Haya mawazo ni pungufu sana mkuu.Kumbuka kwamba kitunguu ni kiumbe hai,kwa hiyo kina uwezo wa ku-break down sumu,kama na wewe kiasi fulani ulivyo na uwezo huo, kama huja overload ini lako kwa masumu!Come back to your senses mkuu,acha kutetea vitu visivyofaa.Na hata kama vitunguu visingekuwa na uwezo wa ku-break down poisons,si busara kupunguza the amount óf poisons going into your body, ili ulipunguzie ini mzigo?
soda mimi nakunywa kama kawa, siku sumu ikijaa ntakufa kama ndio itakuwa sababu ya kifo changu. landa uniambie yupi hata mmoja hajanywa soda mpaka leo anaishi tokea karne ya 19
soda mimi nakunywa kama kawa, siku sumu ikijaa ntakufa kama ndio itakuwa sababu ya kifo changu. landa uniambie yupi hata mmoja hajanywa soda mpaka leo anaishi tokea karne ya 19
Sawa mkuu, endelea,ila hiyo ni logic na msimamo wa ajabu sana,mbona soda sio chakula?Labda unahitaji kuhoji kwa nini unapenda kitu ambacho wala hakina manufaa yeyote mwilini mwako kiasi hicho.Jibu ni kwamba wewe umeshakuwa addicted na caffeine na cocaine walizoweka huko.Hata hivyo with determination naamini unaweza ku-break hiyo addiction.Mbona mimi niliweza many years ago.Ila pole.
ASILI YA NENO COCA COLA NI MMEA WA COKE AMBAO NDIO SOURCE YA COCAINE KWA HIYO NASIKITIKA WALE WANAOILANI POMBE HUKU WAKIBUGIA SODA NA NDIO MAANA UKIMALIZA MOJA UNATAMANI INGINE KWA AJILI YA HIYO ILI UWE ADDICTED 😱😱😱😱😱😱😱😱😱
ASILI YA NENO COCA COLA NI MMEA WA COKE AMBAO NDIO SOURCE YA COCAINE KWA HIYO NASIKITIKA WALE WANAOILANI POMBE HUKU WAKIBUGIA SODA NA NDIO MAANA UKIMALIZA MOJA UNATAMANI INGINE KWA AJILI YA HIYO ILI UWE ADDICTED 😱😱😱😱😱😱😱😱😱
ASILI YA NENO COCA COLA NI MMEA WA COKE AMBAO NDIO SOURCE YA COCAINE KWA HIYO NASIKITIKA WALE WANAOILANI POMBE HUKU WAKIBUGIA SODA NA NDIO MAANA UKIMALIZA MOJA UNATAMANI INGINE KWA AJILI YA HIYO ILI UWE ADDICTED 😱😱😱😱😱😱😱😱😱
Mkuu umechanganya madawa sana!Ngoja tuweke mambo sawa.
Coca Cola ni kinywaji mkuu, ambacho kimechanganywa na Cocaine kiasi kidogo na kemikali nyingine.Hii cocaine kidogo ina nia ya kuifanya Coca Cola iwe addictive.Wamechanganya pia na Caffeine kwa nia hiyo hiyo. Cocaine inaitwa pia Coke, na ni very addictive.Cocaine inatokana na mmea unaoitwa Coca ambao unalimwa sana South America.
Mkuu umechanganya madawa sana!Ngoja tuweke mambo sawa.
Coca Cola ni kinywaji mkuu, ambacho kimechanganywa na Cocaine kiasi kidogo na kemikali nyingine.Hii cocaine kidogo ina nia ya kuifanya Coca Cola iwe addictive.Wamechanganya pia na Caffeine kwa nia hiyo hiyo. Cocaine inaitwa pia Coke, na ni very addictive.Cocaine inatokana na mmea unaoitwa Coca ambao unalimwa sana South America.
Imeandikwa "Watu wangu wanaangamizwa kwa Kukosa maarifa"
Sishangai sana kuona kuwa kunawatu ambao wanapuuza mambo ya msingi!
Leo hii ukienda Kwenye mahospitali Watu kibao wanaumwa magonjwa yasiyo ambukiza ambayo kimsingi kwa asilimia kubwa yanaepukika!
Imeandikwa " Mkamate sana elimu usimwache aende zake maana Ndiyo uhai wako"
Nimekuwa nikitafali kwa kwa nini Mungu amesema elimu ni uhai?
