Wapangaji wenzangu, mnakabiliana vipi na jirani asiyetaka kulipia bili ya maji na umeme?

Mawele

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
354
Reaction score
1,038
1772602902874.png

Maisha haya! Hii dunia ina mambo sana, hivi wapangaji wenzangu mnakabiliana vipi na mpangaji mwenzako asiyetaka kulipia maji na umeme jamani na mnatumia wote?

Huyu jirani yangu kanishinda tabia walahi, angekuwa bidhaa ningemgawa bure kabisa maana hafai msikitini wala kanisani, hafai kwa mchuzi wala kuchomelea, kha, mtu gani kila bili ana sababu mpya jamani mwaka mzima halipi maji, umeme kaweka 5000 mwaka unaisha!

Jirani yangu ana mwaka hapa alihamia akanikuta, tangu kaja hajawahi lipa maji hata siku moja, yeye kila bili ana sababu ni magomvi tu jamani mpaka nachoka kupigizana naye kelele maana tupo wawili tu ila halipi, mtaishia kugombana tu na bili halipi na kutumia anatumia tena akianza kufua nguo moja anasuuza na ndoo moja ya maji.

Yeye hana mtoto anaishi peke yake ila ana wageni wa kke kila baada ya masaa mawili anakuja mtu na huyo mgeni wake ataoga na kama ni kufua atafua, nafahamu kwa sababu yeye hana choo cha ndani anatumia cha nje hivyo naona maana kipo usawa wa dirisha langu.

Mie nina familia ya watu 5, ila mara nyingi tupo 3, kiustarabu nilimwambia umeme aweke wa 10000 na mie wa 20000 kwa sababu mie nina friji yeye hana ila vingine vyote tuko navyo sawa vinavyotumia umeme akajibu sawa.

Akanunua umeme wa 5000 akasema ataweka 5000 tena ukiisha umeme haujawekwa wala kununuliwa tena nikimwambia anajibu yeye hana matumizi ya 10000 kwa mwezi sababu hana watoto matumizi yake ni madogo sana, mie ndio nitakuwa namaliza umeme hivyo hanunui na saa ni mwaka umepita tangu aweke 5000.

Maji nayo anadai watoto wangu ndio watakuwa wanamaliza maji yeye hana matumizi ya maji hivyo halipi bili, kifupi ni mkorofi kuliko kawaida mpare huyu.

Yaani hana aibu hata kidogo anatumia na halipi na sio shida zake kha, juzi ndio kanitolea kali ya mwaka, anasema hawezi lipa bili ya maji na huku yeye hana bomba la maji ndani kama mimi, kwa nini mie niwe na maji ndani yeye hana hivyo halipi bili!

Soma:Nimechoka kufungiwa MITA ya maji na jirani yangu
 
Ongea na mwenye nyumba aweke sub meters ili kila mtu ajue matumizi yake na awe responsible kwa anachotumia.

Dunia ya sasa unalipia unachotumia, hakuna kunyonyana.

Kama mwenye nyumba nae anaitikadi za kizamani hapo umeumia, tafuta sehemu nyingine uhamie, after all nyumba yako ipo mfukoni.
 
Changamoto ni kwamba mpangaji mwenzake hataki kulipa, unaweza kufunga sub meter akawa anaona umeme anaoutumia lakini kama ni mtata kulipa maana ake umeme ukiisha, atawalaza wenzake giza, kwa mantiki hiyo sub-meter sio suluhisho
Kwanza mpangaji kama huyo hata huo mchango wa kununua sub-meter hatachanga
 
Mpangaji kasema hatumii maji, hana matumizi makubwa ya umeme, maana yake anatakiwa kuonyeshwa kwamba nae ana matumizi tena kwa takwimu. Nimesikia(sina uhakika) kuna sub meters zinaweza kukata ikiwa mtu hajalipa, hizo ndio suluhisho

Yakishindikana anahama tu, nyumba yake ipo mfukoni mkuu.
 
Ndio zipo! Mpangaji ananunua umeme mnajaza ukiisha wake inazimika chap!
 
Maisha haya! Hii dunia ina mambo sana, hivi wapangaji wenzangu mnakabiliana vipi na mpangaji mwenzako asiyetaka kulipia maji na umeme jamani na mnatumia wote?

Huyu jirani yangu kanishinda tabia walahi, angekuwa bidhaa ningemgawa bure kabisa maana hafai msikitini wala kanisani, hafai kwa mchuzi wala kuchomelea, kha, mtu gani kila bili ana sababu mpya jamani mwaka mzima halipi maji, umeme kaweka 5000 mwaka unaisha!

