Wanyakyusa sio Mwa, Mwa.. tu!

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
May 15, 2009
7,325
6,813
Uchunguzi wa haraka haraka umeonyesha kabila la Wanyakyusa sio tu lina majina yenye mwanzo wa Mwa..., Mwa.. .
Imethibitika pia kuwa kwao kila jina linaloanzia na herufi 'A' linaishia na herufi 'E' na kila linaloanza na herufi 'L' linaishia na 'O'!

'A' kuishia 'E'
Asangalwisye
Andendekisye
Anyigulile
Ambwene
Afyusisye
Anyambilile
Andongolile
Asumwisye
.........nk malizia.

'L' kuishia 'O'
Lugano
Lutufyo
Lusekelo
Lusubilo
Lusajo
Lupakisyo
......na mengineyo.

Nao hawa kwa mbwembwe!
 
ahhaahaha wenyewe waje hapa jamvini wajibu....ila ninavyojua mimi kila moja lina maana tena ya Ki Imani zaidi...
kama
Anyigulile-Amenifungulia yaani kama zawadi hivi
Andendekisye(Andy)ametengeneza au amefanya
Ambwene-Aeniona au amesikia kilio changu..

Nk nk....ndaga fijo.......
nimesomea huko najua jua kidogo.
 
ahhaahaha wenyewe waje hapa jamvini wajibu....ila ninavyojua mimi kila moja lina maana tena ya Ki Imani zaidi...
kama
Anyigulile-Amenifungulia yaani kama zawadi hivi
Andendekisye(Andy)ametengeneza au amefanya
Ambwene-Aeniona au amesikia kilio changu..

Nk nk....ndaga fijo.......
nimesomea huko najua jua kidogo.

Alaa kumbe, mie nilipodokezwa nilidhani ni majina ya mizizi! (dawa za kienyeji!)
 
mara nyingi majina ya ukoo yananzia na Mwa;

Mwankenja
Mwampondele
Mwakasyuka
Mwainyekule
Mwamlima
Mwakyusa
Mwasongwe
Mwakalebela
Mwakalindile
Mwamunyange
Mwaipopo
Mwakyusa
Mwakalobo
Mwakibibi
Nk:
 
Wahaya pia : R huishia na A (sio RA ni R...A)

Rutahindurwa
Rutazengelera
Rugemalira
Rutashobya
Rutahakana
Rumanyisa
Rwegoshora
Rutachunzibwa
Rwegalurila
NK:
 
mara nyingi majina ya ukoo yananzia na Mwa;

Mwankenja
Mwampondele
Mwakasyuka
Mwainyekule
Mwamlima
Mwakyusa
Mwasongwe
Mwakalebela
Mwakalindile
Mwamunyange
Mwaipopo
Mwakyusa
Mwakalobo
Mwakibibi
Nk:

safi sana hii, na hii ya Kibona kutoholewa kutoka kwenye Chibhona!
 
Jamani nimeongezewa mengine;
Andalalisye
Angwemelile
Andukamike
Andetemisye
Angongile

Jamani kina Gwakisa Lole tusaidieni tafsiri please..tusijekuwa tumeandika matusi!
 
Lakini.. inapendeza kuwa na jina la Ukoo, kwa mfano Nkawa Mwakalindile na sio Nkawa George Michael, maana naona siku hizi watu wengi hawapendi kuendeleza majina yao ukoo (kiafrika zaidi) yaani kama baba yake anaitwa George Michael Mwakalindile, yeye ataishia George Michael. Imekaaje hiyo?
 
Lakini.. inapendeza kuwa na jina la Ukoo, kwa mfano Nkawa Mwakalindile na sio Nkawa George Michael, maana naona siku hizi watu wengi hawapendi kuendeleza majina yao ukoo (kiafrika zaidi) yaani kama baba yake anaitwa George Michael Mwakalindile, yeye ataishia George Michael. Imekaaje hiyo?

Uko sahihi ndugu tunayasahau majina yetu,
Hongera kwa Jaji huyu NJENGAFIBILI MWAIKUGILE, pamoja na usomi wake hajaacha asili yake!
 
Kibona si mnyakyusa bali ni mndali. Hata hivyo, majina ya kwanza ya Waandali yanafanana na ya kinyakyusa.

Ieleweke kuwa kwa wananyakyusa. Mwa... inamaanisha mwanaume (mr.). Ndiyo maana mwanamke huitwa jina la uko bila kuanza na Mwa..:

Kalikene
Kalindile
Munyange
Mpondele
kasege (ghe)
kalindile...

Sana sana mwanamke aweza kutamkwa jina lake kwa kuanza na kana...:

kana Kalindile
kana Munyange
kana Kalebela

Etc.

Pia ieleweke kuwa matumizi ya Mwa ni kwa makabila yote yenye asili moja na wanyakyusa. Kwa mfano, wahehe, ingawa wengi wao majina ya uko hayaandikwi kwa kuanza na mwa, bali mwanaume aliyeoa na mkubwa kwa umri lazima uanze na mwa kabla ya kutaja jina lake, ingawa siku hizi baadhi yao hupenda kuandika kwa kuanza na mwa:

mwa...kalinga
mwa...vela
mwa...kikoti
mwa...kitalika

Pia wapogolo baadhi ya majina yao huanza na mwa.
 
Mbona GWALUGANO haiishii na "A"
Gwalugano ni jina la kiume na Lugano ni la kike. Nashangaa siku hizi nimewakuta wanyaki wengi wa kiume wanaitwa lugano nadhani ni ubishoo wa kuliandika na kutamka.

Nadeclare insterest kuwa nawafahamu wanyaki kinoma kwani nina ndugu mnyaki. ingawa mie natokea hukooo kaskazi uwekeni
 
Back
Top Bottom