kwa mtazamo wangu kuna mahali unakosea. nako ni kama ifuatavyo.,
1. umeshirikisha watumishi wa Mungu ni vizuri sana lakini zaidi mshirikishe Rhoho Mtakatifu akufishe namna halisi ya kumjua mke wako na kukuwezesha kuishi kwa amani huku ukifurahia ndoa yako. biblia inasema, ' Enyi waume ishini na wake zenu kwa akili...'
2.usijihesabie haki kuwa wewe ni mkamilifu zaidi ya mwenzako kwa sababu tu hujawahi kushiriki ndoa kabla yake, jitahidi kujenga katika fikra zako kwamba huyo ndo mwanamke bora kwako na sahau habari ya kwamba alikuwa na mahusiano kabla yako.