Wapentekoste Ngara wahamia msituni; wangoja kunyakuliwa


Tuko pamoja mkuu. Umesema vyema kabisa, shetani ni mjanja sana na mtu asiye na ROHO wa MUNGU atapotezwa naye (shetani) maana hujigeuza kama Malaika wa nuru na kuwapotosha wengi.
 
Kweli Mganga hajigangi. Wakati wa sakata la Kibwetere huko Uganda mwanzoni mwa 2000 ( nilikuwa Uganda) Tanzania ilitoa ushauri kwa serikali ya Uganda kwamba ni mihumu kupenyeza watu wa Usalama wa Taifa (informers) katika makundi haya ya dini ili ku-monitor situation just in case mambo yanakwenda mrama. Je Usalama wa Taifa uko wapi katika hili la Ngara mpaka watoto hawaendi shule? Come on TIS.
 
Tatizo watu hawataki kujifunza Biblia, wanategemea waalimu wa dini ambao nao pia wameathiriwa na mapokeo ya kidini tuliyoletewa na wazungu ambayo tayari ilishachanganywa na mafundisho ya kipani Source yake Bibiloni la kale. Miracles are no longer existing!!!
 
Kama huyo mama ameweza kuwashawishi wanakijiji wa idadi hiyo kuhamia kijijini, sembuse uongo na ahadi za wanasiasa kwa waTanzania?
Ndio maana hii nchi haitapiga hatua mpaka watu kama hawa (si lazima kama hawa ki imani) waelimike......ubaya ni kwamba hata hiyo elimu yenyewe hawaitaki.
 
Mungu ushaongea naye wapi wewe mama? Si useme tu frustration za maisha under Kikwete zimekuzidi unatafuta escapism tu, si ajabu ukawa-Kibwetere hawa simpleton peasants.

And then some want to tell me that human beings are rational.

Maisha bora kwa kila Mtanzania hayo.
 
watu wako taabani ....JK anaenda kuwaambia ataugeuza mji wao kaa Dubai. huko Dubai watu hata kupasikia hawajawahi acha kupaona!
 

GOOD POINT, Pia imani potofu au kupotoka kiimani huanza na mtu mmoja. sijaamini kuwa hao ni wapentecoste. Ni kama wale jamaa ambao kambarage aliwatimuwa miaka ya 60 walikuwa wanaitwa watch tower kama sikosei. Lakini pia mtu mmoja hata mtumishi wa Mungu anaweza kupotoka na kubeba kundi kubwa la watu.

kwa hao ikiwa huo ni mpango wa Mungu na wameongozwa na roho wataendelea la si hivyo watasambaratika!
 
Dogo nilijua tu utasema. Madrasa si ni yetu wote sasa hasira za nini? Kwa kukosa utetezi wa kupigwa mboko madrasa nimesema sijali kama wanataka kukaa huko wakae tu. Ni haki yao maana wako above 18 wanamaamuzi ya kiutu uzima.:becky:
 
tanzania maendeleo yatachukua muda kupatikana kwa vitu kama hivi. kwa kuwa wamekakosolewa wapentikoste lazima waingizwe waislam nao kwenye mjadala.

sheria ni msumeno tu, kama anaevunja ni mwalmu wa madrasa au mwalimu wa sunday school
Yaani kwako kusema nilipigwa viboko madrasa imekuwa issue ya waislam tena? si nilipigwa mboko? Sasa shida ni nini?

Haya bwana ngoja nitoke kwenye mjadala huu maana kuwasema waislam ni dhambi ati.
 
Hao ni wapentecoste masalia?:confused2:
 

.
Hebu tukumbushane kidogo. Pango alilobanwa mbavu Muhamadi kwa mara ya kwanza alipotakiwa kusoma lilikuwa mjini au nyikani?
Hapa litawezapatikana jibu la wenye akili zaidi ni wa wapi.
 
.
Hebu tukumbushane kidogo. Pango alilobanwa mbavu Muhamadi kwa mara ya kwanza alipotakiwa kusoma lilikuwa mjini au nyikani?
Hapa litawezapatikana jibu la wenye akili zaidi ni wa wapi.

You made my day mkuu.
 
mh! nilisoma mahali "WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA"
 
wanatakiwa waonyeshe ni kitabu gani na mistari ipi katika Biblia inayotoa hayo maelekezo!
 
Vijiji vingi ndani ya Tz chini ya serikali ya ccm havina tofauti na maisha ya msiituni. Ni kijiji gani Tz kinaweza kuvuna mazao wakati wa msimu ikiwa Mungu hakuwanyeshea mvua? Hakuna jitihada zozote za serikali kuweka miundo mbinu ya kilimo cha umwagiliaji, na kama zipo basi zitakuwa ni takwimu kwenye makaratasi za miaka nenda rudi. Hivyo wanavijiji hawaoni tofauti ya kuishi kwenye kile kinachoitwa kijiji na msituni.
WAPENTEKOSTE ZIDISHENI MAOMBI YENU, YESU AWACHUE KUPUMZIKA ILA KWA JINSI NINAVYOZIJUA HURUMA ZAKE HATAWACHUKUA NINYI ILA ATAINYAKUA CCM KUWATOA MADARAKANI NA KUWAKABIZI KWA CHAMA KINGINE KITAKACHO SABABISHA UKOMBOZI WENU KIMAISHA.

KIBY - YOU REALLY IS AMUSING - GOD BLESS YOU - ha ha haaaaaaaaaaaaaaaa ha ha haaaaaaaaaaa - hivi kweli CCM itanyakuliwa??? lets wait and see!!!!
 
Wapentekoste Kanisa gani? Makanisa yao yana majina bwana ebo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…