Wapenzi wa Paka

Nikiona paka na mbwa mwili unasisimka... sivipendi hivi viumbe kabisa...
 
Dah nyau kichuna huyu naona kuna mtu atanipokonya maana keshasema anamtaka haya umposti nyau huyu ndugu yangu umenunua kesi :lol::lol::lol::lol::lol::lol:Kaniganda atampataje!!
 
Dah nyau kichuna huyu naona kuna mtu atanipokonya maana keshasema anamtaka haya umposti nyau huyu ndugu yangu umenunua kesi :lol::lol::lol::lol::lol::lol:Kaniganda atampataje!!

Hahahahh hatolala kwa furaha yake..hebu muoneshe
 

Beautiful kittens n very very cute nilikuwa na mmoja chuoni tangu kakiwa kigoli, balehe uchumba, ndoa hadi watoto,
Wanyama ni kama binadamu kabla hajavunja ungo nilikuwa nalala naye, naenda naye darasani na pengine pote, alipokuja kupata mpenzi wa mtima wake safari nami zikapungua mno, nakumbuka jioni nikimwachia chakula kwenye sahani yake hali mpaka bebi wake aje
Siku anajifungua hakutaka niende popote nilikaa naye mpaka alipopata uchungu na hatimaye kujifungua vitoto vinne vicute hasa

Sitosahau siku naondoka kurudi Tanzania, kuna hisia za ajabu wee acha tu, nilikuwa mzazi kwake na ilibidi nitengane naye nilikuwa nahisi maumivu yake naye alikuwa anahisi ya kwangu

Thanx farkhina
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…