Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 10,651
- 22,819
1. Zamani : Mwanamke anakutana na mwanaume kakonda hana mwili, kimoyomoyo " huyu mwanaume hana mtu anayemtunza hadi ana dhoofu afya nipambane niolewe nae nimtunze hadi apendeze"
Sasa : Mmmmhmn MUNGU aniepushe na hiki kikombe, mtu kakondeana kama mti wa dawa afu anajiamini kunitongoza, usikute ana ngoma,hebu ukoo"
2. Zamani: Mwanamke anakutana na mwanaume miaka 30 bachelor hana hata mtoto. "MUNGU kajibu maombi yangu kanipa wa kwangu wa kujehga nae familia from scratch"
Sasa : Mmmmhmn huyu atakuwa ni muhuni,ogopa mwanaume ambaye hajazaa na mtu na hana hata mtoto wa kusingiziwa. Mimi hapana kwakweli ni bora niendelee kuwa single kuliko mtu wa hivi"
3. Zamani: Mwanamke anatongozwa na mume wa mtu. " Mmmmhmn hii si sawa,nitapata laana kuvunja ndoa ya mtu,watoto watateseka wazazi wao wakitengana,na ni dhambi kwa MUNGU wacha tu nisubirie kupata wa kwangu"
Sasa: " ooooh Hallelujah,ngoja niende kwa mwamposa kutoa sadaka kwa kunieletea mwanaume wa ndoto zangu, ana mali, biashara na ananijali,mkewe na watoto wake itabidi wajikaze mimi siwezi kupishana na bahati"
4. Zamani: Mwanamke anakutana na kijana amehitimu masomo ila hana ajira na anajitafuta. " Hongera kwa kumaliza masomo,usijali, MUNGU atatufungulia njia huko mbeleni tutapata mali kwasasa tujibidiishe na maisha".
Sasa : " mmmmmmmmmn sasa mwanaume hauna hela,hauna kazi unanitaka utanihudumiaje kwa mfano, au unataka ukanifubaze nichakae ndio ufurahi? We kuweza"
5. Zamani : mwanamke akienda nyumba ya ibada. " MUNGU baba naomba unilinde na kuniweka mbali na vishawishi na uovu wa shetani,nilinde huu mwili wangu na hiii bikra yangu hadi ndoa niwe mke mwema na kuishi kwa namna ya kukupendeza"
Sasa : " eeeeh Yesu naomba uningezee tako , shepu na rangi ya mtume ili wanaume wakiniona wachanganyikiwe,nisamehe kwa kutoa mimba ya tatu niliogopa kuzaa mtoto asiteseke. Naomba unipe mume handsome,mrefu,rangi nzuri,ajue kuvaa,awe na hela nyingi,kwao wawe matajiri,awe wangu pekee yangu anipende pekee yangu.
Kwa kifupi wamebadilika sana.