Wanawake wenye pesa ndio wenye True love

Jokajeusi

JF-Expert Member
Jun 1, 2018
6,305
10,582
Wakuu!

Huu ni utafiti Rasmi nilioufanya mimi mwenyewe kwa miaka mitano.

Utafiti wangu niliuweka kwa mtindo wa swali; WANAWAKE WAPI NDIO WENYE MAPENZI YA KWELI?

Muda wa Utafiti: Miaka Mitano
Sampo ya wafanyiwa Tafiti: Mia moja thelasini
Maeneo ya Utafiti: Dar es salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Mtwara, Kigoma na Morogoro, Tanzania. Mombasa, Nairobi, na Kisumu, Nchini Kenya. Sokoto, Osun, na Lagos, Nchini Nigeria. Adelaide, Sydney, na Melton nchini Australia.

Jokajeusi nimegundua kuwa, wanawake wenye pesaa au wenye unafuu wa maisha, waliotoka kwenye familia bora wengi asilimia 95% wana mapenzi ya dhati kabisa.
Asilimia tano iliyobakia ndio wamenipa matokeo kuwa hawana mapenzi ya kweli.

Kupitia utafiti wangu ambao nimeshiriki mwenyewe kwa asilimia 80%. nimegundua kuwa, wanawake wenye fedha wana tabia kuu zifuatazo;
1. Wana roho nzuri
2. Wana msimamo na wavumilivu
3. Wanyenyekevu halisi
4. Waaminifu

Sampo ya wanawake niliowafanyia utafiti ni 130. Wanawake masikini wakiwa 65 sawa na asilimi 50%, na wanawake wenye vipato wakiwa 65 sawa na asilimia 50%

Wanawake matajiri 60 kati ya 65 wamenipa matokeo ya tabia tajwa hapo juu. Ndoa zao ni nzuri, wamekuwa waaminifu kwa waume zao, wavumilivu, wana roho nzuri jambo ambalo unaweza ukadhani utapata papuchi kirahisi lakini utakapojichanganya hapo hapo wanaku-crash.

Kikosi changu cha utafiti kilihusisha vijana wa namna zote, vijana wajanja wenye kujua kushawishi, wazee na vijana wenye pesa ili kuwalaghai wanawake hao wenye pesa lakini kati ya wanawake 65 wenye pesa wanawake watano tuu ndio waliingia mkenge wakashawishika.

Tulitumia pesa, akili, ujanja wa kila namna, watu mashuhuri, pia hata wanaume walioigiza umasikini tuliwatumia ili kuona uhalisia. Muda wa kushawishi kwa kila mwanamke tulitumia miezi sita tuu.

Hii ni tofauti na Kundi l wanawake masikini au wenye vipato duni. Kwenye wanawake masikini 65 ambao tulipima kiwango chao cha uaminifu na mapenzi ya dhati kwa wapenzi wao au waume zao. wanawake masikini 58 kati ya 65 walisaliti wapenzi wao. Hii ni kusema wanawake saba tuu waliomasikini ndio walikuwa waaminifu na wenye mapenzi ya dhati kwa wapenzi wao. Tulipanga kundi nalo tutumie miezi sita lakini wanawake 56 waliisaliti ndoa au mahusiano yao chini ya miezi mitatu, wawili tuu ndio walizidi miezi mitatu, mmoja akijitahidi kukataa mpaka mwezi wa nne, na wa mwisho akifurukuta mwezi wa sita na kutimiza idadi ya wanawake 58 masikini walioshindwa kulinda penzi lao.

Utafiti huu umedhihirisha kuwa wanawake masikini hata wanapoolewa na watu wenye vipato bado wanakuwa sio waaminifu. Kwa mfano; Kwenye wanawake masikini 65, waliokuwa wameolewa na watu wenye vipato vikubwa walikuwa 22, lakini wote hao waliishia kusaliti ndoa zao licha ya kuwa waume zao wanavipato vikubwa.

Zingatia, wanawake masikini ni wale ambao wanamtegemea mume wake au mchumba wake asilimia 80%, kundi la wanawake lisilo na kazi ya uhakika, kundi la wanawake ambalo limetokea jamii fukara, na kundi la wanawake ambalo linaelimu duni, hao ndio tumewa-term kama wanawake masikini.

Katika Utafiti wangu na timu yangu tumegundua Kundi la wanawake masikini limejibainisha kwa sifa kuu zifuatazo;
1. Ubinafsi, Wanawake masikini wote 65 walikuwa na mtazamo wa cha mwanaume ni cha wote na cha mwanamke ni chake yeye mwenyewe.
2. Kutokuwa waaminifu katika ndoa. Wanawake masikini zaidi ya 53 wanamtazamo wa mafiga matatu, kwamba mwanamke sharti awe na mwanaume zaidi ya mmoja kwa mahitaji yake. kumi na mbili waliobaki hawana mtazamo huo
3. Ushirikina na uchawi. Wanawake masikini 61 walikiri kuwahi kushiriki mambo ya kichawi na ushirikina. wanne hawakuwahi. Pia wanawake masikini 56 wanaabudu zaidi na kuamini katika dini za miujiza bandia.

