Kuna fujitsu lifebook sio slim sana ila ni slim kiasi na bei pia sio mbaya 350k ina 4th gen niliwahi nunua Discountkubwa siku si nyingi
Na ukaaji chaji ni wa kawaida.
Kama unataka ukaaji chaji sana na iwe slim unatakiwa utafute angalau 6th gen. Kuna duka fulani linaitwa awale kama sijakosea swahili na uhuru ni la wasomali, wanazo hizi 2 in 1 nyingi na bei zao ni humo humo around laki 6 sema kuwa makini refurbished nyingi zina matatizo unatakiwa uikague kwa umakini, na uchukue warranty ya duka hata miezi 3.
Njia nyengine safe ni kununua mpya ila zitakuwa sio core series bali hizi pentium na celeron. Kwa laki 7 unaweza pata zaa Apollo lake ama Gemini lake, zina nguvu kwa hizo kazi zako, na ukipata yenye ssd ni nzuri zaidi, pia zipo convertible kibao za Hizi pentium na celeron.
Sema uwe makini sana kuna pentium na celeron nzuri na zipo vimeo.
Nzuri sana
Pentium N5000
Celeron N4100
Celeron N4000
Nzuri kawaida
Pentium N4200
Celeron 3450
Celeron 3350
Za kuziepuka
Pentium N3710
Pentium N3700
Celeron N3160
Celeron N3150
Celeron N3060
Celeron N3050
Celeron N3010
celeron N3000