Wanawake wengine wanawezaje kumaintain miili yao baada ya kujifungua?

Njaa haiishi bila plates mbili za wali :D
Mungu anitie nguvu kwakweli
Kawaida mamy. Ni ngumu ila jitahidi tu. Mi nilifanikiwa kutokana na support ya mtu wangu wa karibu. Ikafikia hatua nikawa napakuliwa chakula "kiduchu" ili kuniepusha nisile sana. Nikaambiwa naweza kula hata baada ya nusu saa japo sikuweza tena kula ndani ya huo mda mfupi. Baadae nikazoea. Nikila kidogo natosheka. Mwili ukawa vizuri.
 
Mimi nilipojifungua nilikua nimejaaa hatari ile week ya kwanza nyonyo,tumbo la uzazi nalo kulee. Ila from day one nilikua nakunywa mno majii mengi hata lita tatu na zaidi kwa siku na chakula ni ndizi ndizi tuu huwezi amini wiki ya tatu nilikua mdogo kila kitu kiliisha. So i hope maji mengi ni tiba muafaka na kula chakula kidogo haijalishi ni wanga au whatever.
 
Njia rahisi na natural Zaidi ni mazoezi ya tendo a ndoa na uzingatie ulaji wako, maana kuna wanawake wengine wanakuambia wako kwenye diet ila anakunywa debe zima la bia na kitimoto kila siku.
 
Njia rahisi na natural Zaidi ni mazoezi ya tendo a ndoa na uzingatie ulaji wako, maana kuna wanawake wengine wanakuambia wako kwenye diet ila anakunywa debe zima la bia na kitimoto kila siku.
Mazoezi ya tendo la ndoa?? Hebu fafanua mkuu
 
mm najiuliza pia.
maana mm nna ziwa jamani na sijazaa hata mtoto mmoja... ila kifua changu huwezi kifananisha na cha Hamisa,fayvanny ..hata zari bado ana kifua kidogo kwangu jamani...
hata nikishika watoto wa watu wanaonekana wangu... nakosa hadi wachumba maana wanadhani labda single maza ,au mke wa mtu
mm hata sijui nifanyaje

Usiwe na wasiwasi utapata mume anayependa ziwa kubwa. Kumbuka kila mtu ana mtuwe aliyepangiwa na Mungu.
 
Huwa najiuliza wanawezaje? Wakati wa ujauzito mwili upo vile vile, akijifungua mwili upo vile vile, je hawali sana? Kama hawali mtoto anapaje maziwa?

Mfano Hamisa mobeto, napenda jinsi alivomaintain mwili, msaada tafadhali mwenzenu nmekua na mkono kama wa John Cena, sijui muda unavoenda nitakua kama sim tank hata sielewi
Nb: mazoezi yawe ushauri wa mwisho jamani make ni kipaji, nami sina hicho kipaji. Picha za before and after zinakuja.....

View attachment 690959
View attachment 690961
Tuanzie hapa, wewe ni single mom au married??
 
sawa nakula sana yani nakula ile mbaya, tatizo mwili nao huooo, wengine huwa hawali nataka kujua hapo kwanini hawaongezeki
wanakula kawaida sio into large quantity,kina mama wengi husingizia wananyonyesha so nao hupakia kweli kweli,mwili hauhitaji vyakula vyiingi sana balikwa kiasi na ndo maana kila kinachozidi kinahifadhiwa kama mafuta mwilini haijarishi ulikula mafuta au wanga au protein
 
Mie hata sisingizii kwakweli kwa nnavochukia unene plus kitambi huwa nipo tayari kushinda hata njaa , wiki mbili za mwanzo nlikua nakula kidunchu mwili fresh maziwa hakuna sasa si kumtesa Mtoto
 
Huwa najiuliza wanawezaje? Wakati wa ujauzito mwili upo vile vile, akijifungua mwili upo vile vile, je hawali sana? Kama hawali mtoto anapaje maziwa?

Mfano Hamisa mobeto, napenda jinsi alivomaintain mwili, msaada tafadhali mwenzenu nmekua na mkono kama wa John Cena, sijui muda unavoenda nitakua kama sim tank hata sielewi
Nb: mazoezi yawe ushauri wa mwisho jamani make ni kipaji, nami sina hicho kipaji. Picha za before and after zinakuja.....

View attachment 690959
View attachment 690961
Oh jamani Eve, pole kwa changamoto hiyo ya mwili. Kwa ushauri kama mazoezi ni kitu kigumu sana kwako jaribu diet, badilisha mfumo wako wa ulaji ikiwa ni pamoja na kupunguza portion ya chakula, mwili huhitaji kiasi kidogo tu cha chakula uweze kusavaiv, pia (hapa ni kama mtoto ameshafikisha miezi sita kama bado kwa kweli subiri tu)
 
Mwenzio kazaa mara tano, na anajitunza mwenyewe;
zari-hassan-dangote.jpg
Mi mwenyewe nipo fresh tu bi mkubwa, na najua toto akikua ntarudi kawaida ila kwa sasa tu siupendi unene....
Na mpango wangu ni watano kama zari teh
 
Hakuna mchawi mwingine zaidi ya vyakula unavyokula.... chakula kinaweza kukukondesha na pia chakula kinaweza kukunenepesha.... Last month mange kimambi alitoa somo la diet in case kama mtu anataka kujikondesha
 
Yes utapata with lots of fluids kama juice, uji wa lishe wa maziwa na blue band, chai ya viungo, supu ya kuku, nyama, samaki etc
Ahsante ngoja nihamie huku matikiti matatu kwa siku teh
 
Kwani unakula nini? coz the more mtoto ananyonya the more utasikia njaa, na unavyovila mtoto anavimaliza kwenye maziwa, labda kama unatega kunyonyesha, lakini ukinyonyesha vizuri lazima utapungua tu.
Fanya mazoezi na uwe makini na vyakula unavyokula, maana kama unafanya mazoezi alafu ukirudi unapiga sinia na wali nyama maharage hutaka upungue tehe tehe tehe
Ugali, wali, thermos ya uji :D
Mazoezi nitadanganya labda nikianza kwenda job ntakua natembea
 
Njia rahisi na natural Zaidi ni mazoezi ya tendo a ndoa na uzingatie ulaji wako, maana kuna wanawake wengine wanakuambia wako kwenye diet ila anakunywa debe zima la bia na kitimoto kila siku.
Wakati wa kunyonyesha nyg zinakua mbali hilo tendo lipumzike
 
Back
Top Bottom