Wapi nakosea?

Wapi nakosea?

Una roho mbaya. Hivi kama ukimsaidia tu utapata hasara gani . Kumbuka mabao yake yenye afya ndio yamekufanya uwe binadamu as ulivyo . Katika maisha yako umewahi kuwasamehe wangapi. Na wewe umewahi kusamehewa mara ngapi. anyway haya muache mzee wako aadhirike hadi afe na wewe jisifu na mafanikio yako

Nahisi wewe akili zako hazipo sawa,na hujasoma stori yote ukaelewa pia hujawahi pitia tabu hata kidogo kwenye maisha ndo maana unakurupuka kumshambulia.Jichunguze nahis utagundua umeandika pumba na mashudu hapa.
 
Forgiving and Forgetting is the first step towards healing such wounds my friend.
...come on now! forgiving n forgetting is actually impossible for a situation like his...
 
Fanya hivyo ndugu....wewe mshukuru Mungu umepewa kujitambua mapema,yeye hakupewa huo upeo..pengine hata mama asingekufa mapema....we jifanye zuzu tu nenda fanya yako kisha urudi dsm..angekua mzima walaaa!!!

kua nae karibu wakat wa matatizo......wakati wa furaha yake yeye ndio awe wakwanza kukutafuta....

hutapungukiwa chochote.

Ni kweli kabisa kabisa!tena kwa kumjali na kumuona ndo mungu anazidi kukufungulia milango ya baraka
 
Nashukuru sana, nafanya mchakato wa ruhusa ofisini ya wiki 1 niende nikamuone!

pole na hongera kwa uvumiluvu na busara.naaminpi hadi kufikia hapo moyo wako.unakuongoza vyema.ipo.cku utasahau yote.
 
Pole saana , life is full of challenges. pamoja na yote uliyoyapitia still huyo ndiye ur real papa. Msamehe tu na through kumsamehe utafanikiwa 1000000000 times. kuhusu kumsaidia , msaidie vile uwezavyo achana na lawama maana binadamu ufanikiwapo kila mtu anatamani uwe ATM yake. Hata wakulaumu vipi upatapo nafasi ya kumsaidia mzazi wako hiyo ni tunu na roho ya utu ambayo utaipandikiza hata kwa wanao na vizazi vyako vyote.

Keep it up ukijua Mungu yupo upande wako.
 
slim5 are serious hii ni issue iliyokutokea au story tu? kama ni kweli pole kwa yaliyokukuta aiseeee
 
Last edited by a moderator:
Thanks Karucee,sometimes the regular challenges make life more interesting.To give up and cry is not the way to handle situations that demand our intelligence....it is better to seek solutions instead of crying over the problems in life.nafikir kila mwanadamu anahitaji kupewa second chance ila nawish one day nami nitakutana na my lovely father.
May your wish be granted young man.
 
pole sana..ur the.hero u.came from zero to hero..msaidie kadri uwezavyo..baba ni mmoja tu duniani huwezjua nani alikua na kosa kati yake na mama..wewe mpende na mhudumie kadri uwezavyo..isimnyanyapae
 
Mmh huruma hii jaman kwa kweli mungu ni mwema kila siku endelea kumuombea kwa mwenyez mungu aweze kupona lakin pia ni vizur ukaenda kumuona mmalize tofauti uishi kwa aman ya moyo.
jaman mzazi ni mzazi tu hakuna jinsi
 
Mhh kwanza hongera mana dah..yataka moyo kwa kweli,poleh sana with ur background jmn...omba Mungu akupe moyo wa kumsamehe,then mhudumie utakavoweza,mengine muachie Mungu
 
Mimi nadhani mpaka unamsaidia kumpa support, nikupe hongera tu, mana wazazi kama hao wengine tungeshamzika mioyoni mwetu ili hali yupo... tena mzima wa afya.
 
SOMO – WAPI NAKOSEA?
Nikiwa mtoto niilifurahia maisha yangu ya utoto kama watoto wengine. Nilipokuja kupata akili za kipindi cha utoto, nilianza kupata maumivu kama mtoto kutokana na kutokuwepo kwa baba! Ile kutokumjua baba tu kwangu ilikuwa ni adhabu tena kubwa sana! Niliumia shuleni, niliumia nyumbani kila watoto wenzangu wanapotumia msamiati “baba”. Muda wote wa utoto na maisha ya elimu ya msingi nimekuwa nikiamini kuwa nina mzazi mmoja tu – MAMA! Huyu kwangu alikuwa both, a mother and a father at all time! Ni aina ya mama ambaye alijitambua, na alijua nini kinampasa kufanya katika mazingira ya kuachiwa watoto wawili wa kiume na mwanaume ambaye si tu aliingia mitini, hakugeuka nyuma, bali pia hakutaka kuskia wala kusimulia chochote kuhusu yeye kuwa na watoto wawili wa kiume somewhere in Tanzania!
Hapa namzungumzia “baba” ambaye aliyakimbia majukumu ya kifamilia si kwa vile hakuwa na kipato, laa hasha, alikuwa financially powerful, mtu na ajira yake, mtu na pesa zake! Alikuwa mmoja watu wenye nyadhifa ktk taasisi aliofanyia kazi! Aliishi maisha ya anasa na starehe, wanasema alikuwa mzuri katika anasa za dunia, wapenda anasa wanasema alikuwa mtu mwema sana! Haya yamesemwa na watu wake wa karibu, ndg na jamaa zake waliokuwa nae, akiwemo dadake! Mpaka naandika uzi huu, sijawai kujua nini kilimuachanisha na mamangu mpendwa (rip) na bahati nzuri pia sikuwai kuwa na haja ya kujua sababu!

Maisha ya wakati wa utoto yalikuwa magumu sana, mama hakuwa na uwezo wa kumudu gharama za maisha kwa familia yake kwa kiwango chote, alijitahidi kadri ya uwezo wake kuzimaliza changamoto zetu, na tulimshukuru mungu kwa kile kidogo alichotupatia (rip my hero mama). Pia tulimshukuru mungu kuwa na mama huyu! Bahati iliyopo ni kwamba tulikuwa na uwezo darasani, mimi na kakangu na bahati ikaja tukafaulu la 7 kwenda sekondari! Haya yanatokea baba hajulikani yu wapi! Hajui watoto tu wapi!

Mama aliugua, na 12[SUP]th[/SUP] April 1996 my mama gone to glory [rip mama]. From here, the situation became worse than before! things turned upside – down to my side!
Na mwishoni mwa mwaka huo ndio kwa mara ya kwanza nakutanishwa na baba, I was 18 yrs old! Naikumbuka ile conversation: Tukiwa mezani tunakula, shangazi anamuuliza baba, huyu kijana hapa unamjua? (mm na baba tukiwa tunatizamana mezani). Baba anamjibu hapana! [akilini baba alihisi dadake kapata new shamba boy] then anaambiwa huyu ni ********! Baba anashtuka! Taharuki! Ananiuliza: “ninyi mpo wawili, wewe ndio mkubwa ama mdogo?” [wanaume wenzangu hata kama hawa kinamama wana matatizo yao, tusifikie hatua hii] Halafu akaniuliza kuhusu mama, nikamjibu tumemzika mwaka huu! Taharuki! Shangazi anadakia mazungumzo yetu, anamuelezea kwa niaba yangu kuhusu msiba huo, nilishaanza kulia! Shangazi alibahatika kuhudhuria mazishi ya mama.

Nayakumbuka sana maisha yangu ya sekondari, maisha ya mtaa yalinifundisha kitu more or less similar to what I learnt in school system. Nilipokuwa kidato cha pili tayari nilishajua namna ya kufanya biashara za kimachinga tena za aina mbali mbali ktk jiji la DSM (nikienda DSM wakati wa likizo) nyakati ambazo wenzangu wanahaha kubadili tuition 1 baada ya nyingine kutafuta walimu wazuri!