Maarifa yana muwezesha Mtu kuepuka kuangamia!
Mtu anaambiwa epuka kula vyakula vyenye mafuta mengi, chumvi nyingi, sukari nyingi hasa Za viwandani, epuka vyakula vinavyohifadhiwa (preserved foods), epuka vyakula vilivyo chakatwa(processed food) n.k lakini waTZ walio wengi wanapuuza!
Sasa Mtu atakapoanza kuumwa ndo anaambiwa na Dokta siyo tu atumie kidogo anaambiwa usitumie kabisaaaa!
Na gharama Za Kutunza wagonjwa ni kubwa kuanzia madawa na vyakula!
Wengine wakipata ugonjwa anaambiwa ale Dawa na maisha Yake yote akaacha anaondoka !
Mwenyezi Mungu nakuomba uzidi kutunusuru na mabaya yote! Yatuepuke mabaya Baba!
AFYA za mamilioni ya Watanzania wanaotumia vinywaji vya aina ya soda ipo hatarini, baada ya kugunduliwa uwepo wa chembechembe zenye kemikali za sumu ndani ya vinywaji hivyo, MTANZANIA Jumatano linaripoti.
Utafiti uliofanywa na Muungano wa Waandishi wa Habari za Uchunguzi Tanzania (Investigative Journalists Union of Tanzania- IJUTA) pamoja na tafiti zilizofanywa na wataalamu waliobobea katika afya ya umma duniani, umebaini kuwa vinywaji baridi aina ya soda ni hatari kuliko utumiaji wa sigara inayosababisha maradhi ya kansa katika mwili wa binadamu.
Kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi mbalimbali duniani, yapo madhara makubwa ya utumiaji wa vinywaji vya aina ya soda katika mwili wa binadamu.
Utafiti huo unaonyesha kuwa zipo sababu nane kuu zinazokiweka kinywaji aina ya soda kwenye kundi la vinywaji vyenye sumu ambavyo havifai kwa matumizi ya binadamu.
IJUTA imebaini kuwa makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji baridi aina ya soda yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo yake, bila kutaja madhara ya vinywaji hivyo kwa binadamu.
Kwamba matangazo hayo yanayogharimu mamilioni ya fedha ndiyo yanayokifanya kinywaji hicho kuwa maarufu zaidi duniani, licha ya kuwa na madhara makubwa katika mwili wa binadamu.
Aidha, utafiti huo unaonyesha kuwa umaarufu mwingine wa kinywaji aina ya soda ni utamu wa kupindukia ulio ndani ya soda.
Utafiti wa IJUTA unaonyesha kuwa utamu wa kupindukia iliomo ndani ya soda unawapumbaza wanywaji ili wasisikie ladha kali ya asidi iliyomo ndani ya soda.
IJUTA imegundua kuwa kiwango cha asidi kilicho ndani ya soda hakiwekwi wazi kwa walaji kwa sababu ya kuhofia kuwa wakibaini wataacha kikutumia kinywaji hicho.
Inaelezwa pia kuwa madini ya cola yaliyo ndani ya soda yana kilevi aina kafein kinachomteka mnywaji kuwa teja wa kinywaji hicho.
Tafiti za kitaalamu zimeonyesha kuwa soda inahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa watoto na watu wazima, yakiwemo matatizo ya kuongezeka unene kupita kiasi, ugonjwa wa ini na mengineyo.
Utafiti uliofanywa nchini Marekani unaonyesha kuwa soda huwekewa ‘fructose’ (sukari) nyingi kupitia mfumo wa sirapu (fructose corn syrup) ambayo inaongoza kwa kusababisha magonjwa ya unene, kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine sugu yanayowakabili Wamarekani wengi hivi sasa na dunia kwa ujumla.
Dk. Mercola, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya lishe asilia na tiba mbadala nchini Marekani, amekaririwa na tafiti mbalimbali zilizofanyika nchini humo akieleza kuwa kinywaji aina ya soda ni hatari kwa binadamu, sawa na mtu anayevuta sigara au zaidi, jambo alilosisitiza kuwa siyo la kutia chumvi, bali ukweli halisi.
Watumiaji wa vinywaji aina ya soda wanaelezwa kuwa wamekuwa wakinywa kiasi kikubwa cha kaboni, kafeini (dawa ya kulevya), sukari ya kupundukia na asidi kali ambayo huvuruga afya ya mtumiaji kwa kiwango cha juu.
