Wapi kuna hii huduma ya Money Transfer?

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,635
29,509
Wadau Kwema??

Nina shida moja, nahitaji ku-transfer kiasi fulani (Arround Tshs 50,000 - Tshs 200,000) nje ya nchi ili huyo atakaepokea anitumie mzigo fulani hivi online. Shida ni kwamba Supplier wengi ni feki (matapeli) na tunatafutana online na kukubaliana bei online, zaidi ya hapo hatujuani.

Sasa kuna Benki au Kamapuni yoyote ya Kifedha inayoweza kufanya huduma ya Money Transfer kisha ikazi-hold kwanza hizo hela until pande zote za mtumaji na mtumiwaji tukubaliane na tuithibitishie benki kua tumekubaliana ndio waziachie kwa upande wa receiver??
 
Utamtumiaje mtu hela humujuia na yeye hakujui.

Kama yupo mbagala wewe upo ubungo utajuwaje?
 
Ebay/Paypal kuna baadhi ya nchi wanatoa huduma hiyo. Ila kwa kutuma kutokea Tanzania hakuna.

Huyo online supplier hana wakala Tanzania?

Kama unanunua kutoka UK fanya njia hii.

Kuna watu huwa wanatuma cargo weekly kuja Tanzania mfano Chris Lukosi. Ongea nao uwaambie kama unanunua kitu kutoka Ebay/Amazon/Dr Jay etc. Wao watakupa address ambayo utaitumia kama delivery address. Kwa njia hiyo utakuwa covered mzigo usipomfikia Chris Lukosi pesa yako urarudishishiwa. Halafu kina Lukosi watakutumia kuja Tanzania.

Kingine Always nunua bidhaa kwenye website zenye Insurance kama Ebay, Amazon , Carphonewarehouse, Currys PC World. Pia linganisha bei kwenye website mbali mbali.

Kumbuka nafuu ni ghali.
 
Kama bidhaa inauzwa online Jisajili Paypal hao watachukua hela kutoka kwako supplier akituma mzigo ndio wanampatia hela.

Muulize muuzaji wako kama amejisajili Paypal kama bado mpe masharti awe member wa paypal ndio mfanye biashara.
 
Benki zinafanya hivyo lakini zinafanya kwa transaction kubwa kubwa. Inaitwa Letter of credit... Yani benki inamlipa mteja pale atakapoonesha document za kuonesha kuwa mzigo umekabidhiwa kwa carrier/ meli au ndege.
Cha kufanya, mwambie huyou mtu akupe account number yenye jina lake halisi. Then wawe utaenda kumuingizia fedha benki. Utajaza taarifa za mpokeaji ikiwa ni pamoja na akaunti namba alafu benki itafanya TT.
Huyo mtu kama ni tapeli, ukimwambia hii option atakataa. Ila akikubali ujue sio tapeli.
 
Kama bidhaa inauzwa online Jisajili Paypal hao watachukua hela kutoka kwako supplier akituma mzigo ndio wanampatia hela.

Muulize muuzaji wako kama amejisajili Paypal kama bado mpe masharti awe member wa paypal ndio mfanye biashara.
Mdau mpita-njia pale juu kasema hii huduma ya Paypal haipo hapa Tanzania
 
Atasema vipi huduma haipo wakati Paypal ni online worldwide!
Muuzaji wako akupatie account yake ya paypal. Wewe jisajili na paypal online kufuatilia transaction yako
 
Kwa kifupi muuzaji atakupatia bank account mbili moja yake moja ya paypal.
Kama bidhaa inauzwa Tsh 200,000 kwenye account yake utalipa hiyo hiyo 200,000 kama utalipia kupitia paypal utalipa 220,000 . Elfu 20 ikiwa kama gharama za paypal.

Sasa ukiwa unatuma kutoka kwenye account yako bank hawatakiwi kujua ni account ya paypal au la . Wewe utajaza account # kichwani kwako ndio utajua kiwa ni ya paypal
 
Sasa kuna Benki au Kamapuni yoyote ya Kifedha inayoweza kufanya huduma ya Money Transfer kisha ikazi-hold kwanza hizo hela until pande zote za mtumaji na mtumiwaji tukubaliane na tuithibitishie benki kua tumekubaliana ndio waziachie kwa upande wa receiver??
Sasa kuna Benki.........inayoweza kufanya huduma ya Money Transfer kisha ikazi-hold
- Hakuna, ukituma direct kwenye account yake kwa njia ya benki anapokea fedha moja kwa moja.
- Haishauriwi kutuma fedha kwa njia hizi
1. Bank transfer
2. Western union
3. Moneygram
Kwa mtu ambaye hamfahamiani na haujawai fanya naye biashara awali.
ikazi-hold kwanza hizo hela until pande zote za mtumaji na mtumiwaji tukubaliane na tuithibitishie
Njia ya salama ni kutumia
- Paypal
- Alipay
Ambapo wewe ukisha athibitisha kupokea mzigo ndio seller anapewa fedha yake.

Je nini cha kufanya?
- Wasiliana na huyo jamaa, mwambie njia pekee ya kumlipa ni kwa paypal.
- Iwapo atakataa, Basi angalia utaratibu mwingine

KARIBU www.bit.ly/101buy4me
 
Kwa kifupi muuzaji atakupatia bank account mbili moja yake moja ya paypal.
Kama bidhaa inauzwa Tsh 200,000 kwenye account yake utalipa hiyo hiyo 200,000 kama utalipia kupitia paypal utalipa 220,000 . Elfu 20 ikiwa kama gharama za paypal.

Sasa ukiwa unatuma kutoka kwenye account yako bank hawatakiwi kujua ni account ya paypal au la . Wewe utajaza account # kichwani kwako ndio utajua kiwa ni ya paypal
Poa poa kaka, ahsante sana
 
Back
Top Bottom