Hii ni tofauti na wanawake matajiri wenye vipato ambapo 27 ndio waliwahi kushiriki mambo ya uchawi na ushirikina huku 38 wakisema hawajawahi. Wanawake matajiri 57 husali katika dini kubwa kama Ukatoliki, Ulutheri, Usabato na dini ya kiislamu. Huku nane wakibakia kwenye Madhehebu madogo yaliyozuka na upako za manabii na mitume.

Wanawake masikini 61 walienda kwa waganga kuwaloga waume zao ili wawape pesa yaani wasigeuze kauli waombwapo pesa. Kumbuka idadi hii ndio ile ile ya wanawake masikini 61 waliowahi kwendaa kwa waganga wakienyeji.

Wakati wanawake tajiri 27 walienda kwa waganga kwa ajili ya kuwaloga waume na wapenzi wao wawapende zaidi na waume zao wasiwe na vimada vya nje.

4. Ulimbukeni wa kudandia mambo mathalani mambo ya mitindo
Wanawake masikini ndio wanaongoza kwa kwenda na wakati kuliko wanawake matajiri.
Wanawake matajiri ndio wanaongoza kwa kuwekeza kwenye uchumi wa familia

Wanawake masikini ndio wanaongoza kushobokea wanaume mashuhuri na wenye hadhi kubwa.

Tulifanya utafiti mdogo jijini Nairobi kwa wanawake 18, tisa wakiwa na vipato vikubwa, tisa wakiwa fukara.
Tukaita wasanii wakubwa wawili, mmoja ni msanii mkubwa Tanzania na wa pili ni msanii wa mkubwa wa kike wa Kenya. Tulipowaita wanawake hao 18 ili waonane na wasanii hao wakubwa wawili, wanawake 9 masikini walitokea wakiwa wamejiremba haswa, alafu wanawake 2 tajiri ndio walioitikia wito. Hivyo masikini ilikuwa 9;9, matajiri ni 2;9.

Katika kukutana na wasanii, wanawake masikini walionekana kupagawa na kushindwa kuzuia hisia zao, huku wanawake tajiri wakichukulia ni kawaida.
Wanawake masikini waliweza kuhatarisha mahusiano yao ya kindoa kwa sababu tuu ya kuja kuonana na wasanii.

Kufupisha habari,

Imebainika kwamba, mwanamke mwenye kipato anamapenzi ya dhati maradufu ukilinganisha na mwanamke masini.

Jokajeusi
 
Samahani mkuu....
Hivi mtu anaposema mwanamke mwenye pesa, maana yake awe na kuanzia kiasi gani..??

Awe na uwezo wa kuendesha maisha yake, ya watoto wako na hata mumewe kama ataumwa maisha yake yote bila kuomba msaada kwa mtu. Huyo anapesa.
Na hapa nazungumzia kula mlo kamili, kuvaa nguo nzuri, kuishi kwenye makazi mazuri.

Sio mtu anakulisha kila siku majani kama mbuzi wake alafu anakuambia anakulisha au analisha watoto, huko sio kulisha bali kufuga
 
Awe na uwezo wa kuendesha maisha yake, ya watoto wako, na hata mumewe kama ataumwa maisha yake yote bila kuomba msaada kwa mtu. Huyo anapesa.
Na hapa nazungumzia kula mlo kamili, kuvaa nguo nzuri, kuishi kwenye makazi mazuri.

Sio mtu anakulisha kila siku majani kama mbuzi wake alafu anakuambia anakulisha au analisha watoto, huko sio kulisha bali kufuga
Sawa mkuu
 
Hivi unajua lakini wanawake wenye pesa walivyo kuwa wajeuri mr joka hawa viumbe wakiwa na cha kujivunia kwa mfano elimu,pesa,au uzuri my friend mapenzi waga mazuri yakiwa mapya ila mkizoeana ujipange maana huna la kumwambia akatishika
 
Hivi unajua lakini wanawake wenye pesa walivyo kuwa wajeuri mr joka hawa viumbe wakiwa na cha kujivunia kwa mfano elimu,pesa,au uzuri my friend mapenzi waga mazuri yakiwa mapya ila mkizoeana ujipange maana huna la kumwambia akatishika

Mkuu ujeuri wa mwanamke ni kwa sababu ya athari za ufukara
Ni kama vile mwanaume, ukimuona ni jeuri na anadharau kwa sababu ya pesa basi jua kuwa chimbuko lake ni masikini, anaathari za ufukara.

Wanawake wenye pesa watamu bhana, acheni masihara.

Lakini vimasikini ni vijeuri, yaani vinachukulia ujeuri ndio kujiamini

Shida ya wanawake matajiri ni kuwa wanapenda mwanaume usiwe mtu wa michepuko, hapo mtaendana sawa.

Angalia hata majini, ukipendwa na jini lazima uwe tajiri, shida inakuja halitaki ku-share, likigundua unacheat hakuna rangi utaacha kuona
 
Back
Top Bottom