Wanazuoni qua Coet nchini

RAYAN THE DON

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
679
1,194
Habari wanabodi? Poleni sana wakuu kwa mapambano makali dhidi ya hili janga la korona.

WanaJF wenzangu bila kukupesa macho nomba tusaidiane kuwakumbusha wanazuoni wa vyuo mbalimbali hapa nchini hasa katika kada za udaktari na uhandisi wasijisahau kutenda yale yaliyo katika uwezo wao. Ninawaomba mtumie uwezo wenu binafsi mkishirikiana na uongozi wenu wa chuo ili mtengeneza mashine za kupumulia(Ventilators). Msipende kujisahaulisha wadau wetu.

Huu ndiyo muda wenu wa kutuonesha maarifa na ujuzi mnaoupata huko vyuoni. Mfano kuna chuo kimoja nchini Rwanda wanazuoni hao wamefanikiwa kutengeneza mashine ya kupumulia(ventilators). Hivyo, kwa upande wao wamejinasua katika kuagiza mashine hizo.
Kwani wanazuoni wa Rwanda au Kenya wanawazidi nini?

Amkeni amkeni amkeni amkeni toka usingizini ili muoneshe uwezo na ujuzi wenu.
Najua mtakuja na excuse kwamba hampati uwezeshwi ila kwangu mimi hiyo ni upuuzi mkubwa sana. Ili uwezeshwe lazima uoneshe uwezo wako ndipo watu watawekeza katika huo ujuzi wako.

Sambamba na hilo, kuna kaka zenu walipata hayo masomo lakini nao wapo kimya hakuna sana. Kiukweli inasikitisha sana.

To be honest, nilikuwa na ndoto za kuja kumsomesha mwanangu masomo ya udaktari/uhandisi lakini nimeona hakuna kitu kabisa huko. Sitaki kumuingiza mwanangu katika shimo ambalo atajuta katika maisha yake yote.

Karibuni kwa michango wakuu.

Ahsanteni.
 
Amkeni amkeni amkeni amkeni toka usingizini ili muoneshe uwezo na ujuzi wenu.
Najua mtakuja na excuse kwamba hampati uwezeshwi ila kwangu mimi hiyo ni upuuzi mkubwa sana. Ili uwezeshwe lazima uoneshe uwezo wako ndipo watu watawekeza katika huo ujuzi wako.
 
Kutojiamini ndio changamoto ya kwanza inayofifisha uthubutu. Naamini wakiungana na kuthubutu wanaweza kufanya jambo
 
Hao wanazuoni wako wenyewe waweza kuta mpaka umri huu walionao hawajawahi kuiona hio ventilator kwa macho (live) zaidi ya kuiona kwenye taarifa ya habari ya BBC swahili.
 
Hao wanazuoni wako wenyewe waweza kuta mpaka umri huu walionao hawajawahi kuina hio ventilator kwa macho (live) zaidi ya kuiona kwenye taarifa ya habari ya BBC swahili.
Mhhh basi vyuo vyetu ni utopolo mtupu.
 
Back
Top Bottom