Wapi mmeanza kuisoma namba? Toa ushuhuda hapa

Wapi mmeanza kuisoma namba? Toa ushuhuda hapa

TAWA

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Posts
3,674
Reaction score
1,572
Katika baadhi ya maeneo tayari watu wameendelea kuonja joto ya jiwe kwa maisha magumu.
Mfano ni huko Katoro Geita ambako mauaji ya kinyama yametokea yakihusisha watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa CCM.

Huko ndo kuisoma namba
Polisi kupiga wanafunzi wanaoandamana kudai chakula shuleni na mazingira bora (siyo kuvuta bangi).

Huko ndo kuisoma namba
Maji hakuna Handeni imewalazimu wakazi kutumia maji yenye kinyesi cha binadamu na wengine kuonekana kuchimba chini pembezoni mwa bwawa kupata maji safi.

Huko ndo kuisoma namba
Ongeza ya huko eneo unakoishi
 
Jwetu wameshatangaza kuandikisha mwanafunzi darasa la kwanza elfu kumi na tano.

Kuna madarasa na madawati lakini? Hongereni...Hapakazi tu! TUMUUNGE MAGUFULI MKONO KTK KULETA MABADILIKO!!!
 
Bawacha nchi nzima dhidi ya mgao wa viti maalum, 56% ya viti wamepewa "Ahlul bayt".
 
Jana 16/11/2015 wakazi wa kurasini wameanza kuisoma namba. Nyumba zaidi ya 100 zimebomolewa kupisha uwekezaji wa bandari kavu.
 
Jana 16/11/2015 wakazi wa kurasini wameanza kuisoma namba. Nyumba zaidi ya 100 zimebomolewa kupisha uwekezaji wa bandari kavu.

Huku morogoro vijijini tayari wanaiomba serikali chakula cha njaa
 
Yanayoendelea bungeni muda huu pia tumeanza kuisoma namba
 
Nipo hapa Igunga kikazi nitakaa kwa muda wa miezi 3 lakini Tangu uchaguzi uishe na Magufuli kuapishwa kila siku umeme unakatika zaidi ya masaa 12 na kwa jinsi ninavyowaona wananchi wa hapa wanaCCM wengi waliokuwa wakiishabikia CCM wanaisoma namba wenyewe kwani kwa wapinzani waliyatarajia haya kama CCM ingeshinda hivyo wanaCCM ndio wanaisoma namba kwa kuwa walichokitarajia sio wakipatacho kwa sasa.
 
Kuisoma namba ipo cku zote, kibaya zaidi kuna sehemu wanaishi kwa taabu hadi kuona shida ni sehemu ya maisha yao hivyo hawawezi ng'amua kuwa kuna shida, cha muhimu ni kuwaombea waendelee kuizoea shida hivyohivyo kwani hawana namna nyingine.
Mfano kuna sehemu watu hawapati huduma za kijamii na hilo wanalijua na kulilalamikia ila kipindi cha uchaguzi wanarudisha mtu yuleyule alioshindwa kutatua shida inayowasibu.
 
Mm nadhani tusiwalaumu sana wananchi maamuzi waliyafanya yakapokwa,hapa cha kulaumu ni ukimya wetu watanzania tunawekewa watu tusiowataka hata tukitumia democrasia.
 
Kuisoma namba ipo cku zote, kibaya zaidi kuna sehemu wanaishi kwa taabu hadi kuona shida ni sehemu ya maisha yao hivyo hawawezi ng'amua kuwa kuna shida, cha muhimu ni kuwaombea waendelee kuizoea shida hivyohivyo kwani hawana namna nyingine.
Mfano kuna sehemu watu hawapati huduma za kijamii na hilo wanalijua na kulilalamikia ila kipindi cha uchaguzi wanarudisha mtu yuleyule alioshindwa kutatua shida inayowasibu.

Mkuu yaani tuwaombee njaa ili waizoee shida hahaha hili dua mbaya sana kwa Magamba.

swissme
 
Back
Top Bottom