Jirani yangu ana mwaka hapa alihamia akanikuta, tangu kaja hajawahi lipa maji hata siku moja, yeye kila bili ana sababu ni magomvi tu jamani mpaka nachoka kupigizana naye kelele maana tupo wawili tu ila halipi, mtaishia kugombana tu na bili halipi na kutumia anatumia tena akianza kufua nguo moja anasuuza na ndoo moja ya maji.

Yeye hana mtoto anaishi peke yake ila ana wageni wa kke kila baada ya masaa mawili anakuja mtu na huyo mgeni wake ataoga na kama ni kufua atafua, nafahamu kwa sababu yeye hana choo cha ndani anatumia cha nje hivyo naona maana kipo usawa wa dirisha langu.

Mie nina familia ya watu 5, ila mara nyingi tupo 3, kiustarabu nilimwambia umeme aweke wa 10000 na mie wa 20000 kwa sababu mie nina friji yeye hana ila vingine vyote tuko navyo sawa vinavyotumia umeme akajibu sawa.

Akanunua umeme wa 5000 akasema ataweka 5000 tena ukiisha umeme haujawekwa wala kununuliwa tena nikimwambia anajibu yeye hana matumizi ya 10000 kwa mwezi sababu hana watoto matumizi yake ni madogo sana, mie ndio nitakuwa namaliza umeme hivyo hanunui na saa ni mwaka umepita tangu aweke 5000.

Maji nayo anadai watoto wangu ndio watakuwa wanamaliza maji yeye hana matumizi ya maji hivyo halipi bili, kifupi ni mkorofi kuliko kawaida mpare huyu.

Yaani hana aibu hata kidogo anatumia na halipi na sio shida zake kha, juzi ndio kanitolea kali ya mwaka, anasema hawezi lipa bili ya maji na huku yeye hana bomba la maji ndani kama mimi, kwa nini mie niwe na maji ndani yeye hana hivyo halipi bili!

Soma:Nimechoka kufungiwa MITA ya maji na jirani yangu
Hii ni changamoto, hata kama ni Mimi kwa matumizi basic ya ndani umeme wa 10k ni mkubwa mno. Funga Mita nyingine au hama unapokaa uende mahali kunapo eleweka.

Nyumba nyingi za kupanga Zina changamoto sana.
 
Sema ukiwa na kipato,ni vyema ukapanga kwenye nyumba za aina fulani..ni zile nyumba zinazo jitegemea unaishi peke ako...ama kwenye hizi apartment za kisasa..ni nadra sana kuishi na watu wa hovyo hovyo kwenye hizo nyumba
 
Hii ni changamoto, hata kama ni Mimi kwa matumizi basic ya ndani umeme wa 10k ni mkubwa mno. Funga Mita nyingine au hama unapokaa uende mahali kunapo eleweka.

Nyumba nyingi za kupanga Zina changamoto sana.
Sema kwa sasa hivi umeme wa elfu 10 haukai kabisa! Hata week mbili ukimaliza unashukuru! Unit zimepanda bei sijui
 
Duu sasa hapo mwenye nyumba sii afunge submeter NV power . Yaani umeme wako ukiisha unakata kwako. Unaaamua unajinunulia wewe wa kiasi gani hata 2000 hii imesaidia kuondoa migogoro ya wapangaji watukutu. Yaani hata mwenye nyumba akiishiwa analala giza
Sio unakaa nyumba hata kusaga juice kelele kuwa unamaliza umeme
 
Hasa hizi nyumba za standard ya chini,,unakutana na watu walio choka kimaisha..
Sana nyumba nyingi za bei che zinachangamoto mno. Na kuishi kwenye such kind of house unaweza kujikuta cost of living ni kubwa kuliko nyumba standards.

Issue nyingine za hizi nyumba ni ugomvi, hasa unapojaribu kuhususha issue za michango au kusolve kero fulani. It's better unatafuta amani, na pia ukawa mbinafsi tu kuliko kutafuta low standard, ukawa very social ukidhani utaishi kwa amani.
 
Sema kwa sasa hivi umeme wa elfu 10 haukai kabisa! Hata week mbili ukimaliza unashukuru! Unit zimepanda bei sijui
Nadhani ni matumizi, Kuna kiwango ukivuka umeme unalipia tofauti na watu wengin. Kupandishwa grade same unit unazonunua kwa 10k mtu mwingine anapata zaidi ya hizo.
 
Back
Top Bottom