Msimlaumu Babu wa watu wala kiongozi yeyote wa dini maana wao ni viongozi wanaohubiri suala la imani na Babu alisema kabisa wazi kwamba ili mtu upone inabidi uwe na imani, sijui kwanini watu walikuwa wagumu kuelewa.
Nothing to say sorry for Miss.It's quite ok i was just thinking aloud kwa sababu niliona ni moja ya watu waliokuwa wakichangia sana wakati ule hii single ya Samunge ilipokuwa "inahit"
Kifupi huyu babu ni muongo na dawa yake haitibu haya magonjwa.Acha aburuzwe mahakamani,kama kuachwa huru akaachwe hukohuko mahakamani,pengine itakuwa somo kwa matapeli wengine
Lizzy,Imani yao ndio iliyotakiwa kuwaponya...imani yao ikakataa kuwaponya.
Imani yao ndio inayotakiwa kufikisha kortini..kama kweli wana nia.Wamwache babu wa watu maana yeye hakusema ni daktari wala mtenda miujiza.Kama walichagua kutokumuelewa aliposema imani ya wanywaji ndo itakayowapona ni makosa yao wenyewe!
Alichodanganya ni nini wakati alisema tiba yake ni ya kiimani? Unajua maana ya imani? Ukijua maana ya imani basi utaona kuwa hakuna kesi hapo.
Acha kutetea ujinga kwa maswali ya kipuuzi.Babu ni muongo,dawa yake haitibu hayo magonjwa.Wewe una uwezo wa kupima imani ya mtu?au huyo babu yako tapeli aliyeoteshwa na mungu wake feki,ana uwezo wa kupima imani ya mtu?umeshaambiwa watu mpaka wameuza viji asset vyao tegemezi,mpaka wamekopa,wameacha matibabu hospitali,wamesafiri kilomita kibao na kusubiri sana kwenye foleni ili wapate dawa ya babu,lakini hawakupona/wamekufa.Imani gani unayozungumza hapa?
Ni wazi hujui maana ya imani na ndiyo maana unang'aka kama fisi aliyenyang'anya kipande cha nyama mdomoni.
Mimi nasema hivi, hapo hakuna kesi. Kama wanadhani wana kesi acha na waende huko mahakamani and if needs be I'll step and defend Babu by myself pro bono coz it's a slam dunk case.
wewe sema imani nini according to you na huyo babu tapeli?naam ni kweli kwa mahakama zenu,hakuna kesi hapo maana wahusika ni nyie kwahiyo ni sawa na kesi ya nyani kumpelekea ngedele ahukumu,au vipi?
Babu alichotapeli ni nini? Na kuhusu imani, kama hujui tafuta kamusi usome fasili yake.
<br />Walioenda kwa Babu walikua na imani kwamba Babu katumwa na Mungu kumbe wapi, katumwa na mashetani.
Katapeli kuwa dawa yake inatibu magonjwa sugu yasiyotibika hospitali.Umesema,sijui imani nini,sasa tuambie wewe unayejua imani maana yake nini kwa faida ya wengi hapa jamvini na siyo kuniambia nitafute kamusi.
Dawa ya babu si ya kisayansi. Dawa ya babu ni ya kiimani na hilo aliliweka bayana kabisa tokea mwanzo. Watu walioenda kwake walikuwa wanalijua hilo na kama walikuwa hawalijui basi hilo si kosa la babu kwa sababu yeye aliweka kila kitu wazi.
Sasa utapeli sijui uko wapi hapo wakati kila kitu kilikuwa wazi na hata serikali ilitoa matamko kadhaa kuwa hiyo dawa si ya kisayansi. Babu hana kesi ya kujibu. Wamwache babu wa watu apumzike na kufurahia ustaafu wake.
mbona husemi imani maana yake nini?ok dawa yake ya kiimani kama unavyodai,kwanini aliwahakikishia watu kuwa inatibu magonjwa sugu yaliyoshindikana hospitali?Kwahiyo kisheria si kosa kudhuru/kuua watu kwavile tu mauaji ni ya kiimani?