Dr.adams faida
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 1,885
- 3,343
Habari za Jumapili hii ndugu zangu. Kiafya mimi niko vyema kabisa, wacha niende moja kwa moja kwenye mada.
Nimekuwa nikifanya uchunguzi juu ya biashara ya ufyatuaji tofali nikaona soko kubwa lipo mijini kwa maana wajenzi wengi ndipo walipo. Nimekaa nikafikiri na kugundua kuwa wajasiriamali walio wengi wanaouza tofali wengi wao hawafungui matawi madogo madogo pembeni ya miji ambapo watu wengi hukimbilia kujenga maeneo hayo.
Sasa basi linapokuja swala la ujenzi watu hawa wanapata taabu kwenye swala la tofali kwani wengi wao huwabidi waende mijini kununua tofali ambapo kuna machine za umeme za kufyatua tofali.
Gharama za usafirishaji huwa ziko juu na pengine mteja hufikisha tofali zikiwa baadhi zimeharibika kwa kupasuka kutokana na ubovu wa miundo mbinu ikiwemo barabara kuwa mbovu.
Mteja katumia gharama kununua tofali let say kanunua tofali kwa bei ya 850/=@ tofali, mpaka kuzifikisha site na amechukua tofali 1000 ambayo thamani ya 850000/=. Mteja huyohuyo anafikisha tofali hata 20 zimevunjika ambayo ni sawa hasara ya shilingi 17000/=.
Nimekaa nikafikiri niteke soko kwa watu waliopembeni na miji wanaofanya ujenzi nianzishe mradi wa kufyatua tofali kwa kumfata mteja palepale site nitafute vijana 10 wapate utaalamu wakuzitumia mashine,pia ninunue machine kama 6 hivi niingie mitaani kuzisaka pesa nitajitahidi nahakikisha natoa bidhaa zilizo bora zaidi.
Biashara hii nimependa niifanyie Kahama kwa maana ni mji unaokua kwa kasi ya ajabu. Makazi yangu yapo Dar es Salaam ila nitafanya niwezalo ili niweze kusimamia mradi wangu.
Mwisho nataka nipate uzoefu kwa walionitangulia kwenye hii project ikiwemo changamoto zake.
Pia wapi nitapata mashine yenye ubora kwa bei nzuri?