Mpaka nafika Form 4 nilishajua kuuza misokoto, nilishamjua pusha, nilishajua nini maana ya booster! Nilishakuwa na uhusiano wa karibu na mateja! Najua bidhaa yao inapatikanaje pale mkoani kwetu! Nilishajua namna gani DSM mzigo unaingia! Kwa nini nisijue wakati walionifadhili maisha yangu ya mtaani na shuleni, hizo zilikuwa shughuli zao za kila siku! Katika njia hii nilimpoteza my only lovely brother (rip brother). Pengine kukosa muongozo kulichangia, na pia labda iliandikwa iwe – ikawa! Thanks lord I had never used such a stuff! Wana-JF mnajua madhara ya mtoto wa rika la sekondari kukosa muongozo wa maisha, kukosa mtu wa kumsimamia kwa karibu! Kumuacha mtoto wa umri huu afanye anachoweza! Hayo maisha niliyapitia!

To cut the story short! Nilifanikiwa kumaliza A – level, nikafanya undergraduate, then nikafanya postgraduate udsm. Nina ajira yangu ya serikali! A good loving wife ambae nilikutana nae kipindi cha dhiki iliopitiliza (kama unasoma huu uzi, jua nakupenda sana, una maana kubwa sana kwangu). Tumebahatika kupata 2 baby girls! Mkubwa anasoma shule nzuri, mdogo is only 1.5 yrs old.

Turudi kwa “baba”. Yupo ktk maisha yake ya uzee. Vijana wanasema amefulia! Amebaki kuwa ni mkulima wa hapa na pale. Sasa hv anapigania afya yake hospitalini, anaumwa huko aliko. Namhudumia na kumpa msaada [tigopesa, mpesa zinahusika hapa] kadri ninavoona naweza. Watu wake wa karibu (wengi wao nawaskia kwa majina tu mf. Baba mdg, baba mkbw n.k) wananilaumu kuwa sijajitolea kiwango cha kutosha! Sijajitolea kama mtoto anavojitolea kwa mzazi wake! Wanasema sina mapenzi na baba. Mimi najua mapenzi ni natural, an inborn attitude, huwezi ambiwa PENDA na wewe UKAPENDA! Kweli sina mapenzi nae, lakini nambieni naanzia wapi kumpenda “baba”? Naendelea kupokea lawama! Unaesoma uzi huu, naomba nasaha zako, hapa mimi nakosea wapi? Pia zingatia kuwa mimi ni mwanadamu, kama ambavyo yeye pia! Siwezi kuvaa viatu vya kulipiza, ila haya ni maisha yangu na yeye ana maisha yake!

Pole kaka I feel it too...I just passes a somewhat a similar kind of life 'single parent" and the worst thing is my daddy passed away one year ago hzo lawama za kutompenda baba nilizipokea sana tu and some even said umefurah ss babaako kafariki? Unampenda sana mamaako ww kuliko baba..hv utaachaje kumpenda mzazi alieangaika na ww kukusomesha etc? Karma has no menu wazaz wa hvyo wanalupiwa hapa hapa duniani...nilikua naumia nikimuona my step young sister anasomeshwa na nakutana nae mjin anawaka akat huki mama yetu anahangaika na ss (na my young bro) as if we dont have a daddy..anyway RIP dady nisiongee mengi ila jua kaka mwenye post I feel it and I know hw it is be strong do what u can usifatshe wanasema nn live ur own life..saidia unapoweza ukishindwa usijiforce..pole sana
 
Pole kwa mapito hayo.
Kibinaadamu ungetamani mama angekuwepo sasa kufaidi matunda ya malezi yake lakini jua Mungu ana makusudi yake.
Mhudumie baba yako kadri utakavyoweza hasa katika kipindi hiki cha ugonjwa.
Timiza wajibu wako kama mtoto,kwa aliyowafanyia ni ngumu ila inawezekana.
Mwisho wa siku ndio mzazi wako pekee aliyebaki.
 
