Waombolezaji watupa jeneza katika lango la kituo cha polisi

Waombolezaji watupa jeneza katika lango la kituo cha polisi

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,276
1472925699757.jpg
Kulitokea kizaazaa katika kituo cha polisi cha kisumu Nairobi,ambapo waombolezaji walipoacha jeneza katika langoni mwa kituo cha polisi kwa hasira

Inadaiwa walikuwa wanateta baada ya polisi kumkamata dereva na msaidizi wake aliyekuwa akiwasafirisha hadi eneo la mazishi.

Maafisa wa trafiki katika soko la Otonglo lililoko eneo la barabara ya Kisumu - Busia, waliikamata Matatu (daladala) iliyokuwa ikiwasafirisha kutoka hospitali ya kaunti ya Kisumu kuelekea Gem Akala.

Inadaiwa Matatu hiyo ilikiuka sheria za trafiki

"Wamesema tulipe faini ya shilingi 7000 na sisi tumepata shilingi 5000 inafaa kuturuhusu kwenda mazishini "alisema David Owaga akilalamika baada ya polisi kuwachelewesha kwa muda wa saa nne.

Waombolezaji waliamua kulibwaga jeneza katika lango la kituo cha polisi jambo liliwafanya polisi kuangalia namna ya kuwaachia

Waombolezaji waliondoka kituoni baada ya wawili hao kuachiliwa kutoka kituo hicho.
 
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
Hivi otongolo bado legal currency KE. Natania tu.
 
Back
Top Bottom