Soda pia imebainika kutokuwa na lishe ya aina yoyote zaidi ya maji na sukari.
Uchunguzi wa IJUTA na utafiti ya wanasayansi mbalimbali duniani, umeonyesha kuwa watu wengi hawajui kuwa unywaji wa soda huwaongezea kiasi kikubwa cha madini joto.
Chupa moja ya soda yenye ujazo wa mililita 330 husababisha unene kwa kiwango cha paundi moja kwa mwezi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kisukari Tanzania (TDA), Ramadhan Mongi, amepata kukaririwa na vyombo vya habari hapa nchini akieleza kuwa ugonjwa wa kisukari Tanzania umeongezeka mara sita katika siku za hivi karibuni.
Alisema miaka kumi iliyopita, hali ya kisukari ilikuwa asilimia tatu (3), lakini katika miaka ya karibuni umeongezeka mara sita.
“Tunastahili kuongeza jitihada ya kupambana na gonjwa hili la kisukari kwa gharama zote kwa sababu kisukari ni moja ya magonjwa manne yanayomaliza Watanzania,” alisema.
Utafiti uliofanyika Mkoa wa Dar es Salaam ulibaini kwamba kati ya watu watano waathirika wa kisukari, mmoja tu ndiyo hupata matibabu ya serikali.
Unywaji kwa mpigo wa kabohaidrets iliyo na sukari nyingi kwenye soda hudhoofisha seli zinazozalisha vimeng’enya tofauti na vyakula vingine na pia imebainika kuwa sukari ikiingia kwa wepesi kwenye mzunguko wa damu husababisha kongosho kuzalisha vimeng’enya vingi mwilini.
Uchunguzi wa kitabibu katika Hospitali ya wanawake ya Boston nchini Marekani na katika Chuo cha Kitabibu cha Harvard umeonyesha wanawake 51,000 hawakuwa na kisukari mwanzoni mwaka wa 1991, lakini miezi minane baadaye wanawake 741 waligundulika na kisukari.
Ripoti ya utafiti huo ilionyesha kuwa wanawake waliokuwa wakitumia kinywaji aina ya soda moja ama mbili kwa siku waliongezeka uzito maradufu na walikuwa hatarini kupata ugonjwa wa kisukari.
Pia ilionyesha kuwa soda hudhoofisha mifupa na husababisha hali ya mifupa kupuputika, hali inayomuweka mtumiaji kuwa katika hatari ya kuvunjika mifupa kirahisi.
Madhara mengine yaliyobainika kusababishwa na unywaji soda ni kupukutika kwa meno na ama kuoza. Pia soda husababisha matatizo ya figo.
Soda yenye chembe ya cola husababisha figo kuwa na mawe kwa sababu ya asidi na kemikali mbalimbali zinazofichwa vipimo vyake kwa walaji.
Madaktari bingwa wa wanamichezo wanaeleza madhara yanayosababishwa na soda mwilini kuwa ni pamoja na shinikizo la damu, uharibifu wa ini, huvurugu mfumo wa kumeng’enya chakula tumboni kutokana asidi ya kiwango cha juu iliyo kwenye soda.
Wanashauri kuwa soda haistahili kutumika kama kishawishi kwenye mchezo, kwa sababu ina madhara makubwa kwa wanamichezo kwa sababu hunyonya maji kwenye mwili na kudhoofisha mwili.
Wakati utafiti huo ukidhihirisha hayo, Taasisi ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imeshindwa kutoa tamko lolote kuhusu utafiti huo, hata baada ya kupelekewa maswali kwa maandishi yanayoomba ufafanuzi wa ubora wa vinywaji vya soda katika mwili wa binadamu.
Yaani ndiyo mnajua sasa wakati watu wameshaumia.Too little to late.Ndio maana mimi siiamini serikali yeyote duniani.Kama wanaruhusu wananchi kuuziwa sumu, tutawaaminije kwenye C-19 vaccines.Upuuzi mtupu.
Kati ya soda na kitimoto kipi kina madhara zaidi ? Nyanya zilizopuliziwa madawa makali je ? Mafuta ya korie yale ya chura nayo utasemaje ? Moshi wa magari na viwandani ? Hzo chipsi na bager na kuku broiler utasemaje ? Anyway kila mtu afate anachoona ni sahihi...but Pepsi ya bardi iache hivyo hivyo
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.