Mada maalum kwa wapenzi wa Tamthilia ya Isidingo

Angie yupo sana. Angalia epsode ile ambayo Gabri atakuwa mahabusu. Atabadilisha nywele kuwa some how black lakini yupo sana. Ila Linc nahisi ndo mwisho wake. Hii attempt itampoteza. Kama kawa Nina ashaanza kumpamba Maloi na atamtoa tu.
So Linc atauliwa ama vp?
 
Thursday

Lerato anaongea kwa simu na matlala akiulizia kama amepata taarifa za sechaba,matlala anajibu hajapata. Lerato full huzuni

Wale wazungu wamemalizia kumfukia sechaba na kuondoka eneo la tukio. Jamaa mmoja anapita eneo alipofukiwa sechaba akitafuta miti shamba anasikia sauti na kuifatilia

Lerato akiwa home anaangalia nguo za sechaba huku akiomba arudi nyumban

Mdada aliyetoka jela anaamka eneo alilokua amelala huku kakaa kwenye kiti

Jamaa kawaita wenzie na kuanza kufukua eneo alilofukiwa sechaba

Lerato akiwa home mpweke anamuomba Mwenyezi Mungu amlinde sechaba alipo

Mdada mjela anafungua begi lake na kutoa notebook yenye namba za simu anaangalia na kuirudisha kwenye begi

Wakazi wakiendelea kumfukua sechaba akiwemo matlala anaewataka wawahi kumfukua na pia wasimuumize. Anawataka watumie mikono na wawe makini

Home lerato ana huzuni huku kakumbatia shati la sechaba

Mjela anainuka alipokaa na kuiba nguo zilizokua zimeanikwa kamban

Gabr anamakaratasi kama sticker,mhudumu anatenga msosi mezan,gabr anamgombeza,nikiwe anatokea na kumwambia mfanyakazi aende jikon. Gabr anamwambia nikiwe kuwa anataka kuibadilisha the rec. Nikiwe hafurahishwi na mpango huo

Gerezan,gabr anaenda mtembelea nina,nina anamtaka amtoe kwa dhamana kisha atamlipa. Gabr anakataa kujihusisha na mambo hayo anahisi nae ataunganishwa humo. Nina anamuuliza kama nikiwe anafahamu kuwa linc alitaka kutoroka gerezan. Gabr anasema mabosi wa gereza wanaficha maana itawasababishia aibu. Nina anauliza siri hio itakaa kwa muda gan. Nina anatumia nafasi hio kumtishia gabr kuwa siri ikifichuka nae ataumbuka na kuuza sura gazetin hivyo atafute pesa amtoe huko gerezan

Lerato akiongea kwa simu na mama yake akimweleza kuhusu kupotea kwa sechaba huku akianua nguo anagundua kuna nguo zimepotea na kushangaa

Kgotha akiwa anamalizia kuvaa viatu rajesh anatokea akiwa na suti yake ya kuvaa kwenye opera,rajesh anauliza kama na nikiwe atakuwepo kwwnye safar ,kgotha anakubali mara nikiwe anapiga simu na kusema gar lake limeharibika,kgotha anamwambia watamfata ili waemde pamoja,gabr hafurahii kusikia nikiwe atafatwa na akina kgotha na kumwambia angejua gar kuharibika ni ishara mbaya,nikiwe anakubaliana nae na kusema atamtumia kgotha sms kumjulisha hataenda nao

Morogwa akihudumia wateja,anamfata mdada aliyetoka jela mezan na kumuuliza atahitaji kinywaj gan ila mdada anamjibu haitaji kinywa huku akiinuka na kusema alikua anaangalia palivyo. Morogwa anamuuliza kama ni mpelelezi au polis. Mdada anatoa pete akisema anataka kuiuza ni gold,morogwa anamtaka aende duncan,mjela anajitambulisha kwa jina la wwndy huku akimshawishi morogwa kuhusu pete aliyonayo. Morogwa anakubaliana na bei akitaja pesa na bia na kuipata pete

Kgotha na rajesh wanaenda penthouse kumpitia nikiwe,nikiwe anauliza kama sms yake haikuwafikia. Kgotha anasema aliipata na kuipuuzia maana sababu haina mashiko. Gabr anasema nikiwe haendi,wao waende wakainjoi. Kgotha anafanikiwa kumshawishi nikiwe,nikiwe anaenda kujiandaa waondoke,rajwsh anasema hawez kwenda kapata muito muhimu,kgotha anamkubalia,rajesh anaondoka. Kgotha anamshushua gabr kwa mchezo aliocheza kisingizio gar

Linc yupo selo askar wa kiume anamsimamia,linc anampa kitu na kumtaka akampe nina,askar anakataa,linc anamtishia atawaambia polisi kuwa alimsaidia kutoroka,askar anakubali na kuweka mfukon

Lerato anaongea na simu hukh kapanic kwa swchaba kupotea,mara jamaa wanampeleka sechaba humo salun,lerato aanulizia kilichotokea,jamaa wanamwambia walimkuta kazikwa huko alipokwenda

Eddie anampeleka nina selo akimwambia ndo nyumba yake mpya hio. Nina anamlaumu eddie kwa kusababisha akanyimwa dhamana. Eddie anaondoka,anatokea askar na kumkabidhi nina kitu,nina anaangalia na kukuta ni simu linc kapicha video call na kumpa ofa ya kumtoa nje ikiwa atamfanyia kitu kimoja

Gabr yupo penthouse,nikiwe anaingia na kumuuliza kamuitia nini na kwamba alikua tayari keshafika Johannesburg. Gabr anamwambia akae na amsikilize yeye badala ya wadaku. Gabr anamwambia kuwa nina yupo jela sababu alikua anamtorosha linc jela.pia anamwambia lic karudishwa jela na nina kanyimwa dhamana. Nikiwe anasema anaenda jela kumuuliza linc sababu ya kufanya hivyo ila gabr anamkataza na kumwambia bwana jela wanafanya siri tukio hilo. Nikiwe anamlaumu linc

Sechaba anavua nguo huku akisikilizia maumivu makali na kwenda bafuni kuoga
 
Back
Top Bottom