AICC kukuza uchumi wa nchi katika uwekezaji

Apr 9, 2022
66
32
Na. Mwandishi Wetu,

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) Ephraim Mafuru amesema kituo kinajiimarisha na kujipanga zaidi kimkakati, katika mipango yake ya baadae ambapo sio kutoa huduma kukodisha kumbi za mikutano tu bali ni pamoja na kujenga hoteli kubwa za nyota tano na nyumba mbalimbali za kupangisha, ikiwa ni pamoja na kufanya marekebisho ya majengo ya zamani.


Amesema, lengo la AICC sio tu kukodisha kumbi za mikutano bali kusaidia kukuza uchumi za nchi katika Nyanja ya uwekezaji zaidi ili kuongeza pato la Taifa.

Mafuru ameyasema hayo Septemba 14, katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa JNICC jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza katika kikao kazi na wahariri wa vyombo vya habari nchini.

Amesisitiza kuwa, serikali iko katika hatua za mwisho za kuidhinisha uboreshaji wa JNICC. Lakini pia inajiandaa na ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa kufanyia mikutano ya watu 2500,wenye 10000 sqm na nafasi ya maonyesho utakaokuwa na vyumba 3 vya VVIP na vyumba vingine 4 vya mapumziko vyenye uwezo wa ‘pax’ 150, pia uboreshaji wa ‘AV’ ya kisasa na mfumo mzuri wa sauti na uta runinga.

Vilevile ameonyesha umuhimu zaidi katika na kujali wateja hususani katika upande wa chakula kwa kuihabarisha hadhira kuwa wana mpango wa kuwa jiko la kisasa lenye ubora na viwango kwa ajili ya kuhakikisha usalama na ubora wa chakula kwa wageni hapo baadae.

“Lakini pia Kituo kinadhamiria kupanua wigo wa kibiashara kwa kujenga vituo zaidi Zanzibar na Dodoma ili kuongeza idadi ya watu kufika 2000, ambapo nchi itaingiza mapato zaidi na kufikia USD 96m kwa mwaka”, amesema Mafuru.
 
2027 Arusha wa host mkutano wa masuala ya nyuki wa washiriki zaidi ya 6,000 nilitegemea wangejenga ukumbi wa kukaa watu kuanzia elfu 10,000 kwa faida ya miongo mingi ijayo.AICC wangekuja na mipango ya kujenga hoteli za Nyota 5 zenye uwezo wa kulaza watu 1,000 kwa wakati mmoja hii pamoja na setka binafsi ingewasaidia kuhost mikutano mikubwa kwa wakati mmoja hasa Arusha.
 
Back
Top Bottom