Wanunuzi wa mpunga/mchele karibuni

Wanunuzi wa mpunga/mchele karibuni

....Umeshawahi kulima mpunga mkuu? Hiyo ni wastani wa gunia 50 kwa ekari, hata kwenye irrigation schemes hupati hiyo.
Mkuu kuna watu wanaongea tu mtu ajawahi kulima anaongea pumba.
ekari 6 uvune gunia 300??
 
Ukifika dar huo mchele tufahamishane,ila mie nataka kwa ajili ya matumizi yangu kama kilo 30 ama 50
 
....Umeshawahi kulima mpunga mkuu? Hiyo ni wastani wa gunia 50 kwa ekari, hata kwenye irrigation schemes hupati hiyo.
Samahan ni miscalculation, kwa ekari sita ni maximum ya gunia 162 za mpunga.
 
Mkuu nawaza tu kwa sauti kwamba kwanini usiukoboe huo mpunga na uuze mchele nahisi kama utapiga pesa sana tofauti na kuuza mpunga kama mpunga.

Halafu kingine unaweza ukatulia kidogo usiuze now ili usibiri bei ikae poa kidogo.
 
nitauza gunia 15 au 20 tu za mpunga ili nipate hela ya kukobolea na kusafirishia mchele kupeleka dar,
 
Hongera mkuu kwa mavuno, naomba kujua ukikoboa gunia moja la debe 7 za mpunga unapata kama kilo ngapi za mchele.
 
Hongera mkuu kwa mavuno, naomba kujua ukikoboa gunia moja la debe 7 za mpunga unapata kama kilo ngapi za mchele.
nazani nishalijibu hilo swari ktk comments zilizopita but sio mbaya km nikijibu tena,
kwa kawaida gunia moja la mpunga ukikoboa unaweza kupata kilo 55 mpaka 65 za mchele, kutegemea na ujazo wa hilo gunia ila kuna wanunuzi wengine wanawalalia wakulima wasio na misimamo na kushindilia zaid wanapojaza gunia hivyo utoa hata kilo. 70 mpaka 80 baada ya kukoboa
 
Sawa ndugu yangu ngoja nijipange nichukue kama gunia mbili kwa matumizi ya nyumbani.
 
Ukifika dar huo mchele tufahamishane,ila mie nataka kwa ajili ya matumizi yangu kama kilo 30 ama 50
MREJESHO.
ndugu wanajamvi, katika mavuno yangu nimefanikiwa kupata gunia 80 za mpunga, ambazo 25 niliziuza kwaajili ya kugharamia shughuri za mavuno, pia baada ya mavuno nikakoboa gunia 30ambazo mchele niliopata nikauza huko huko morogoro nikabakisha gunia 25 ambazo 5 mchele na 20 mpunga ambo juzi nimeusafirisha mpaka dar es salaam ambako ndio makazi yangu yalipo maeneo ya pugu kigogo fresh.
Utoe na location inawezekana tukapitia na chenji zetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gunia 80 masharti kibao hapo bado hajazikoboa.Yaani mpaka msimu uishe hana pesa,maana anauza nusu nusu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom