Sahihi kabisa, unatukumbusha mengi, isitoshe ni kama waliwahi kupiga pamoja katika bendi moja, walipishana kidogo sana (Maneti na Charles) wakati Maneti anakaribia kutoka TK Lumpopo mwishoni mwa 1973 ndipo Charles Ray Kasembe naye alipokuwa akijiunga na bendi hiyo. Huenda kufahamiana huko japo kwa muda mfupi ndipo kulipojenga mashirikiano kutengeneza kibao hiki. Charles Ray Kasembe hatimaye naye alitoka TK Lumpopo na kujiunga na Super Volcano (jambo adimu sana wkati huo yaani kutoka kwa Kilaza kwenda kwa Mbaraka ama kinyume chake lilikuwa jambo gumu).