Wanzibar ni vigeuvigeu?

Kwani ni lini hawa watu wameanza kuwa na akili! Mimi siwashangai hata kidogo ndivyo walivyolaaniwa hivyo. Nilishawasamehe bure. Wacha tuwabebe tu kwenye huu Muungano maana tukiwaacha peke yao tumewapoteza.

Mzee kuwa na staha kidogo. Unawatukana hata ambao hawahusiki na maamuzi au hizo harakati za kuchoma baa.
 
Mara kwa mara viongozi wa serikali ya Zanzibar wamekuwa wakipinga makampuni ya pombe kudhamini michezo Zanzibar pamoja na kilio cha vyama vya michezo vya huko kuishawawishi serikali yao bila mafanikio.

Na hivi sasa kumekuwa na wimbi la uchomaji bar huko visiwani kisingizio cha imani ya dini, lakin cha kushangaza mwishoni mwa wiki Makamu wa pili wa rais mh. Balozi Seif Idd alipokea milion 10 kutoka TBL kama msaada kwa wahanga wa ajali ya meli.

Kama kweli serikali inapinga pombe wangegomea pesa hizo chafu za wauza pombe ambayo ni haramu au ni ndio baniani mbaya kiatu chake dawa.

..nilimwani mwanasiasa nikampa kura yangu mwishowe akanigeukia..
 
Du!!! Sasa waislam wanaofanya kazi tbl? Pesa zao nzuri kweli?
Wanaweza kwenda kuhiji kwa mshahara wa tbl?
 
Wanapinga udhamini ambapo maana yake ni promosheni ya pombe ktk maeneo yake ambapo ita sababisha kuwa na walevi wengi ktk jamii ya watu wachache na kusababishwa kudhoofika kwa nguvu kazi ,kurutubisha umaskini na utovu wote wa maisha mabovu ndani ya jamii.
Na kutoa msaada si promosheni -my views
 
Hawakatai pesa bali wanakataa kuitangaza pombe.. Timu za mpira watalazimishwa kuvaa jezi zenye nembo ya Tbl.
 
Waislamu wote hata wa bara ni vigeugeu. Sasa hivi waislamu wa Bara wanaomba kuanzisha mahakama ya kadhi ambayo wanataka igharamiwe na serikali. Serikali imewaambia waislamu waanzishe na kuindesha wenyewe lakini hawataki wanataka kodi za serikali ndiyo ziendeshe mahakama ya kadhi.

Juzi tu Pinda amesema bungeni mlipa kodi mkubwa nambari moja ktk JMT ni TBL (kampuni ya bia). Sasa je waislamu wako tayari mahakama ya kadhi iendeshwe kwa pesa zitokanazo na pombe ambayo kwa mjibu wa imani yao ni haramu?

Shuhudia majibu ya waislamu kuhusu hili swali. And be the juror yourself.

Zanzibar hawakatai kuuza pombe bali wanakataa baa za mitaani ambazo kisheria nimarufuku kwa zanzibaar ila kwa bahati mbaya bahizo ziko na zimesimama katika mazingira ya rushua lakini sio kisheria.
Serekali ya zanzibar inamiliki hoteli kila mkoa wa zanzibar na ziko katika miji na zinauza vileo kila aina kwa mujibu wa sheria,na pia ziko hoteli za kitalii kila kona ya fukwe ya zanzibar lakini mbona hatujasikia bugudha yoyote na zinauza pombe pia na haijatokezeapo kuchomwa moto ni kwakua zimekaa kisheria. au hamulijui hilo? hamujiulizi kwanini zichomwe baa za mititaani tu?

Kuhusu serekali kukataa pesa Haramu hilo halitakua wakwanza zanzibar kwani si tunajua kua biashara ya unga Heroin na kokein ni haramu,hilo halina sura ya dini wala serekali lakini watuhumiwa wakikamatwa na pesa walizozipata kwa njia haramu hazichomwi moto wala kuchanwa bali huingizwa serekalini na zikatumiwa kama zile pesa za walipakodi wengine, au Mavi anye bata tu akinya kuku kahara?
 
Kwani ni lini hawa watu wameanza kuwa na akili! Mimi siwashangai hata kidogo ndivyo walivyolaaniwa hivyo. Nilishawasamehe bure. Wacha tuwabebe tu kwenye huu Muungano maana tukiwaacha peke yao tumewapoteza.

Mukiacha kutubeba tutapata shida mana mushatuzoesha migongo yenu.
 
watu wa visiwani huwa wana akili za kubadilikabadilika kila leo na huwa hawaeleweki! mfano mzuri ni hao waingereza kila kukicha wanabadilikabadilika nadhani maupepo ya bahari huwa yanaathiri akili ya binadamu!
 
Nadhani kwa jambo la dharura kama hili inabidi upime uzito wa hitaji au tatizo na athari za kutopata huo msaada.
 
hawa wazanzibar hata mi wananishangaza sana. wanapinga pombe wakati cocaine and nude beaches ziko kibao hapo visiwani. beach kibao pale zenji utakuta mademu wa kizungu wanatembea uchi au wanapewa massage na hao hao wazanzibar (waislamu) au cocaine ipo nje nje. pure hypocrisy.
 
duu basi hii dharura ni ya ajabu....inayohalalisha haramu kuwa halali ...
uislaam ni dini inayomjari muumini akiwa ktk mazingira magumu mfano nguruwe ni haramu, lakini ktk mazingira fulani ya njaa na hakuna chakula chochote kile zaidi ya nguruwe, ili kunusuru maisha muumini dini inamruhusu muumini huyo kumega kipande cha nguruwe huyo na kuweza kula, sembuse pesa iliyotokana na pombe kwenye ajali iliyogharimu watu zaidi ya 200 na majeruhi wengi wakihitaji msaada
 
Back
Top Bottom