Wangapi huwa mnatetemeka mkiwa na hasira? Mnafanyaje kutuli.!?

Wangapi huwa mnatetemeka mkiwa na hasira? Mnafanyaje kutuli.!?

The Dictator

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
4,475
Reaction score
12,281
Kawaida sichukuliagi mambo kwa uzito hata mtu akinikera ila kuna muda najikuta napoteza udhibiti wa hasira najikuta naanza kutetemeka kabisa. Hakuna baridi wala uoga. Najikuta nipo mpakani mwa maamuzi: lolote linaweza kutokea ndani ya muda huo.

Sitamani hali hii kuendelea.

Wengine mnawezaje kudhibiti hasira mambo yanapoenda juu ya kiwango chako?
 
kunywa maji husaidia
 
Pumua taratibu na utulivu kwa kuingiza kiasi kikubwa cha hewa kutumia pua hadi ijae tumboni/kifuani Kisha achilia itoke taratibu kupitia kinywa/mdomoni.

Hesabu mizunguko kumi kwa maana kitendo cha kuvuta na kutoa pumzi ni mzunguko mmoja.

Weka akili na mawazo yako yote katika pumzi yako isikilize na hisi jinsi hewa inavyotoka na kuingia.

Kichwani kwako tambua kuwa unapumua. Pumzi yako ndio msaada wako hadi utakapohisi umekuwa sawa.
 
Back
Top Bottom