Wanga wameninyoa ndevu hazioti

Pole Sana Mkuu, inatisha hii. Unaweza ukawa unalala usingizi wa mang'amung'amu kwa kuogopa jamaa kuja kuchukua nywele sehemu nyingine.
 
kama umejenga basi si uoe kwanza?
mkilala wawili hata wanga wataogopa...
au inawezekana una ugonjwa wa kutembea usiku.........
 
Jamani nina tatizo kubwa kweli naombeni msaada kama kuna anayejua namna ya kutatua;

Ni hivi, mwezi wa tatu mwaka huu 2010 jumamosi moja niliamka asubuhi na kukuta sehemu ya ndevu zangu imenyolewa tena kipara hasa kinafanya kuwaka, nikajishangaa kwelikweli maana sijawahi kupata kisa kama hiki kabla.

Sasa huu ni mwezi wa saba unaisha ndevu hazijaota, nifanyeje ndevu ziote jamani mwenzenu!!!!

Msaada tafadhali wana JF.

:twitch:

Duh mkuu pole sana hawa wanga noma. inawezekana ulikorofishana na jirani nini?, maana stori yako imenifanya nicheke sana na kuwakumbukuka hawa jamaa hapa chini
 
Last edited by a moderator:
Umeambiwa wahi kwa Yesu hujajibu chochote! Au na wewe una vya kwako unaogopa kuviachia? Hapo jibu ni Yesu tu mkuu. Ukiwafuata hao unaotaka kuwafuata watakuongezea matatizo mengine kibao.

hahahha huku JF saa nyengine kunachekesha sana.
 
Jamani nina tatizo kubwa kweli naombeni msaada kama kuna anayejua namna ya kutatua;

Ni hivi, mwezi wa tatu mwaka huu 2010 jumamosi moja niliamka asubuhi na kukuta sehemu ya ndevu zangu imenyolewa tena kipara hasa kinafanya kuwaka, nikajishangaa kwelikweli maana sijawahi kupata kisa kama hiki kabla.

Sasa huu ni mwezi wa saba unaisha ndevu hazijaota, nifanyeje ndevu ziote jamani mwenzenu!!!!

Msaada tafadhali wana JF.

:twitch:
Ukitaka Wanga wasiweze kuingia nyumbani kwako jaribu kuwafuga Bata mzinga wawili Mwanamme na Mwanamke umewaweza Wanga hataweza kuingia tena nyumbani kwako. kuhusu kunyolewa ndevu zako jaribu kwenda kwa mtaalam wa kienyeji ataweza kukupa dawa za ndevu zako zikaota kama kawaida kama ni kweli umenyolewa na wanga . Bata Mzinga.jpg
 
Mzizi mkavu...mara ya pili hii unaniwacha wondering if you are not mganga wa kienyeji???
duh:tape::tape:
 
huyo alikuwa malaika kaja kukupunguzia bajeti ya kushave na kuota vipele. Ameona shave cream uliyokuwa unatumia sijui ni ipi itazidi kukutoa majipu na itakutoa mapele.

Kama mashine yako inasimama na antena insearch ndevu kitu gani? au ndevu ndo zinafanya usimamishe? Au kuna tatizo lingine zaidi ya ndevu? watu wanahangaika kuvinyoa ndevu we ndo unaulizia . duh . wewe ni mtaliban?
 
Ukitaka Wanga wasiweze kuingia nyumbani kwako jaribu kuwafuga Bata mzinga wawili Mwanamme na Mwanamke umewaweza Wanga hataweza kuingia tena nyumbani kwako. kuhusu kunyolewa ndevu zako jaribu kwenda kwa mtaalam wa kienyeji ataweza kukupa dawa za ndevu zako zikaota kama kawaida kama ni kweli umenyolewa na wanga .View attachment 11937

Hao bata mzinga wataruhusiwa kulala nyumba moja? je wataruhusiwa kujaamiana? na wanatakiwa kuwa wa rangi gani?

Kweli mzizi mkavu umenipa burudani ya week end na utabibu wako
 
Pole sana kwa hilo tatizo. Inaweza kuwa ni tatizo la fungus liliathiri eneo hilo nywele zikanyonyoka ukadhani umenyolewa na wanga. Jaribu kuwaona wataalamu wa tiba za ngozi unaweza pata msaada zaidi.
 
weka photo hapo niuone huo mng'ao ntakupa msaada fasta man....ndevu dili hata kama unazinyoa mwana
 
Nashangaa watu tunajifanya kuwa hatujui uchawi upo. Tunafanya bidii kubwa kujisadikisha kuwa mambo ya uchawi ni nadharia tu na jinsi mtu binafsi anavyoyachukulia. Huu ni uongo. Uchawi upo na unafanya kazi. Inawezekana kweli umenyolewa kichawi na hao wachawi kuna shughuli wanaifanya kutumia ndevu zako. Nakushauri uende pale Tanganyika parkers kuna kanisa linaitwa Ufufuo na Uzima watakusaidia. Aiseee hao jamaa wana maombi hatari sana kwa mtu anaonewa na wachawi.
 
Hao bata mzinga wataruhusiwa kulala nyumba moja? je wataruhusiwa kujaamiana? na wanatakiwa kuwa wa rangi gani?

Kweli mzizi mkavu umenipa burudani ya week end na utabibu wako

Bata Mzinga si nimekuonyesha kwenye picha uwafuge kwenye mabanda yao rangfi yoyote ile.
 
huyo alikuwa malaika kaja kukupunguzia bajeti ya kushave na kuota vipele. Ameona shave cream uliyokuwa unatumia sijui ni ipi itazidi kukutoa majipu na itakutoa mapele.

Kama mashine yako inasimama na antena insearch ndevu kitu gani? au ndevu ndo zinafanya usimamishe? Au kuna tatizo lingine zaidi ya ndevu? watu wanahangaika kuvinyoa ndevu we ndo unaulizia . duh . wewe ni mtaliban?

Mkuu Mtazaöaji unanifurahisha sana kwa maneno yako
 
Unahitaji sala

wasiliana na kanisa huyu baba atakusalia huitaji mengi kuwa na imani tu

yumo kwenye channel za free to view hapa bongo

usaliwe

ni uchawi tu huo wanakuzuilia kitu maishani mwako au vingine vingi
mara nyingi ni wanafamilia...
havianziagi mbali kama hujakosana na mtu maishani

ubarikiwe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom