Wangapi mmeshapanda mlima Kilimanjaro? Tupeane uzoefu

Wangapi mmeshapanda mlima Kilimanjaro? Tupeane uzoefu

Jina lingine linaitwaje?[/QUOTE

Bado sijapata jina lingine mkuu ila ni sehemu unapopaswa kupita kiupande kwa maana njia ni nyembaba na kuna jiwe kubwa ukipita kama unalibusu nashindwa kupaelezea poa sijui kama umenielewa
 
Anzisha utamaduni wa kuwa na adventure yeyote maishani mwako, haata ukiwa busy atleast mara moja kwa mwaka.

Take a vaccation kwenda kuupanda mkuu.

Hutajuta.
Nimeupokea ushauri wako kwa mikono yangu yote miwili.

Ahsante
 
Nilifika Gilman's Point miaka ya 80 (kishule). Nilichoka sana hata kusaini nilishikishwa kalamu bado nikashindwa nikasaidiwa. Hata hivyo nashukuru kufika hapo japo nilidhamiria kufika Kibo kwa sababu waliokuwa wanafunzi wenzetu wanamichezo waliojiamini waliishia njiani wakabebwa na guides kurudishwa chini wakiwa hoi.
 
Wakuu,

Ninajindaa kimwili na rasilimali fedha na muda, In shaa Allah Mungu akijalia August 2016 au September 2016 niupande huu Mlima,Tuhamasishane!!
 
Kweli mkuu
Tufanye hamasa at least watu wanne au watano sio mlima upo kwetu and we don know about it
 
Novemba 18, 2008 nilifika kileleni

  1. Tulianza safari Marangu getini majira ya saa tisa alasiri na kufika Mandara Hut saa 12.30, hapo inabidi upumzike
  2. Tuliondoa Mandara Hut saa 12oo asubuhi na kufika Horombo saa 12 jioni
  3. Tulipumzika kwa siku nzima horombo na kupasha kwa kwenda kilele cha mawezi ambacho kufika ni takiribani masaa 2-3 na kurudi Horombo
  4. Tuliondoka Horombo saa 12 asubuhi na kufika Kibo saa moja jioni na kupumzika
  5. Tuliondoka Kibo saa sita usiku na kufika Gilman saa 12 30-hapo ukifanikiwa kufika unapata Green Certificate tayari maana ni steep sana na unapumzika muda mfupi kabla ya kuelekea Uhuru Peak ambapo tulifika majira ya saa moja unusu na kupiga picha kesha kurudi hadi Kibo ambapo tuliunga hadi horombo na kisha kesho yake kurudi hadi Marangu getini na kuoewa cheti cha dhahabu
Muhimu sana kufuata ushauri wa wangozaji na kutumia vimiminika sana-maji ya kunywa na enegizers, moja ya vitu vinavyokosesha wengi kufika kileleni ni kutumia nguvu kubwa sana wakati wa kutembea ilihali unatakiwa mdogomdogo, chengine hakikisha unakula vyakula vya kujenga nguvu cha ajabu kuna menyu maalum za mlima unazopewa kule ila mtu anakunywa chai na sukari badala ya asali au kutumia blue band badala ya peanut batter etc

SIKU NNE KUPANDA MBILI KUSHUKA............
 
Tuongee uzuri woteeee ila mwisho wa siku hizi routes zinahitaji bajeti.
ukitoa nauli ya kutoka mikoani hadi mkoani kilimanjaro. ni kiasi gani
cha chini ambacho mtu unapswa kuwa nacho kwa route nzima kwenda
Na kurudi pia
Hili swali lako lilishajibiwa mkuu?
 
Back
Top Bottom