stephot
JF-Expert Member
- Mar 1, 2012
- 17,746
- 27,214
Wadau,
Nimesukumiwa kesi na rafiki yangu wa karibu nikashindwa kuitolea suluhisho ndipo nimeamua niiweke humu jamvini tupeane mawazo. Alinitaarifu kuwa nyumbani kwake moto unawaka ana muda wa mwezi sasa hajapata unyumba kisa yeye binafsi hataki kuoga na mkewe. Anasema toka wameoana yapata miaka mitatu iliopita hawakuwa na huo utaratibu.
Lakini ghafla kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu mkewe anataka wawe wanaoga wote kitu ambacho yeye hakiafiki kabisa, kikubwa ni kuwa hana sababu ya msingi ya kukataa zaidi ya kudai kuwa yeye hajazoea na hataki hilo jambo.
Sasa naombeni wadau mnipe mawazo ambayo yanaweza kumsaidia huyu bwana ili akubaliane na hiyo hoja ya mkewe na hatimaye apewe tena unyumba kwa faida yake mwenyewe. Kwa wale wajuzi wa haya mambo labda ingesaidia pia kama mtatuwekea uzuri na ubaya wa hili jambo kwa wanandoa au wapenzi.