Wanga wameninyoa ndevu hazioti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanga wameninyoa ndevu hazioti

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kimox Kimokole, Jul 24, 2010.

 1. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #1
  Jul 24, 2010
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Jamani nina tatizo kubwa kweli naombeni msaada kama kuna anayejua namna ya kutatua;

  Ni hivi, mwezi wa tatu mwaka huu 2010 jumamosi moja niliamka asubuhi na kukuta sehemu ya ndevu zangu imenyolewa tena kipara hasa kinafanya kuwaka, nikajishangaa kwelikweli maana sijawahi kupata kisa kama hiki kabla.

  Sasa huu ni mwezi wa saba unaisha ndevu hazijaota, nifanyeje ndevu ziote jamani mwenzenu!!!!

  Msaada tafadhali wana JF.

  :twitch:
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 23,993
  Likes Received: 2,714
  Trophy Points: 280
  labda mkeo alitaka kukufanyia sapraiz akakunyoa.....shauri ya imani yako haba unadhani umenyolewa na mchawi...hakunaga hivo vitu
   
 3. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,729
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Ujue kile unachokiamini kinaweza kukutokea katika maisha. Kama daima umekuwa na wasiwasi wa kulogwa au kutendewa ushirikina na mtu, basi hayo ndo matokeo yake. Mategemeo/matarajio yako yamei-convince nafsi yako yote mpaka imeweza kukuathiri physically. Ni matokeo ya kisaikolojia kuliko uhalisia. Kwa maneno mengine wewe mwenywe 'umejinyoa' ndevu kwa imani yako mwenyewe kwa vile nafsi yako daima imelilia matokeo hayo. Hakuna cha mchawi.
   
 4. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,681
  Likes Received: 639
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwa jinsi mimi nisivyo zipenda ndevu, ingenitokea hakika ningeshukuru sana!! Anyway, pole sana kwavile wewe unazihitaji na zimenyolewa bila ya ridhaa yako.

  Jamani anayejua jawabu la tatizo hili amsaidie...
   
 5. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 4,841
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  .
  Ajisalimishe kwa Yesu. Huu ndio msaada uliokaribu nae kuliko chochote!
   
 6. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #6
  Jul 24, 2010
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Sina mke Preta, yaani nimeamka tu nikakuta kuna kaduara ka kunyolewa tena kanang'ara kishenzi, sasa kama nilijinyoa kama unavyosema si zingeota? Mbona miezi sasa inakatika hazioti

  kwa anayejua msaada anisaidie tafadhali
   
 7. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #7
  Jul 24, 2010
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Sikujinyoa kaka na huwa siweki wembe chumbani na nalala peke yangu, daima huwa nanyoa Saluni za kiume
  sasa hii fasheni yangu ya ndevu imekuwa haikai vyema tena, mpaka naona aibu
  Msaada tafadhali wana JF
   
 8. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #8
  Jul 24, 2010
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  halafu hilo duara la kunyolewa kama mtu katumia Bikari vile kunyoa yaani duara safi kabisa 360 degree
   
 9. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #9
  Jul 24, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,729
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Hujanielewa katika bandiko langu. Rudia kusoma tena. Sidhani kama ni gumu japo ni la kisaikolojia/ kifalsafa kidogo na kiimani.
   
 10. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #10
  Jul 24, 2010
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  sasa nimejinyoaje ndo najiuliza na mbona hazioti tena
   
 11. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #11
  Jul 24, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,904
  Likes Received: 281
  Trophy Points: 180
  Usikimbilie kufikiri kuna vigagula vimekutembelea!
  Kwa vile umesema unanyoa saluni jaribu sana kwenda hospitali.
  Kuna fangasi zinazotoa mabaka kwenye ngozi na kula vinywelea.Mimi nomeona kitu kama hicho kwa jamaa yangu kichwani, alitibiwa na akapona kabisa.
   
 12. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #12
  Jul 24, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 133
  Kijana maisha yako yapo vibaya fanya uwahi wataalamu haraka.
   
 13. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #13
  Jul 24, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,370
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  nenda ukaombewe na watumishi wa mungu upate amani!
  ila mie nadhani umepata yale mashilingi..aina fulani ya fangasi...muone daktari!
   
 14. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #14
  Jul 24, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 0
  Maradhi ya ngozi labda nenda hospitali
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Jul 24, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,838
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 145
  sijaelewa.... ndevu imenyolewa, tena hazioti...

  labda ziling'oka tu
   
 16. Asante

  Asante JF-Expert Member

  #16
  Jul 24, 2010
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,809
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  Hao wataalamu wanapatikana wapi?
   
 17. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #17
  Jul 24, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 23,993
  Likes Received: 2,714
  Trophy Points: 280
  unawahitaji nikuelekeze?
   
 18. Asante

  Asante JF-Expert Member

  #18
  Jul 24, 2010
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,809
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160

  Au ni akina mzee ndevu mbili?
  . Kama ndiyo hao NO. YESU anatosha.
   
 19. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #19
  Jul 24, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 9,596
  Likes Received: 2,486
  Trophy Points: 280
  wewe ule virutubisho una minyoo, ukurutu au fungus!
   
 20. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #20
  Jul 24, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,534
  Likes Received: 21,011
  Trophy Points: 280
  Ushauri wangu mimi kwanza uhame maeneo hayo unayoishi.....
  Ili uwe clear kujua ni ushirikina au hisia zako...
  Halafu anza sala....
   
Loading...