Wanawake wenzangu Ebu tutete kidogo hapa!

Heloo

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
4,227
2,000
Wasalaam!
Kutokana Na malalamiko mengi mengi ya mahusiano Nimegundua ya kwamba matatizo mengi yanatokana Na wanaume.
Kwanza kabisa Ni kutojali kwao pia Na kuwachukulia wanawake kama vyombo vya starehe, kwamba anaweza akamchukua huyu, akamwacha. Hata kwa kosa Dogo, anatafuta sababu anaenda tongoza kwingine Na ahadi za ndoa fasta, Na mdada mgeni bila kujua akisikia ndoa anavua bila shida. Baadaye Tena anamwacha.A nafanya mchezo huu kisa aliumizwa nyuma.Makosa ya wengine yanahamishiwa kwa wanawake wengine.Wakipata mimba huyo huyo tena,anakuja kuanzisha thread kwamba ' masingle maza Sio'
Je wanawake wenzangu kifanyike kitu gani Na Je ukiwa.Na mpenzi hana matatizo ya Hapo juu ila hakujali kwa maana ya Huduma kisa unafanya kazi Na kwa kuwa humuombi pesa au Huduma yoyote Ndo kwanza anakusifia Eti ' you are a wife Material' Na wewe kwa kuwa unaogopa kubadilisha badilisha unakomaa Na shida zako maskini. Ivi akija tokea wa kukushika mkono atakuja lalamika kweli???
Mbona hawa wanaume wanajisahau sana?? Halafu wanaume wabahili wana Mawivuuu hatari.Eti nikuhudumie Mimi baba ako? Ndo maneno yao.Haya kama Ni hivyo.Msilalamike.
Narudia swali kwa wanawake wenzangu.Wanaume wa hivi Huwa mnawafanyaje?? Na Je kazi ya Mwanaume kwa mwanamke Ni nini hasa_????? Majibu.
 
Mgibeon

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
8,889
2,000
Dah, Mistake ya kwanza unayofanya ndio hii, hakuna kitu kibaya kama muda huu jamaa kalala wewe unashika simu na kuandika Uzi, halafu unakuja kusema wanaume Ni chovya chovya!

Samahani lakini, Mimi sio mwanamke, nilikua napita Tu japo nitoe "Hi" kwa mbali ILA nilipoona mada inatuhusu na sisi nikaona sio mbaya japo na Mimi ninene machache, samahani lakini.

a
 
Usijali.Wangu muda huu hayupo kasafiri.Usihofu.Ila kwa nini mnatesa wanawakeeee! Enyi viumbe!!!!
 
Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
3,626
2,000
Daah!! Nyie kinadada
Hivi hii kauli eti "wanatutumia kama chombo cha starehe" mnakuwa na maana gani hasa??
Hivi kwani nyinyi huwa hamustarehe katika ule mchezo??
Inamaana nyie kwenu ule mchezo ni karaha kwenu.???

Mnipe majibu hapa sio kila siku mnatulalamikia tu bila sababu wakati hiyo kitu imeumbwa kwa ajili ya kazi hiyo.
 
Ni Ivi.Badala ya uwe Na mmoja mjenge familia Kimara Na kuvumiliana Wakati wa shida Na raha.Wewe unamjaza mimba, angali anarambaramva malimao Na kichefuchefu unatunga uongo' jeuri, ana kiburi, anaomba hela sana. N.k.Unamtelekeza unaenda kwa ' she' mwingine.Nako unatoa kasorooooo.Unawapitia kama 10 kwa mwaka.Hapa Ndo ' dhana ya ' kama chombo cha starehe!!!!! Why doing this to Innocent women?????
 
Mgibeon

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
8,889
2,000
Usijali.Wangu muda huu hayupo kasafiri.Usihofu.Ila kwa nini mnatesa wanawakeeee! Enyi viumbe!!!!
Mkuu, mateso ya mwanamke yanatokana na mwanamke mwenyewe! Shida Ni kwamba wanawake mna ghubu Sana, yaani kila kitu Ni LAWAMA na KUNUNG'UNIKA Tu, what do expect? Yaani Kuna muda unajiulizaa inamaana huyu mwanamke haoni jitihada zangu za kujenga huu uhusiano/ndoa hata kidogo.?

So ugomvi/Mateso/Hekaheka za mahusiano Ni "wewe mwenyewe Tu". Ukiamua kuishi kwa Amani na furaha Ni "wewe mwenyewe Tu".

Ingawa PIA wapo wanaume wachache ambao Hua wanalewa upendo WA mwanamke na kuutumia vibaya, na hawa Mara nyingi huandamwa na KARMA, so hawa wasikupe kuwaza, its a matter of time Tu.

NB; utamu wa pipi mate yako mwenyewe, remember; A man can build a house but without a woman it can not be a home.
 
But..Causative wa mateso mengi Ni Mwanaume.Ebu fanyeji kama forum ya Wanaume mjirekebishe.Mnawaliza sana wanawake.Hatukatai.Kuna makosa wadada, wamama wanatenda but fatiliaaaa chanzo.Ni ninyiiiii!
 
Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
3,626
2,000
Ni Ivi.Badala ya uwe Na mmoja mjenge familia Kimara Na kuvumiliana Wakati wa shida Na raha.Wewe unamjaza mimba, angali anarambaramva malimao Na kichefuchefu unatunga uongo' jeuri, ana kiburi, anaomba hela sana. N.k.Unamtelekeza unaenda kwa ' she' mwingine.Nako unatoa kasorooooo.Unawapitia kama 10 kwa mwaka.Hapa Ndo ' dhana ya ' kama chombo cha starehe!!!!! Why doing this to Innocent women?????
Kwahiyo wanawake ndo huwa wanatulia na mwanaume mmoja???
 
Heloo

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
4,227
2,000
Kwahiyo wanawake ndo huwa wanatulia na mwanaume mmoja???
Fatilia.Mwanamke akimpenda Mwanaume anatulia Tena sana, Mapenzi ya wanawake yapo moyoni.Tofauti Na ninyi yapo machoni( ninyi mnatamani tu kwanza)Kwa nn mwanamke anaanza kubadilika Bdy? Ni kutokana Na mabadiliko anayoanza nayo Mwanaume Baada ya kuanza kuhangaika Na michepuko Na kumpuuzia. Mapenzi ya mwanzo Mwanaume anayaamishia kwa michepukwaaa!sasa huku Na huku. Changes zinaanza.Ushauri.Wanaume badilikeni.Mtaona mambo yanatulia.Mwanamke ukimpatia hakika utaishi Paradiso angali upo Duniani.Kwa sababu kama tabia hizo utamfanyia mwanamke huyu, unakimbia unaenda kwa mwingine unafanya the same, mwisho wa siku utawachukia wanawake maana wanawake wana hulka moja.Jitahidini kuwaenzi wake/ wapenzi Wenu.
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
5,658
2,000
Hapo pa wanaume wabahili{mkono wa birika} eana wivu balaa, naunga mkono hoja.
Kwani mke amekuwa umeme, kwamba utazimika usipolipa bill ? Muono finyu wa kuwaza leo unawaponza. Eti mkono wa birika !! Kama umekula na umeshiba, unataka hela ya nn ? Nguo subiri mwaka mpya, nywele fanya kuzipunguza kwa mkasi, ama jifunge mabutu (vishungi).

wanaume wengi wako worried na kesho, siyo leo. Ndiyo maana wanabana leo ili kesho ipite salama
 
Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
16,438
2,000
Mkuu mpaka sasa hivi mwanamke aliyechangia ni mmoja naye hajasema kua wanaume wana matatizo ila kaunga mkono kua watu bahili wana wivu.

Inawezekana haya maoni yako ni makubwa kushinda uhalisia.

Wanawake mkijua kama mnapendwa mnasumbua isivyo kawaida, unaongea na bwana ako utadhani unaongea na binti mwenzio kibarazani.

Wanaume shit tupo, ni marafiki zenu, kaka zenu, wadogo zenu n.k. lakini huu ushit haujatokea tu bila chanzo. Na wanaume wanaotimiza ndoto za wasichana wapo pia, usiweke wote kwenye kapu moja.

Pia ukiandika acha aya.
 
Mkereketwa_Huyu

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
7,120
2,000
Usijali.Wangu muda huu hayupo kasafiri.Usihofu.Ila kwa nini mnatesa wanawakeeee! Enyi viumbe!!!!

Wanawake wenyewe wengi hawajitambui na vicheche mno ndiyo maana wanaume hatuna Imani nanyi kwani tunajuwa mda wowote mnaweza badilika. Ya nini kuamini mtu asiye na msimamo/asiyejitambua? Jiulize kama wewe ungekuwa mwanaume na una imani kuwa wanawake walio wengi wako hivi, ungefanyaje?
 
Raphello

Senior Member
Mar 20, 2017
162
250
Ni Ivi.Badala ya uwe Na mmoja mjenge familia Kimara Na kuvumiliana Wakati wa shida Na raha.Wewe unamjaza mimba, angali anarambaramva malimao Na kichefuchefu unatunga uongo' jeuri, ana kiburi, anaomba hela sana. N.k.Unamtelekeza unaenda kwa ' she' mwingine.Nako unatoa kasorooooo.Unawapitia kama 10 kwa mwaka.Hapa Ndo ' dhana ya ' kama chombo cha starehe!!!!! Why doing this to Innocent women?????
Ukimpata mtu sahihi unatulia tu, tatizo watu wana haraka ya tunda ndio matokeo yake hayo. Kwa sasa Hakuna wa kumlaumu, si mwanamke wala mwanaume kila mtu ana mapungufu yake ni kamuomba Mungu akujalie upate ambae mtaendana.
 
Raphello

Senior Member
Mar 20, 2017
162
250
Wanawake wenyewe wengi hawajitambui na vicheche mno ndiyo maana wanaume hatuna Imani nanyi kwani tunajuwa mda wowote mnaweza badilika. Ya nini kuamini mtu asiye na msimamo/asiyejitambua? Jiulize kama wewe ungekuwa mwanaume na una imani kuwa wanawake walio wengi wako hivi, ungefanyaje?
Kuna dada alishawai kuniambia et angekuwa mwanaume angekuwa anawa*some text missing*mba.,kumbe wenyewe ndo chanzo afu wanatulaumu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom