Mada maalum kwa wapenzi wa Tamthilia ya Isidingo

Future gabriel
26733753_1714553885250256_5232191360737156720_n.jpg
 
Tuesday

Lerato analia huku akiwa na hofu,sechaba anagundua kosa lake na kumwaomba msamaha huku akisema hafahamu kinachoendelea juu yake. Lerato anamtaka akapumzike maana dokta kasema hivyo na kwamba wale jamaa lazima walipe atake asitake

Majola anaenda ofisin kwa eddie kuulizia maendeleo ya kesi ya nina na kuambiwa kanyimwa dhamana na anapigania hilo ,majola anauliza kama kuna uwezekano akawa na hatia eddie anasema ni kwa asilimia chache maana mashahidi wanadanganya kumlinda nina. Majola anatoa wazo la kutumia mbinu nyingine ila eddie anakataa. Majola anambembeleza eddie ,eddie anamwambia ampe muda afikirie

Shebeen morogwa anamtaka matlala alipoe vinywaji vyake na kwamba ofa ya bure imeisha,matlala anamwambia hizo ni hasira sababu ya kushindwa na wendy kisha anamwambia akimuona huyo binti atampa mkono wa pongezi

Nikiwe akiwa kwenye huzun sababu ya jaribio la linc,gabr anataka kutumia nafasi hio kuwastopisha kgotha na rajesh kwenda kula msosi wa usiku penthouse. Nikiwe anakataa wazo hilo. Gabr anasema atapika msosi huo. Nikiwe anasema afadhali kabakiwa na hofu moja ya kuonana na eddie ambae atamhoji ikiwezekana na gabr pia atahojiwa. Gabr anashtuka kuwa na yeye atahojiwa na kuwa na wasi wasi

Asubuh sechaba anaweka vitu vyake vya kazi kwenye begi ila lerato anamwambia asiende kazin huku akimuuliza anaendeleaje,sechaba anamwambia dawa hazimpunguzii maumivu pia ana wasi na sikio lake maana ana maumivu na pia anahisi hataweza kusikia tena. Matlala anagonga mlango lerato anamfungulia,matlala anaenda ongea na sechaba akimwambia kuwa wale jamaa lazima walipe walichokifanya na kwamba wakiwaacha watarudia tena huku akisema watawatafuta popote walipo. Sechaba anaona sio mbinu nzuri pia sechaba anasema hawez enda onana na watu akiwa katika hali hio. Matlala anamwambia asijali yeye atasimamia kila kitu


Kgotha na rajesh wapo ofisin kwa rajesh wakiongelea masuala ya kazi kisha kgotha anamshukuru rajesh kwa kuwa nae katika kipind kigumu alichopitia. Kgotha anaaga kuondoja,rajesh anasimama toka alipokua amekaa. Kgotha anaondoka kisha anarudi,rajesh anauliza kama alisahau kitu kgotha anjibu ndio na kumcata rajesh na kumkiss kwenye lips,kisha anasema alisahau hicho na kuondoka

Wendy(mdada wa kizungu)anaenda salun kwa lerato na kuulizia kuoshwa kwa shampuu bei gani,lerato anamtajia bei,wendy anaangalia pesa kwenye begi lake na kukosa na kumwambia lerato kuwa kasahu wallet yake huku akiondoka,lerato anapanic na kumuuliza kama katumwa au yeye ni dada wa wale walimomvamia sechaba.wendy anasema hajui anachoongea na kwamba yeye ni mgen mjin hapo. Lerato anamwomba msamaha na kumwelezea kidogo kilichomtokea sechaba. Wendy anabadili topic na kuomba ajira akisema yeye ni mtaalamu wa kucha,lerato anamwambia hakuna nafasi kisha anamtaka aandike namba yake ikipatikana nafasi watamtafuta

Eddie anaenda ofisin kwa nikiwe kumhoji ila nikiwe anasema hajui chochote na kwamba eddie anatakiwa akamhoji nina na aulize alizipataje shares za sibeko toka kwa linc

Shebeen matlala anawaambia waliopo humo kuhusu sechaba kufukiwa na sikio moja kuzuba huku akiwataka wawatafute waliomtendea jambo hilo. Anaingia mbaab aliyemuokoa sechaba,anafuta kiti cha kukalia kwa kitambaa chake,analetewa bia na glass,anaifuta glass kwa hicho kitambaa,anapinga wazo la matlala na kuwataka wawaachie suala hilo polisi ila matlala anagomea wazo hilo.

