale maji alafu utapona hilo tatzo
 
Duh hii unafanya kwa muda gani au mara moja tu?
 
Katika ukuaji wangu sikuwa naugua ugonjwa wa tonsils mara kwa mara ilikuwa inatokea kwa nadra sana.
Miaka mitano nyuma nilikuwa kikazi ukanda wa nyanda za juu kusini kikazi ndio ugonjwa wa tonsils ukawa ni kama ugonjwa wangu wa kudumu.
Nikinywa kitu chochote cha baridi baada ya dakika tano ugonjwa unaanza.

Hapa nilipo sinywi kitu chochote cha baridi kwa miaka zaidi ya mitatu na nikijaribu iwe soda, maji, juice, ice cream au chochote kesho yake nalala ndani kwa homa kali.

Nimekuwa natumia antibiotics kutibu tonsil lakini naona nitakunywa hizi dawa mpaka lini? Nitaacha kunywa/kula vitu vya baridi mpaka lini?

Naomba mwenye kufahamu tiba ya kudumu inapopatikana iwe hospital au kienyeji anisaidie nimalize ili tatizo, naamini kuna watu walishapitia hali kama yangu na sasa washasahau hii dhahma. Au kuna wenye utaalam wa tiba wanaweza nisaidia ushauri.

Natanguliza shukrani
tonsillectomy
nenda kwenye Clinic za Ent watakusaidia
 
Samahani ndg zangu nilikuwa nje ya mji kidogo. Kuhusu tonses kama zimevimba na zinakusumbua sana basi dawa yake ni kuzitoa kwa kufanyiwa operation.

Binafsi nilikuwa nazo na nikafanyiwa operation kwenye hospital moja iko pale magomeni mwembe chai inaitwa EKENYWA. wao wamespecialize kwenye ENT. Siwapigii debe ila kiukweli huduma zao ni excellent!

Nilivhojifunza baada ya kufanyiwa hii operation nikwamba kwa watoto haisumbui sana kama kwa watu wazima. Mtoto anaweza tumia wiki moja tuu anakula ugali lakn kwa watu wazima kuna complications kidogo itakuchukua almost 2-3 weeks kupona. Japo chakula lazima kiwe rojorojo kwa wiki ya kwanza na ya pili

Wiki ya kwanza chakula chako ni Uji, maziwa fresh, mtori, ice cream, Big G original na juice zote ambazo hazitakiwasha kwenye jeraha
Wiki ya pili na yatatu chakula ni

Bokoboko ya ubwabwa, juis, ugali mlaini sana na mrenda(wa mhogo unafaa zaidi)
N:B baada ya operation hadi kupona epuka vyakula vyenye citrus acid, vyenye ncha kali kama chips, nafaka kama karanga, nyama n.k

Ukiwa na bima pale EKENYWA hutotakiwa kulipia fedha yoyote tofauti na vipimo na chanjo ya homa ya ini utakayopewa baada ya operation (45,000/). Mambo mengine kama operation, dawa kabla na baada ya huduma, kitanda vyote viko kwenye bima

Ukishaonana na Dr na akakushauri kuwa utafanyiwa operation basi utapangiwa siku ya operstion na utapewa dawa za vidonge za kumeza siku tatu za mwisho kuelekea siku ya operation. Na operation inachukua kama 45 mins to 1:30 hrs, utapigwa nusu kaputi hivyo hutosikia maumivu yoyote yale wakati wa operation.
Nikushauri kitu,

Ukishafanyiwa operation omba kukaa hospital kwa siku tatu ya nne ndo utoke. Kwasababu baada ya hiyo tonsillectomy kuna dawa utakuwa unapewa kwa kupitia mishipa yaaani ziko effective sana kuliko vidonge ukipewa ukamezee home.

Karibu kwa maswali. Maana mimi nilitolewa pia hizo tonses mwaka huu mwanzoni na kwasasa niko vzuri sana hakuna kukoroma tena wala harufu mbaya mdomoni wala kutema makohozi mara kwa mara
 
Pole sana mkuu,,,unaweza ukaenda hospital
Ukafanyiwa operation ya kuziondoa na tatizo likaisha kabisa
 
Tonsils ni part of sensory receptors ambazo hukupa taarifa ya uwepo wa bacteria wabaya kwenye mwili wako ambao wamekuingia kwa njia ya hewa au kumeza kitu kilichowabeba.

Bacteria wanasafiri kwa njia ya hewa na maji maji kuingia mwilini. Unaweza kuwa umevuta hewa yenye vimelea vya bacteria au umetumia maji, chakula, kinywaji kilichoandaliwa kwa maji ambayo si salama na yamebeba bacteria wengi.

Sababu yako ya kupata chronic bacterial infection inaweza kuwa inahusiana na matumizi mabaya ya dawa zozote zenye asili ya antibiotics au matumizi ya dawa zenye nguvu inayosababisha kidhoofu kwa kinga ya mwili au vyote kwapamoja ikichangiwa na lishe duni.

Kukushauri kama ni mtumiaji sana wa dawa kali especially antibiotics na zinginezo basi upunguze kama sio kuacha kabisa, nenda kapate vipimo hospital wakupe picha halisi ya mwili wako kiafya.

Kukusaidia zaidi, chukua maji ya moto wastani ambayo utaweza yaweka na kusukutulia mdomoni mwako, weka chumvi kwa uwiano wa 250 ml kijiko cha chakula kimoja. Halafu tumia hayo maji kujigurgle kooni yaani ile kuweka maji kooni bila kuyameza ukisukutua.

Itakusaidia kuwashambulia hao bacteria hapo kooni na kuwapunguza kwa kasi sana na hatimae kuwatokomeza kabisa wasiwepo hapo kooni.

Usiishie hapo, tafuta vidonge vya vitamin C na D au ukikosa then fanya upate vile vya multivitamin itakuwa poa zaidi. Umeze kwa maelekezo ya pharmacist atayokupa.

Ongezea na kutumia maji ya limao yaani Lemonade kwa vipimo hivi, maji yaliyochemshwa jikoni ukatia mdalasini yakapoa vizuri hata yakiwekwa kwenye friji yakapoa ni sawa tu. Hayo maji unakamulia limao kubwa zile moja na nusu au hata mbili, kisha unaweka asali (kama ni mtumiaji wa asali). Ila unaweza kuweka sukari kwa kiwango kidogo tu. Then unakunywa kama juice.

Vitamin C inaboost sana Immunity yaani kinga ya mwili, na vitamin D inamsaada sana kuzisaidia seli zako kuweza kufyoza virutubisho kama vitamin C na vinginevyo kwa haraka na urahisi.

Limao inabeba vitamin C kwa wingi sana lakini pia ina vihuisho vya seli na kuzipa uwezo wa kuzaliana kwa wingi zaidi ikiwa kuzipa ufanisi kuputia nourishment.

Najua ukienda hospital utapewa antibiotics, sikushauri utumie. Hazitakupa unafuu.

Kwa ushauri zaidi unajua namna ya kunipata.
 
Pole sana mkuu,,,unaweza ukaenda hospital
Ukafanyiwa operation ya kuziondoa na tatizo likaisha kabisa
Haishauriwi kutoa hizo kitu sababu zinafanya kazi yake. Kutoa tonsils ni sawa na kutoa thermostat kwenye gari ili isikupe taarifa juu ya jotoridi la gari eneo la engine.
 
Back
Top Bottom