SOMO – WAPI NAKOSEA?
Nikiwa mtoto niilifurahia maisha yangu ya utoto kama watoto wengine. Nilipokuja kupata akili za kipindi cha utoto, nilianza kupata maumivu kama mtoto kutokana na kutokuwepo kwa baba! Ile kutokumjua baba tu kwangu ilikuwa ni adhabu tena kubwa sana! Niliumia shuleni, niliumia nyumbani kila watoto wenzangu wanapotumia msamiati “baba”. Muda wote wa utoto na maisha ya elimu ya msingi nimekuwa nikiamini kuwa nina mzazi mmoja tu – MAMA! Huyu kwangu alikuwa both, a mother and a father at all time! Ni aina ya mama ambaye alijitambua, na alijua nini kinampasa kufanya katika mazingira ya kuachiwa watoto wawili wa kiume na mwanaume ambaye si tu aliingia mitini, hakugeuka nyuma, bali pia hakutaka kuskia wala kusimulia chochote kuhusu yeye kuwa na watoto wawili wa kiume somewhere in Tanzania!
Hapa namzungumzia “baba” ambaye aliyakimbia majukumu ya kifamilia si kwa vile hakuwa na kipato, laa hasha, alikuwa financially powerful, mtu na ajira yake, mtu na pesa zake! Alikuwa mmoja watu wenye nyadhifa ktk taasisi aliofanyia kazi! Aliishi maisha ya anasa na starehe, wanasema alikuwa mzuri katika anasa za dunia, wapenda anasa wanasema alikuwa mtu mwema sana! Haya yamesemwa na watu wake wa karibu, ndg na jamaa zake waliokuwa nae, akiwemo dadake! Mpaka naandika uzi huu, sijawai kujua nini kilimuachanisha na mamangu mpendwa (rip) na bahati nzuri pia sikuwai kuwa na haja ya kujua sababu!

Maisha ya wakati wa utoto yalikuwa magumu sana, mama hakuwa na uwezo wa kumudu gharama za maisha kwa familia yake kwa kiwango chote, alijitahidi kadri ya uwezo wake kuzimaliza changamoto zetu, na tulimshukuru mungu kwa kile kidogo alichotupatia (rip my hero mama). Pia tulimshukuru mungu kuwa na mama huyu! Bahati iliyopo ni kwamba tulikuwa na uwezo darasani, mimi na kakangu na bahati ikaja tukafaulu la 7 kwenda sekondari! Haya yanatokea baba hajulikani yu wapi! Hajui watoto tu wapi!

Mama aliugua, na 12[SUP]th[/SUP] April 1996 my mama gone to glory [rip mama]. From here, the situation became worse than before! things turned upside – down to my side!
Na mwishoni mwa mwaka huo ndio kwa mara ya kwanza nakutanishwa na baba, I was 18 yrs old! Naikumbuka ile conversation: Tukiwa mezani tunakula, shangazi anamuuliza baba, huyu kijana hapa unamjua? (mm na baba tukiwa tunatizamana mezani). Baba anamjibu hapana! [akilini baba alihisi dadake kapata new shamba boy] then anaambiwa huyu ni ********! Baba anashtuka! Taharuki! Ananiuliza: “ninyi mpo wawili, wewe ndio mkubwa ama mdogo?” [wanaume wenzangu hata kama hawa kinamama wana matatizo yao, tusifikie hatua hii] Halafu akaniuliza kuhusu mama, nikamjibu tumemzika mwaka huu! Taharuki! Shangazi anadakia mazungumzo yetu, anamuelezea kwa niaba yangu kuhusu msiba huo, nilishaanza kulia! Shangazi alibahatika kuhudhuria mazishi ya mama.

Nayakumbuka sana maisha yangu ya sekondari, maisha ya mtaa yalinifundisha kitu more or less similar to what I learnt in school system. Nilipokuwa kidato cha pili tayari nilishajua namna ya kufanya biashara za kimachinga tena za aina mbali mbali ktk jiji la DSM (nikienda DSM wakati wa likizo) nyakati ambazo wenzangu wanahaha kubadili tuition 1 baada ya nyingine kutafuta walimu wazuri!

Mpaka nafika Form 4 nilishajua kuuza misokoto, nilishamjua pusha, nilishajua nini maana ya booster! Nilishakuwa na uhusiano wa karibu na mateja! Najua bidhaa yao inapatikanaje pale mkoani kwetu! Nilishajua namna gani DSM mzigo unaingia! Kwa nini nisijue wakati walionifadhili maisha yangu ya mtaani na shuleni, hizo zilikuwa shughuli zao za kila siku! Katika njia hii nilimpoteza my only lovely brother (rip brother). Pengine kukosa muongozo kulichangia, na pia labda iliandikwa iwe – ikawa! Thanks lord I had never used such a stuff! Wana-JF mnajua madhara ya mtoto wa rika la sekondari kukosa muongozo wa maisha, kukosa mtu wa kumsimamia kwa karibu! Kumuacha mtoto wa umri huu afanye anachoweza! Hayo maisha niliyapitia!

