Waziri2025
Senior Member
- Sep 2, 2019
- 148
- 379
Wapangaji zaidi ya 30 wa nyumba Za kuishi zilizoko kijenge jijini Arusha zinazomilikiwa na kituo cha mikutano cha kimataifa Arusha,(AICC) wamekituhumu kituo hicho kuwapangisha kwenye nyumba mbovu zilizooza na zimekuwa zikivuja kama mwembe wakati wa mvua.
Katika kikao chao cha Siri kilichofanyika majira ya usiku katika msitu uliopo Kando na nyumba hizo za kijenge, waandishi wa habari hawakuruhusiwa kufika na wale waliofika walitimuliwa.
Wapangaji hao wakiongozwa na Kiongozi wao, Elisia Gama (Binti CCM) walionesha kuwa na nia ovu ya kutaka kukihujumu kituo hicho kikimbiwe na wapangaji na hivyo kukosa mapato ya kujiendesha.
Kikao hicho kilianza majira ya Saa 12 jioni Kwa hoja mbalimbali, ikiwa Madai yao makubwa ni kulalamikia uongozi wa kituo cha AICC kutokukarabati nyumba Zake kiasi kwamba baadhi ya nyumba zinavuja kama mwembe wakati wa mvua, kupandishiwa kodi pamoja na kuombwa rushwa na baadhi ya watendaji wake Pindi wanapompangisha Mteja Mpya.
"Mimi mwenyewe lililipa sh, Laki nne kando na kodi ili kupata nyumba hapa AICC huu ni mradi unaofanywa na watendaji na wamwgeuza dili ya kujipatia fedha haramu" alisikika Esilia alisema.
Baadhi ya wapangaji walisikika katika kikao hicho wakidai ni bora kuhamasisha watu wasusie kupanga ili zibaki magofu hatuwezi kuishi nyumba mbovu, tunaandika barua za malalamiko lakini hakuna chochote.
Mkurugenzi wa AICC, Elishilia Kaaya alisema hakuna mpangaji aliyefika ofisini kulalamika ila alisema wapangaji hao wengi wao ni wadaiwa sugu na wanatumia kigezo hicho kukwepa kodi ya pango.
Kaaya alimtaka mpangaji anayeona hastahili kuishi katika nyumba hizo aondoke.