Eddie anaenda selo ya nina na kumhoji kuhusu shares za sibeko,nina anasema kazinunua kwa pesa zake.eddie anamtaka aonyeshe ushahidi,nina anasema alinunua kwa cash. Eddie anasema hamuamin

Wendy anaenda shebeen na kumwomba msamaha morogwa kwa vurugu aliyomfanyia huku akimwambia asimshtaki polisi,morogwa anamuuliza kwann anaogopa polisi. Wendy anamwambia ktoka gerezan muda si mrefu hatak kurud tena huko

Matlala na kikund chake wanaingia kanisani wakiimba nyimbo za kuhamasisha huku wameshika mapanga. Matlala anawatuliza na kuanza sema sechaba alipigwa kwenye ardhi yake. Morogwa anasema sechaba kaipatia wapi ardhi,yeye ni kama wao hana ardhi. Mbaba anajibu sechaba ana ardhi na kwamba ben aliirudisha ardhi kwa familia ya sechaba. Matlala anasema waende wakawafate huko huko ila mbaba wa kanisan anawataka wasali,matlala anamjibu waende wote huko. Matlala na kundi lake hawataki ushaur wanaondoka

Gabr na nikiwe wanawasubiria rajesh na kgotha,rajesh na kgotha wanaingia. Rajesh anampa nikiwe maua. Kgotha anamkabidh gabr wine ila gabr anakwepa kuipokea na kwenda kukaa kwenye kiti cha linc dinning hapo. Rajesh anamvutia kiti kgotha.Nikiwe anamwangalia gabr kisha anajivutia kiti. Nikiwe anasema ana njaa na kutaka kupakua ila gabr anakataa na kusema wasali kwanza kwa kushikana mikono kisha nikiwe atoe sala,kgotha anashangaa na kitopendezwa na jambo hilo. Nikiwe anasali

Usiku Matlala na kikund chake wakiwa wameshika miti yenye moto kwa juu wanaimba huku wakienda nyumba moja ya geti na kuruka ruka hapo wakiimba
 
Kuwa mpole
mmoja wa ma mod ni jirani yangu hapa kitaani. Nitampa acc yako akufanyie online screen kabla hajakuunganisha na hilo jukwaa la wakubwa.
Dreka vipi Mkuu. Mm pia nilikutumia kama ulivyoagiza. Nategemea jibu kwako mkuu.
 
Dreka hamishia basi PM haya mambo ya jukwaa la wakubwa sio mahala pake hapa.

Leo wanakwambia hawa kesho watakuja wengine pia kukuomba uwaunge huko,mwisho wa siku haitakua isidingo thread bali uzi wa kuomba kuunganishwa jukwaa la wakubwa,i know u r enjoying teasing them ila sio fresh ujue.
 
Wapenzi wa isidingo mmaweza burudika hapa..
 

Attachments

  • Pasi%C3%B3n_y_Poder___Nina_y_Eladio_se_besan.mp4
    11.2 MB · Views: 30
Wednesday

Wale jamaa waliompiga sechaba wameenda duncan na kupata chumba. Barker anawaona ila hakuwatambua. Jamaa mmoja wapo anapata wasiwasi na kumuuliza mwwnzie kama barker hajawatambua maana habar zitakua zimeenea,mwenzie anamtoa wasiwasi na kuelekea vyumban,mhudumu anatoa simu na kupiga namba flan

Skhu kaenda kuchukua vitu vyake kwa sechaba na kumuaga wanaishia kunywa kama ishara ya kuagana

Majola kaenda selo kwa nina kumhoji na kumtishia ataenda mhoji askar mthomben ili aeleze ukweli. Nina anasema kuwa linc alimtishia

Rajesh na kgotha wanatoka mazoez ya tenis na kuingia duncan wakiagiza maji,kgotha anamuuliza rajesh ratiba zake kisha anamtaka muda akiwa free aende rum kwake,nikiwe anatokea akitoka mazoez ya kukimbia na gabr. Baada ya nikiwe na gabr kuondoka kgotha anaonyesha hajapenda tabia ya gabr kumlinda sana nikiwe

Majola anamkuta mthomben shebeen na kumhoji kuhusu mpango wa linc kutoroka na kama nina alimtishia ila mthomben anasema linc ndo alihusika na aliwatishia maisha kama hawatamsaidia

Eddie anamuuliza rajesh kuhusu nikiwe kuhusika na mpango wa linc kutoroka ila rajesh anamjibu nikiwe hawez fanya hivyo

Morogwa anaenda salon kwa lerato na kumuuliza kama anafahamu kilichotokea kwenye shamba walilovamia,lerato anasema kasikia ila haungi mkono wazo hilo na kwamba watu wanakamatwa kwa uharibifu huo.wakiwa katika maongez lerato anamwambia morogwa kuwa anakaribia muajili msichana aitwae wendy ,morogwa anataman kumwambia kitu lerato kuhusu wendy ila anasita

Rajesh yupo rum kwa kgotha wakipata kinywaj,rajesh anasema anakumbukia kiss aliyopewa jana ake

Matlala yupo na wenzie shebeen wakiongelea walichokifanya jana yake huku wakisema polis hawez wakamata wote waliofanya uharibufu huko,sechaba anatokea hapo na kumuuliza matlala kama ni wao walioharibu mali za watu,matlala anakubali,mara anapigiwa simu na kwenda kuongea pemben. Anapishana na nina anaueingia shebeen,morogwa anamsifia nina kwa alichokifanya ila nina anasema alitishiwa na linc,morogwa haamin story ya nina,matlala anarudi na kuwaambia wenzie kuwa wale watu wao wapo duncan. Sechaba anawaambia yeye hataweza kwenda nao ila anawaunga mkono wakifanyacho,matlala nasema wao wataenda kisha wote wanaondoka

Lerato anaingia salun kwake kachelewa na kumkuta wendy kampaka vizur mteja rangi ya kucha,lerato anamuita pemben na kumuuliza anafanya nn hapo,wendy anasema alikuja kwenye interview akakuta kuna mteja anasubiria kupakwa rangi,lerato anamtaka wendy akamalizie kazi aliyoianza

Nikiwe yupo duncan anaongea na jamaa mmoja ila anakatizwa na kelele za akina matlala na kuamua kuondoka,barker anasikia kelele hizo pamoja na wale jamaa wa kizungu. Matlala na wenzie wanaingia wakiwa na silaha za jadi,wanafika mapokez na kuulizia walipo wale wabaguzi waliompiga sechaba na kusema waletewe huku wakiendelea kuimba nyimbo zao. Jamaa mmoja anawachukua video kwa simu,matlala anaipiga simu akimgombeza hio sio movie. Brad anatokea na kuuliza kulikon,matlala anamtaka awaletee wale wabaguzi. Walinz wa duncan wanatokea,brad anawaambia akina matlala waondoke wao watashughulikia swala hilo. Matlala na wenzie wanabisha na kusema hawaondoki,brad anasema hawez watoa hapo wateja wake. Matlala anasema hawaondoki watalala hapo na kuendelea kuimba,brad aanwaambia walinz walinde ngaz za kuingilia vyumban
 
Back
Top Bottom