To cut the story short! Nilifanikiwa kumaliza A – level, nikafanya undergraduate, then nikafanya postgraduate udsm. Nina ajira yangu ya serikali! A good loving wife ambae nilikutana nae kipindi cha dhiki iliopitiliza (kama unasoma huu uzi, jua nakupenda sana, una maana kubwa sana kwangu). Tumebahatika kupata 2 baby girls! Mkubwa anasoma shule nzuri, mdogo is only 1.5 yrs old.

Turudi kwa “baba”. Yupo ktk maisha yake ya uzee. Vijana wanasema amefulia! Amebaki kuwa ni mkulima wa hapa na pale. Sasa hv anapigania afya yake hospitalini, anaumwa huko aliko. Namhudumia na kumpa msaada [tigopesa, mpesa zinahusika hapa] kadri ninavoona naweza. Watu wake wa karibu (wengi wao nawaskia kwa majina tu mf. Baba mdg, baba mkbw n.k) wananilaumu kuwa sijajitolea kiwango cha kutosha! Sijajitolea kama mtoto anavojitolea kwa mzazi wake! Wanasema sina mapenzi na baba. Mimi najua mapenzi ni natural, an inborn attitude, huwezi ambiwa PENDA na wewe UKAPENDA! Kweli sina mapenzi nae, lakini nambieni naanzia wapi kumpenda “baba”? Naendelea kupokea lawama! Unaesoma uzi huu, naomba nasaha zako, hapa mimi nakosea wapi? Pia zingatia kuwa mimi ni mwanadamu, kama ambavyo yeye pia! Siwezi kuvaa viatu vya kulipiza, ila haya ni maisha yangu na yeye ana maisha yake!
Nenda kamuone na umwambie ushenzi wake ayubu ili Hata akienda mbele ya haki Mungu amsamehe
 
Pole sana kwa yote.
Ni ngumu lakini nakuomba umsaidie tu kwa kadri ya uwezo wako tena nenda hata ukamtembelee..kwa moyo safi tu.Mungu aliyekupigania mpaka ukafika hapo ulipo,atakubariki zaidi na zaidi.
Hongera kwa mkeo na Mungu azilaze roho za mama na kaka yako pema peponi.
Na zaidi akutie nguvu
 
slim5 are serious hii ni issue iliyokutokea au story tu? kama ni kweli pole kwa yaliyokukuta aiseeee

Sista hii ni story ya kweli, inanihusu kabisa! ktk vitu ambavo bado naumia, ni hata sitaki kuskia watoto wng watumie surname ambayo mimi naitumia, nataka ukoo wao uanzie kwangu tu!
 
Pole kwa mapito hayo.
Kibinaadamu ungetamani mama angekuwepo sasa kufaidi matunda ya malezi yake lakini jua Mungu ana makusudi yake.
Mhudumie baba yako kadri utakavyoweza hasa katika kipindi hiki cha ugonjwa.
Timiza wajibu wako kama mtoto,kwa aliyowafanyia ni ngumu ila inawezekana.
Mwisho wa siku ndio mzazi wako pekee aliyebaki.

Ennie umeingia ktk moyo wangu! Napata tabu sana ku-define huu msamiati "Mzazi"
 
Nahisi wewe akili zako hazipo sawa,na hujasoma stori yote ukaelewa pia hujawahi pitia tabu hata kidogo kwenye maisha ndo maana unakurupuka kumshambulia.Jichunguze nahis utagundua umeandika pumba na mashudu hapa.

Sijajisifu kwa mafanikio Bupe, sina uwezo kivile, sio tajiri, ni muajiriwa wa serikali, wa kada ya kawaida sana! nimejaribu kuwaonyesha walimwengu namna gn maisha ya duniani yalivo, na mungu alivo na mipango yake! Namsaidia lkn sifurahishwi na shinikizo nnazopata kutoka kwa ndg na jamaa zake tena wngne hata kunijua hawanijui, eti sijajitolea vya kutosha! Inawezekana nina roho mbaya, sawa lakini yeye ana mchango ktk roho mbaya yangu!
 
Back
Top Bottom