Ng'wanapagi
JF-Expert Member
- Sep 18, 2013
- 9,116
- 8,658
Ndugu zangu habari za weekend.
Tangu nianze kuota ndevu zimekuwa zinaongezeka kila mara. Mwanzoni nilikuwa natumia nyembe za Gillet lakini nikinyoa natokwa na upele unaowasha sana. Baadaye nikaanza kuhudhuria saloon lakini hali ni ileile, baadae nimeanza kutumia magic powder hapo ndo tatizo la upele na muwasho likaisha.
Tatizo kubwa linalonikumba ni kuwa kila baada ya siku tatu ndevu zinakuwa nyingi na zinawasha hadi ninyoe kwa magic ndipo tapata usingizi tofauti na hapo ndugu zangu usingizi hakuna. Kuna kipindi niliambiwa na rafiki zangu nisizinyoe na zitaniwasha mwanzoni lakini itafikia hatua zitaacha na nilitii lakini nilionekana kituko kwa watu walionizoea kwa kuitwa majina mbalimbali japo hata mimi sipendi kufunga ndevu.
Ndugu zangu kwa yoyote anaweza kunisaidia naomba anipe msaada wa vitu vya kutumia aidha kupunguza wingi wa ndevu zinazoota au muwasho pindi zinapoanza kuota kwani sawa hivi sasa nina uwezo wa kutumia hivyo bidhaa (magic powder,Eskinol,After shave) lakini naamini maisha huwa yanachenji na ukajikuta hata wembe huwezi nunua. Nisaidieni waungwana.